Amkata mkewe mkono kwa wivu wa mapenzi

Amkata mkewe mkono kwa wivu wa mapenzi

dope bwoi

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2009
Posts
236
Reaction score
602
Shinyanga. Mkazi wa Bushushu mjini Shinyanga, Debora Rwekwama (34) amekatwa mkono wa kushoto na mumewe, Jacob Mwajenga (35) ikidaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9, 2021 mtaa wa Bushushu manispaa ya Shinyanga.

Amesema mwanaume huyo alimkata mkono Debora baada ya mwanamke huyo kuzimia kwa kipigo.

"Inadaiwa mwanaume huyo mchana alikwenda benki (inayodaiwa mkewe kufanya kazi)hakumkuta mkewe lakini alikuta mkoba wake katika ofisi na aliporejea alitaka kuanzisha vurugu lakini wakamshauri ugomvi wao wakaumalize nyumbani."

"Walipofika nyumbani waliendelea na ugomvi na alimpiga sana mkewe hadi akazirai. Alichukua kisu na kumkata mkono inaonekana zilitoka damu nyingi. Mkewe akiwa amezimia huyu mwanaume alimbeba na kumpakia kwenye gari na kwenda wilayani Kahama katika kituo cha polisi na kuripoti kuwa amepata ajali. Kwa sababu Debora alikuwa hawezi kuongea hawakumhoji huhu mwanaume walimpa PF 3 ili aweze kutibiwa lakini hawakujua kama ni mke wake."

"Alipomfikisha hospitali madaktari walifanya uchunguzi wao na kugundua kuwa hajapata ajali bali amepigwa na walitoa taarifa polisi wilaya ya Kahama ambao walimkamata mhusika ambaye shughuli yake ni kuongoza watalii huko Arusha na kutokana na changamoto ya corona alikuwa nyumbani tu, nadhani ndio wivu ulipoanzia hapo, "amesema Kyando.
Mwananchi News
 
Kuna wivu na kuna USALITI WA MAPENZI/NDOA. Siyo kila tukio linatokana na WIVU mengi ni USALITI NA KUTOKUWA WAAMINIFU. Hususani kizazi hiki UKAHABA(Prostitution/Kudanga) imekuwa ufahari.
 
Wivu wa mapenzi ni hatari sana,sasa umekamatwa unaenda ndani bado umtibu uliyemjeruhi,muda unapotea,stress zinakuandama,Eeh Mungu tunusuru viumbe wako.
 
Tukumbuke kuziombea ndoa zetu wadau maana hakuna sehemu shetani anaisaka kwa udi na uvumba kuiteketeza kama ndoa.

Tatizo si umepata Mke mwema wala Mume sahihi, bali namna ya kuyaishi maisha yanayotafsiri ndoa kama ilivyoasisiwa na Mungu pale bustanini Eden.
 
Jamaaaa kazingua sana asingempiga na kukata mkono,alitakiwa wakayamalize home kwa SHOW moja matata, full makamuzi ya kukomoa,mixture kusimamia ukucha break pu***bu....yaani okomandoo wote.
 
Vipi ikiwa siri ya ndani mwenye mali huwa hapewi haki yake ya tendo la ndoa zaidi ya siku kadhaa au miezi?
 
Sasa ndo inaitwa kubaka mkeo,unakatamata kwa nguvu,binua kwa hasira zote na kupiga miti mpaka akome......hamna namna kamanda.Alafu akashtaki amebakwa,watamshangaa hata yeye atajishtukia.
... hakuna kitu kinaitwa KUBAKA kwenye kitanda cha ndoa! OK, watamshangaa kweli!
 
Hiyo move ya kwenda kufuatilia kazini imeendeshwa na wivu, huenda kuna shilawadu walikuwa wanapenyeza ubuyu au alihisi mabadiliko katika mienendo na tabia, pia ile dili zake za kazi zinazomuingizia mshiko kuingia mushkeli kulimletea intimidation fulani mbele ya mkewe.....vijana wekeni michongo ya kutafuta fedha mapema kuepuka mitihani kama hii..
 
Hii kesi imejirudia iko kama ile iliyotokea arusha

Ova
 
Tukumbuke kuziombea ndoa zetu wadau maana hakuna sehemu shetani anaisaka kwa udi na uvumba kuiteketeza kama ndoa.

Tatizo si umepata Mke mwema wala Mume sahihi, bali namna ya kuyaishi maisha yanayotafsiri ndoa kama ilivyoasisiwa na Mungu pale bustanini Eden.
Ameongea jambo kubwa sana, shetani anahangaika sana na ndoa maana ndio msingi wa kila kitu. Akishavuruga hapo kazi yake inakuwa rahisiii.
 
Anachotaka shetani. Kuona watu waamini kuwa ndoa ni ngumu na hakuna ulazima wa kuoa au kuolewa.
Tunamuacha sana Mungu na ndiyo matokeo yake hayo.
Mwanaune upo tu nyumbani na hauna kazi.
Atakayekuvumilia ni mama yako mzazi tu lkn hao wengine hawawezi kukuvumilia.
Tukumbuke kuziombea ndoa zetu wadau maana hakuna sehemu shetani anaisaka kwa udi na uvumba kuiteketeza kama ndoa.

Tatizo si umepata Mke mwema wala Mume sahihi, bali namna ya kuyaishi maisha yanayotafsiri ndoa kama ilivyoasisiwa na Mungu pale bustanini Eden.
 
Anachotaka shetani. Kuona watu waamini kuwa ndoa ni ngumu na hakuna ulazima wa kuoa au kuolewa.
Tunamuacha sana Mungu na ndiyo matokeo yake hayo.
Mwanaune upo tu nyumbani na hauna kazi.
Atakayekuvumilia ni mama yako mzazi tu lkn hao wengine hawawezi kukuvumilia.
Sahihi kabisa Chifu, ndipo maana halisi ya lile agizo " Wanaume tule kwa jasho" yani hakuna kupendwa ikiwa hauna chochote kifuta jasho sababu Mwanamke anahitaji matunzo.
 
Back
Top Bottom