Amkata mkewe mkono kwa wivu wa mapenzi

Amkata mkewe mkono kwa wivu wa mapenzi

Masikini Debora,angeolewa na mimi asingepata haya.

Ila simjui
 
Shinyanga. Mkazi wa Bushushu mjini Shinyanga, Debora Rwekwama (34) amekatwa mkono wa kushoto na mumewe, Jacob Mwajenga (35) ikidaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9, 2021 mtaa wa Bushushu manispaa ya Shinyanga.

Amesema mwanaume huyo alimkata mkono Debora baada ya mwanamke huyo kuzimia kwa kipigo.

"Inadaiwa mwanaume huyo mchana alikwenda benki (inayodaiwa mkewe kufanya kazi)hakumkuta mkewe lakini alikuta mkoba wake katika ofisi na aliporejea alitaka kuanzisha vurugu lakini wakamshauri ugomvi wao wakaumalize nyumbani."

"Walipofika nyumbani waliendelea na ugomvi na alimpiga sana mkewe hadi akazirai. Alichukua kisu na kumkata mkono inaonekana zilitoka damu nyingi. Mkewe akiwa amezimia huyu mwanaume alimbeba na kumpakia kwenye gari na kwenda wilayani Kahama katika kituo cha polisi na kuripoti kuwa amepata ajali. Kwa sababu Debora alikuwa hawezi kuongea hawakumhoji huhu mwanaume walimpa PF 3 ili aweze kutibiwa lakini hawakujua kama ni mke wake."

"Alipomfikisha hospitali madaktari walifanya uchunguzi wao na kugundua kuwa hajapata ajali bali amepigwa na walitoa taarifa polisi wilaya ya Kahama ambao walimkamata mhusika ambaye shughuli yake ni kuongoza watalii huko Arusha na kutokana na changamoto ya corona alikuwa nyumbani tu, nadhani ndio wivu ulipoanzia hapo, "amesema Kyando.
Mwananchi News
Being single is really cool
 
Debora hana mkono tena na alikuwa mfanyakazi wa bank. Je atasimamishwa kazi ilhal mume hana kazi yupo tu home na tiyari ana kesi..
 
Adhabu tu sheria kali zichukuliwe, kitendo alichofanya huyo jamaa siyo cha utu kabisa, alikuwa na uwezo wa kuachana nae kuliko kumkata mkono, labda kama sheria ingeruhusu saa hivi na yeye alitakiwa awe amekatwa mkono.
 
Back
Top Bottom