Amnesty International: Kenya, Tanzania Miongoni Mwa Wakandamizaji Wapinzani

Remark

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2015
Posts
510
Reaction score
989
Hili ni tatizo kwa nchi nyingi sana hapa Africa huku nikishangaa jamaa wa kaskazini wakitusema wakati mambo ni yale yale tu hata kwao.

Amnesty International
Kenya na Tanzania zimetajwa katika jumla ya nchi za kiafrika ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuwakandamiza wapinzani na kunyongesha uhuru wa kujielezea.

Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, limesema mwaka 2016/17 uligubikwa na wimbi la uvunjifu wa haki za binadamu.

Pia limeeleza kuwa watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari, kwa mfululizo, wameendelea kukabiliwa na vitendo vya uvunjifu wa amani.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa haki ya uhuru wa kujielezea ilikabiliwa na mmomonyoko mkubwa pamoja na wimbi jipya la vitisho kutoka katika vyombo vya dola.

Kumekuwa na jaribio la kukandamiza wapinzani na kunyongesha uhuru wa kujielezea vilivyo jitokeza katika bara zima la Afrika, imesema ripoti hiyo.

Nchi nyingine zilizoorodheshwa katika ripoti hiyo na kuhusishwa na uvunjifu huo wa haki za binadamu ni pamoja na Botswana, Burundi, Cameroon, Chad, Côte d’Ivoire, Gambia,Mauritania, Nigeria, Somalia, South Sudan, Sudan, Togo and Zambia.

Ripoti imesema hayo ni kati ya zaidi ya matukio 177 ya watu binafsi waliouwawa kinyume cha sheria, wakati wakiwa mikononi mwa vyombo vya usalama kwa mwaka mzima (2016/17).

Nchi nyingine hizo 14 ziliorodheshwa ni kati ya zile zinazoongoza katika kukandamiza uhuru wa kujielezea na pia ukamataji wa kiholela na kuwaweka kizuizini wanachama wa vyama vya upinzani na makundi mengine.

Katika ripoti hiyo ya Amnesty International matukio mengi yameshuhudiwa katika maeneo ya pwani, na vitendo hivyo vya uvunjaji wa haki za binadamu vimekuwa vikitekelezwa kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na mashambulizi ya kundi la kigaidi la al-Shabaab.

“Kwa mujibu wa Haki Afrika, kikundi cha haki za binadamu, kulikuwa na mauaji 78 kinyume cha sheria na kutoweka kwa watu bila ya taarifa yoyote katika kaunti ya Mombasa katika miezi 8 ya kwanza ya 2016.
 
Kenya hapo imetajwa sana sana kwa ajili ya vita dhidi ya ugaidi. Kuna watu wamepoteza maisha yao kimya kimya kisa tuhuma za ugaidi.

Lakini kwa hilo la kukandamiza wapinzani lipo sana Tanzania. Kule Zanzibar ndio usipime, hadi ikatokea tishio la kunyimwa misaada.
 
Sijuwi kwanini unafikiri Kenya mko mbali kisiasa. Manual election results imeonyesha mnavyo kandamiza upinzani. Unakumbuka jubilee walivyo piga kura kibabe bungeni na ngumi zikapigwa bungeni? Hivi kuhusu maandano ya upinzani ya kupinga sheria ya uchaguzi, wapinzani walikula kichapo na police mpaka Raila akasema basi. Siasa Kenya bado sana kuitwa siasa ya demokrasia, kuna watu bado wanaogopa kujieleza kuhofia usalama wao

a7ed485387c93257e5e6b2a3f2e17d99.jpg
 
Sijuwi kwanini unafikiri Kenya mko mbali kisiasa. Manual election results imeonyesha mnavyo kandamiza upinzani. Unakumbika jubilee walivyo piga kura kibabe bungeni na ngumi zikapigwa bungeni? Hivi kuhusu maandano ya upinzani ya kupinga sheria ya uchaguzi, wapinzani walikula kichapo na police mpaka Raila akasema basi. Siasa Kenya bado sana kuitwa siasa ya demokrasia, kuna watu bado wanaogopa kujieleza kuhofia usalama wao

a7ed485387c93257e5e6b2a3f2e17d99.jpg

Polisi hawakua na haki ya kuzuia maandamano Kenya, maana katiba inaruhusu haki za kuandamana, tatizo ni pale waandamaji hawaifanyi kwa amani, wanalianzisha na kulia baadaye wakipokea kichapo. Lakini Bongo ndio kabisa hamna hata pa kupumua, kipindi upinzani wanaitisha maandamano, jeshi la JWTZ wakaingia kitaa eti wanafanya usafi....hehehe yaani jeshi la nchi.

Halafu kwenu hata sio maandamano tu, mumewazuia wanasiasa hata kuhutubia au kufanya siasa kwa aina yoyote ile.
 
Haya unayasema umejifunika shuka la jubilee, leo hii jaribu kuhoji rushwa zinavyo kithiri serikalini ukione, andika kashfa yoyote inayo wahusu wakubwa fulani halafu wakujuwe ni wewe ndio umeandika uwone kama utapumua siku ya pili. Kenya, bado mnajaribu, Ukitaka kutuaminisha kama mmevuka kisiasa, wengine tunawaangalia kwa jicho la pembeni. Tunajuwa kemikali gani ikichanganya kwenye siasa ya kenya inavyo weza kulipua nzima.
 
Tumeipenda wenyewe wacha tuisome namba. Nchi ya ajabu sana na ikiwa na idadi kubwa ya raia wasiojielewa na washangiliaji wa matukio ya muda.
 
Haya unayasema umejifunika shuka la jubilee, leo hii jaribu kuhoji rushwa zinavyo kithiri serikalini ukione, andika kashfa yoyote inayo wahusu wakubwa fulani halafu wakujuwe ni wewe ndio umeandika uwone kama utapumua siku ya pili. Kenya, bado mnajaribu, Ukitaka kutuaminisha kama mmevuka kisiasa, wengine tunawaangalia kwa jicho la pembeni. Tunajuwa kemikali gani ikichanganya kwenye siasa ya kenya inavyo weza kulipua nzima.

Nina uhakika hata ndani ya nafsi yako unajua tena kwa kina kwamba unyanyasaji wa Tanzania ni wa level nyingine, tofauti sana na Kenya. Huko kwenu hata kumuita rais dikteta hilo linakupeleka jela, mbunge wa Arusha ananyea debe kwa kusema ameota kumhusu rais.

Hapa Kenya rais anaambiwa vitu, kuna mengine huwa anaambiwa hadi wengine tunahisi aisei kama ingelikua mimi pangechimbika.
 
Hivi ni Kenya ya sayari ya Pluto au ni hii iliyo hapa equator? Labda uwadanganye wengine kama Kenya kuna Uhuru wa kujieleza bila mipaka. Lakini sidhani kama familia ya Willie Kimani au Alan Wadi Okengo au Robert Alai watakuelewa. Hebu Google hao watu utuambie kama unazungumzia Kenya ya equator au Kenya ya Pluto.
 
Jamaa wako sahihi kabisa hawajakosea na huu ukandamizaji nkutokana na failure of most African misleaders to realize their nation's potentials na hii itakuwa ngumu xn kwa mataifa yalyomengi barani Africa kama viongozi wana- element za ukandamizaji na unyanyasaj wa raia na vyama pinzan because the more unakandamiza na kunyanyasa raia the more you create rooms for havocs, tension and cheos within the nation and no prosperity can be achieved under such situation. Thus african misleaders should be meditative on reconstructing their nations otherwise their nations will go on punching below their performance
 
Hivi ni Kenya ya sayari ya Pluto au ni hii iliyo hapa equator? Labda uwadanganye wengine kama Kenya kuna Uhuru wa kujieleza bila mipaka. Lakini sidhani kama familia ya Willie Kimani au Alan Wadi Okengo au Robert Alai watakuelewa. Hebu Google hao watu utuambie kama unazungumzia Kenya ya equator au Kenya ya Pluto.

Thubutu!!! Yaani wewe hapo unafikiria mambo anayoyafanya huyo Robert Alai ingelikua Bongo si angekua ananyea debe leo hii.
Halafu huyo Okengo, naomba ufuate matusi aliyomtukana rais, ubadilishe na kuelekeza kwa Magu, uone utaikimbia hata hiyo computer yako.
 
Kutukana ni kutukana, cha msingi kuna watu Kenya wanafungwa na wengine wanapoteza maisha kwa kutoa yaliyo moyoni mwao. Na hapo hatujaenda kwenye watu wanaopachikwa jina la mungiki kumbe ni watu wasio na hatia kisa mtu fulani hataki kusikia wanacho sema. Halafu nashanga unataka kulinganisha Kenya na Tanzania kwenye haki za binadamu. Hebu tafuta UN human right index halafu ndio tuanze hapo.
 
Vifo vinavyotokana na mambo ya kupachikwa ugaidi ua umungiki ni mojawapo wa donda linalotuharibia jina, hilo nimekiri tangu mwanzo. Lakini kumbuka ni jambo la kawaida pale nchi inapoingia kwenye machafuko ya kigaidi, wana usalama huwa wanakurupuka na kuanza kufanya vitu vya ovyo. Leo hii Marekani wameibuka na kauli za kuzuia waislamu wa kutokea baadhi ya nchi walizozitaja.

Nakumbuka kipindi fulani Tanzania kulikua na operesheni ya kutokomeza ujangili, JWTZ waliwaibukia wanavijiji na watu walipokea kichapo cha mbwa, haikujalisha wana hatia au la. Hivyo kama nilivyosema pale nchi ikikumbwa na tatizo la kiusalama, watendaji hufanya mambo mengine hadi yanapitiliza, na hili limetokea Kenya mara kadhaa.

Lakini sasa turejelee hali ya kawaida wakati nchi ipo tulivu, hapa kwetu wanasiasa wanafanya yao, wanakusanyika na kumkashifu rais, wanampa majina ya kila aina. Lakini kwenu, hata kuota ndoto kumhusu rais inabidi uishie jela kama yule mbunge wa Arusha. Kuna yule anaitwa Tundu Lissu naye jela imekua kama nyumbani kila akitoa tamko dhidi ya rais, huwa ananikumbusha Besigye wa Uganda ambaye kila uchaguzi huwa inabidi kujiandaa maana lazima anyee debe. Niliona wapinzani hata kutoa misaada kwenye wahanga wa tetemeko la ardhi waliishia matatani.

Kwenu hapo hata mkuu wa mkoa anatoa tamko kwamba ana uwezo wa kukuhamisha Dar wakati wewe ni Mtanzania na una uhuru wa kuishi popote. Hebu ndio ujue mpo mbali sana kufikia level yetu, mwambie gavana wa Nairobi bwana Kidero atoe tamko kama hilo ndio uone shughuli yake.
 
Tena umesema vizuri kwamba ikitokea hali ya hatari kama magaidi, vyombo vya usalama vinatumia mbinu ambazo watu wa kawaida hawajazizowea. Lakini je, machafuko ya 2008 yaliletwa na magaidi? Madaktari kufungwa jela kwasababu za kisiasa na huo ni ugaidi? Mimi sioni unachokiona wewe, Kenya ya leo sio Kenya iliyoshiba demokrasia, rushwa ya kisiasa bado ipo juu, madaraka ndani ya chama au hata serikalini ni lazima uwe karibu na kundi la watu wa aina fulani. Wananchi wa kawaida wanashindwa kuona faida ya katiba mpya, matatizo mbayo katiba mpya ilitakiwa kuyatatua, ndio yaliozidi kuwatafuna hao wananchi. Mishahara ya wanasiasa inazidi kuongezeka, Wakati vijana wa juakali hata leseni ya kibanda chake watu wana wakamua pesa.

Bado nashidwa kuelewa hiyo siasa ya Kenya iliyoipita Tanzania iko wapi? Ikiwa wanasiasa wanaweza kuamka asubuhi na kuandikisha chama cha siasa kesho ukakiweka kwenye uchahuzi na ukashinda, utatowa wapi muda kwa wananchi kuweza kuwasoma wanasiasa?. Tanzania itakuchukuwa sio chini ya miaka miwili kabla hijapata usajili wa kudumu wa chama cha siasa. Kenya hata kuhama chama kimoja kwenda kingine ikiwa karibu na uchanguzi ilikuwa inakatazwa mpaka mahakama ikaingilia kati na kukubali watu kuhama chama.
 
Hujaelewa na hutaelewa maana umeghubikwa, mimi namaanisha machafuko yoyote yanayofanya wana usalama kupanic lazima wataishia kufanya vitu vya ovyo. Hilo lipo dunia yote.

Lakini Bongo hata hali ikiwa shwari mumewakandamiza wanasiasa wa upinzani kiasi kwamba leo hii hata kuota ndoto kuhusu rais ni hatia, kamuulize mbunge wa Arusha kwanini alithubutu kuota.

Halafu la madaktari Kenya lilikua baina yao na mahakama, hilo unalijua japo unajitoa ufahamu.
Madaktari Bongo walithubutu kugoma kipindi fulani, kamuulize yaliyomkuta daktari Ulimboka, hehehehe!! Yaani jamaa alitekwa na kupelekwa mbugani na baada ya hapo kimyaaaaaaa!! Sasa hapa Kenya kiongozi wa madaktari anatiwa ndani siku moja kwa kukiuka agizo la mahakama halafu inaishia kuwa makelele nchi yote maana mfumo wetu upo hai.
 
Subirini TWAWEZA nao waje na utafiti wao ndiyo mtajua Tanzania tunasingiziwa
 
Kwa kuruka viunzi tuu, hujambo. Lini uliona Tanzania maiti zinaokotwa barabarani kwaajili ya siasa? Hao unao waita upinzani yupi ni mkimbizi wa kisiasa? Au kuna mkimbizi gani wa kisiasa unayemjua ametokea Tanzania? Huyo unayemtaja Dk.Ulimboko, unahuhakika gani kwamba ni serikali ndio ilimchukuwa? Je, unakubali Makaburi na yeye aliuwawa kinyama kule Mombasa na watu wa serikali ya Kenya?. Halafu umeshikilia kuhusu kesi ya mtu kuonta ndoto, hivi hapo ulipo ukitamka hadharani matamshi yanayolenga kutishia usalama wa Rais Kenyatta, unafikiri wana usalama wa Kenya watakuchekea na waendelee kukupa ruhusa ya kukaa karibu na Rais Kenyatta tena? Niambie ni nchi gani duniani au idara gani ya usalama duniani itapuuzia matamshi yanayo ashiria kutishia uhai au usalama wa kiongozi wao?
Maamuzi yakitolewa na mahakama ya Kenya unasema hayana shinikizo la kisiasa, lakini kwa Tanzania ni ya siasa, mbona unanichanganya? Kinacho nishangaza mimi, ni pale unaposema siasa ya Kenya imeendela kuliko siasa ya Tanzania, lakini unakuta ni nchi hiyo hiyo ina watu walio poteza makazi (IDP) kwa sababu za kisiasa. Utasema machafuko yaliletwa na vyombo vya usalama, lakini ukweli utabaki kuwa ukweli, tamaa ya madaraka ndio imesababisha Kenya kuwa na wakimbizi wa ndani.
 
Wakuu, endeleeni kubishana, tunajifunza mengi kupitia hoja zenu MK 254 na Mwanzi 1.
 
Polisi hawakua na haki ya kuzuia maandamano Kenya, maana katiba inaruhusu haki za kuandamana, tatizo ni pale waandamaji hawaifanyi kwa amani, wanalianzisha na kulia baadaye wakipokea kichapo. Lakini Bongo ndio kabisa hamna hata pa kupumua, kipindi upinzani wanaitisha maandamano, jeshi la JWTZ wakaingia kitaa eti wanafanya usafi....hehehe yaani jeshi la nchi.

Halafu kwenu hata sio maandamano tu, mumewazuia wanasiasa hata kuhutubia au kufanya siasa kwa aina yoyote ile.
Marekani uchaguzi ulishaisha na Trump alishinda, Je, mpaka sasa Obama na Clinton wanazunguka kufanya mikutano ya kujenga chama chao eti kwa sababu kilipokea kipigo kikubwa kuanzia Seneti mpaka House of reps au wameacha wanasubiri uchaguzi mwingine ??

- Tatizo la wanasiasa wa Kenya na Tanzania hususani wapinzani ni UBINAFSI Wanataka wao ndo tu wawe na POWER, PESA kuandamanisha raia wasiojielewa wakati wa kazi, Wamefanya SIASA kuwa AJIRA Rasmi 24/7/365 !
 
Kwa kuruka viunzi tuu, hujambo. Lini uliona Tanzania maiti zinaokotwa barabarani kwaajili ya siasa? Hao unao waita upinzani yupi ni mkimbizi wa kisiasa? Au kuna mkimbizi gani wa kisiasa unayemjua ametokea Tanzania? Huyo unayemtaja Dk.Ulimboko, unahuhakika gani kwamba ni serikali ndio ilimchukuwa? Je, unakubali Makaburi na yeye aliuwawa kinyama kule Mombasa na watu wa serikali ya Kenya?. Halafu umeshikilia kuhusu kesi ya mtu kuonta ndoto, hivi hapo ulipo ukitamka hadharani matamshi yanayolenga kutishia usalama wa Rais Kenyatta, unafikiri wana usalama wa Kenya watakuchekea na waendelee kukupa ruhusa ya kukaa karibu na Rais Kenyatta tena? Niambie ni nchi gani duniani au idara gani ya usalama duniani itapuuzia matamshi yanayo ashiria kutishia uhai au usalama wa kiongozi wao?
Maamuzi yakitolewa na mahakama ya Kenya unasema hayana shinikizo la kisiasa, lakini kwa Tanzania ni ya siasa, mbona unanichanganya? Kinacho nishangaza mimi, ni pale unaposema siasa ya Kenya imeendela kuliko siasa ya Tanzania, lakini unakuta ni nchi hiyo hiyo ina watu walio poteza makazi (IDP) kwa sababu za kisiasa. Utasema machafuko yaliletwa na vyombo vya usalama, lakini ukweli utabaki kuwa ukweli, tamaa ya madaraka ndio imesababisha Kenya kuwa na wakimbizi wa ndani.

Hehehe! Unazunguka mbuyu, lakini utafika tu, japo najua hata tukeshe hapa hutokubali kuelewa na utaendelea kujitoa ufahamu hadi ahera.
Hilo la Dk. Ulimboka sina uhakika kwamba ni serikali ilihusika, ni kwamba alitekwa nyara na kupokea kichapo cha mbwa kipindi hicho hicho yeye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari kama inavyotendeka kwetu leo. Pia sina uhakika wowote au ushahidi wa kuhusisha serikali kwenye mauaji yoyote yanayotokea Bongo, kama ile ya miili kupatikana kwenye mto Ruvu huku imehifadhiwa kwenye viroba halafu waziri wenu akasema hao walikua wahamiaji haramu.
Maiti 6 zimekutwa zikielea katika Mto Ruvu eneo la Bagamoyo huku zikiwa zimearibika vibaya | Bongo5.com
Pia kuna yule jamaa msaidizi wa Mbowe, sijui kama keshapatikana au ndio yale yale.

Huwa vigumu sana kuhusisha serikali kwenye matukio ya mauaji ya kihivi, ndio pia ilivyo Kenya. Huku kuna matukio ya watu kutoweka kimya au kuuawa, hususan wakati wana usalama wamepanic kwa ajili ya matukio kama vile ugaidi, ujangili au machafuko ya aina yoyote.

Hilo la wakimbizi wa ndani, ni picha mbovu na ya aibu Kenya na huwa tunaikemea kwa nguvu zote. Maana hutokea pale wanasiasa wanabisha matokeo ya kura na kuanzisha vurugu. Viongozi wa upinzani Tanzania ni wazalendo wasiopenda fujo, namkumbuka Lowassa alipodai kwamba kura zake zimeibwa, lakini papo hapo akawaomba wafuasi wake wadumishe amani na uzalendo. Kwa hilo nawapa heko viongozi wenu wa upinzani, viongozi wa Kenya huwa wanatibua hadi panachimbika.
 
Back
Top Bottom