Hehehe! Unazunguka mbuyu, lakini utafika tu, japo najua hata tukeshe hapa hutokubali kuelewa na utaendelea kujitoa ufahamu hadi ahera.
Hilo la Dk. Ulimboka sina uhakika kwamba ni serikali ilihusika, ni kwamba alitekwa nyara na kupokea kichapo cha mbwa kipindi hicho hicho yeye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari kama inavyotendeka kwetu leo. Pia sina uhakika wowote au ushahidi wa kuhusisha serikali kwenye mauaji yoyote yanayotokea Bongo, kama ile ya miili kupatikana kwenye mto Ruvu huku imehifadhiwa kwenye viroba halafu waziri wenu akasema hao walikua wahamiaji haramu.
Maiti 6 zimekutwa zikielea katika Mto Ruvu eneo la Bagamoyo huku zikiwa zimearibika vibaya | Bongo5.com
Pia kuna yule jamaa msaidizi wa Mbowe, sijui kama keshapatikana au ndio yale yale.
Huwa vigumu sana kuhusisha serikali kwenye matukio ya mauaji ya kihivi, ndio pia ilivyo Kenya. Huku kuna matukio ya watu kutoweka kimya au kuuawa, hususan wakati wana usalama wamepanic kwa ajili ya matukio kama vile ugaidi, ujangili au machafuko ya aina yoyote.
Hilo la wakimbizi wa ndani, ni picha mbovu na ya aibu Kenya na huwa tunaikemea kwa nguvu zote. Maana hutokea pale wanasiasa wanabisha matokeo ya kura na kuanzisha vurugu. Viongozi wa upinzani Tanzania ni wazalendo wasiopenda fujo, namkumbuka Lowassa alipodai kwamba kura zake zimeibwa, lakini papo hapo akawaomba wafuasi wake wadumishe amani na uzalendo. Kwa hilo nawapa heko viongozi wenu wa upinzani, viongozi wa Kenya huwa wanatibua hadi panachimbika.