Naamka asubui naangalia wallet yangu kitandani " dah! amna kitu, Mungu wangu nimekosa nini mimi?". Hii ilikuwa sentensi yangu kila siku nilipokuwa nikiamka na nililaani sana mfumo wa nchi hii kama kijana niliyesoma na mwenye Stahasha ya Biashara ya Uhasibu( B.A. BBA-Acoounting). Nililaumu viongozi wetu ,wazazi wangu na ndugu kwa kukosa ajira ya maana. Siku moja nikajiuliza hivi ningekuwa yatima au ningekuwa mzazi wa watoto watatu ningefanyaje mbona vijana wengi wanamaduka yao, biasharaa zao kama Fredy Vunjabei na kwanini mimi siwezi. Majibu yalikuja baada ya kuamka na kutambua vijana wengi tunaangamia kwa;
- Kukaa mitaani na kusikiliza maneno ya watu ambayo ayajengi wala hayaleti chakula kichwani mwetu.
- Kubeti kila siku, Kubeti sio kosa ila je unapata fedha ya kujikimu na mahitaji yako unayapata kwenye kubeti.
- Ideology mbaya ya kuajiliwa kwa waliosoma .
- Maneno ya kukatishana tamaa ya mbona huyu kashindwa, je wewe utaweza?
- Kukalia mambo ya simba na yanga, Diamond na Alikiba au ManU na ManCity. aya yote hayawezi kuleta chakula kichwani mwako.
- Jifunze kuweka budget yako vizuri na punguza matumizi ambayo hayana umuhimu.
- Jifunze kutunza kila kiasi kidogo ata 500/= kwenye kibubu au M-pesa, Tigopesa maana kutunza kwako leo kunaweza kukuinua miaka ijayo.
- Kuna baishara nyingi za kufanya zinazohitaji mtaji mdogo mfano ufugaji wa kuku, nguruwe au kilimo.
- Andaa proposal yako au mwone mtaalamu yeyote wa biashara akusaidie na unaweza kwenda Benki au mashirika yanayojishugulisha na biashara na wanaweza kukukopa mtaji kwa muda mrefu na ukasimama.
- Hii ni kubwa kuliko vyote, mkumbuke muumba wako kila saa na kila muda.