PostGE2025 Amnesty International: Nguvu kupita kiasi ilitumika Oktoba 29

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Yaani wanaona kama tukio la October 29 ni la kawaida,LAA HASHAAA...muda ukifika,mtawajibika
 
Shirika la kimataifa linaloshughulikia haki za binadamu la Amnesty International, limetoa ripoti yake inayodai kwamba, vyombo vya usalama vya Tanzania vilitumia nguvu zisizohitajika au kupita kiasi katika kudhibiti maandamano ya uchaguzi kati ya tarehe 29 Oktoba na 3 Novemba 2025.
‎
‎Ripoti ya Shirika hilo iliyotolewa Desemba 19, 2025, imeeleza kwamba shirika hilo limegundua kuwa vyombo vya usalama vilitumia silaha kwa uzembe, na kusababisha majeraha na vifo kwa watu wasiokuwa na hatia, huku wakitumia gesi ya kutoa machozi katika maeneo ya makazi na hata kuirusha ndani ya nyumba za watu.
‎
‎Kulingana na Katibu Mkuu wa Amnesty international, Agnes Callamard, vurugu zilifanywa na vyombo vya usalama dhidi ya waandamanaji na watu wengine waliokuwa wakitekeleza shughuli zao za kila siku.
‎
‎Kwa mujibu wa Katibu huyo, baada ya kuzimwa kwa mtandao, maafisa wa usalama waliwapiga watu na kuwatesa kwa njia mbalimbali, kuwanyima waliojeruhiwa huduma za afya, kuwakamata waliokuwa bado wanahitaji matibabu, na kuchukua miili ya waathiriwa kutoka mochwari na kuipeleka kusikojulikana.
‎‎
Hata hivyo, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza na Wazee wa Dar es salaam, Desemba 2, 2025, alieleza kwamba kiwango cha nguvu iliyotumika kudhibiti maandamano ya Oktoba 29 kiliendana na tukio husika.

Mapema ‎tarehe 14 Novemba, Rais Samia alitangaza kuundwa kwa tume ya uchunguzi kuhusu kilichotokea wakati huo; tume ambayo uhuru wake umetiliwa shaka na vyama vya siasa, wanaharakati na mashirika ya kiraia nchini.

Kitenfo cha Wambura na Muliro kuendelea kuwepo kwenye nafasi zao mpaka sasa ni ujumbe tosha kuwa walifuata maelekezo tu.
 
Wahalifu wakirudia kufanya walichofanya 29/10 akina wambura na muliro watafanya vilevile tena
 
Akili zenu ni zile zile.

Damu haishibishi wala kutoa kiu. Endeleni tu na Ushetani wenu. Hata kabla ya MO 29 wamekuwa wakiyafanya na bado wanaendelea kuyafanya.
 
Tanzania: Vikosi vya usalama vilitumia nguvu kinyume cha sheria katika ukandamizaji wa maandamano ya uchaguzi na ‘kuchukua’ maiti.

Vikosi vya usalama vya Tanzania vilitumia nguvu zisizo za lazima au zisizo na uwiano, ikiwa ni pamoja na nguvu za mauaji, kukandamiza maandamano ya uchaguzi kati ya Oktoba 29 na 3 Novemba 2025, yakionyesha kutozingatiwa kwa kushangaza kwa haki ya kuishi na uhuru wa kukusanyika kwa amani huku mamia ya watu wakiripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kote nchini, Amnesty International imesema leo.

Tanzania: Security forces used unlawful lethal force in election protest crackdown and ‘took away’ dead bodies
 
Shirika la kimataifa linaloshughulikia haki za binadamu la Amnesty International, limetoa ripoti yake inayothibitisha kwamba, vyombo vya usalama vya Tanzania vilitumia nguvu zisizohitajika au kupita kiasi katika kudhibiti maandamano ya uchaguzi kati ya tarehe 29 Oktoba na 3 Novemba 2025.
‎
‎Ripoti ya Shirika hilo iliyotolewa Desemba 19, 2025, imeeleza kwamba shirika hilo limegundua kuwa vyombo vya usalama vilitumia silaha vibaya, na kusababisha majeraha na vifo kwa raia, huku wakitumia gesi ya kutoa machozi katika maeneo ya makazi na hata kurusha ndani ya nyumba za watu.
‎
‎Kulingana na Katibu Mkuu wa Amnesty international, Agnes Callamard, vurugu zilifanywa na vyombo vya usalama dhidi ya waandamanaji na watu wengine waliokuwa wakitekeleza shughuli zao za kila siku.
‎
‎Kwa mujibu wa Katibu huyo, baada ya kuzimwa kwa mtandao ukatili uliendelea, maafisa wa usalama waliwapiga watu na kuwatesa kwa njia mbalimbali, kuwanyima waliojeruhiwa huduma za afya, kuwakamata waliokuwa bado wanahitaji matibabu, na kuchukua miili ya waathiriwa kutoka mochwari na kuipeleka kusikojulikana.

Amnesty International inasema ilipata taarifa ya baadhi ya waandamanaji kujihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kuiba, kuharibu magari serikali na kuchoma majengo ya utawala. Hata hivyo, katika matukio ambayo shirika hilo liliyachunguza, waandamanaji au wapita njia ambao hawakuonekana kuwa tishio kwa uhai wa maafisa wa polisi au watu wengine, walishambuliwa kwa silaha za moto.
‎‎
Hata hivyo, Rais Samia alipokuwa akizungumza na Wazee wa Dar es salaam, Desemba 2, 2025, alieleza kwamba kiwango cha nguvu iliyotumika kudhibiti maandamano ya Oktoba 29 kiliendana na tukio husika.

Mapema ‎tarehe 14 Novemba, Rais Samia alitangaza kuundwa kwa tume ya uchunguzi kuhusu kilichotokea wakati huo; tume ambayo uhuru wake umetiliwa shaka na vyama vya siasa, wanaharakati na mashirika ya kiraia nchini.
View attachment 3517566
======

AMNESTY INTERNATIONAL
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​

Tanzania: Vikosi vya usalama vilifanya mauaji makubwa kinyume cha sheria katika kuzima maandamano wakati wa uchaguzi na ‘kuchukua’ maiti

Vikosi vya usalama vya Tanzania vilitumia nguvu kubwa kupita kiasi au isiyo ya lazima, ikiwemo mauaji, kuzima maandamano ya uchaguzi kati ya tarehe 29 Oktoba na 3 Novemba2025, vikionesha kiwango cha kutisha cha kutojali haki ya uhai na uhuru wa kukusanyika kwaamani wakati mamia ya watu wakisemekana kuuawa au kujeruhiwa nchini kote, Amnesty International imesema leo.

Utafiti mpya unaelezea kwa kina jinsi vikosi vya usalama vilivyofyatua risasi za moto namabomu ya machozi kuwalenga moja kwa moja waandamanaji na watu wengine binafsiambao hawakuwa tishio la wazi la kusababisha vifo au majeraha makubwa. Shirika hili lilibaini kwamba vikosi vya usalama vilitumia silaha za moto vibaya, vikijeruhi na kuua wapita njia, na kurusha mabomu ya machozi kwenye maeneo ya makazi na miji ya watu Katikati ya kuzimwa kwa intaneti nchi nzima, maafisa wa usalama waliwapiga watu na kuwatendea ukatili mwingine, walizuia majeruhi kupata matibabu, waliwatia nguvuni baadhi ambao bado walikuwa wakihitaji kupata matibabu, na kuchukua maiti za wahanga wa ukatili wao kutoka vyumba vya kuhifadhia maiti, na kuwapeleka sehemu zisizojulikana.

“Ukatili ambao vikosi vya usalama viliwatendea waandamanaji na watu wengine waliokuwa wakienda kwenye shughuli zao za kila siku ulikuwa wa kutisha na haukubaliki, na bado ni ushahidi mwingine wa kuongezeka kwa hali ya kukosa uvumilivu nchini Tanzania,” alisema Agnès Callamard, Katibu Mkuu wa Amnesty International.

Mnamo 14 Novemba, rais wa Tanzania alitangaza kuundwa kwa tume ya uchunguzi wa mauaji ya waandamanaji. Hata hivyo, wanachama wa asasi za kiraia wameonesha wasiwasi kuhusu uhuru wake.

“Uundwaji wa tume ni hatua ya kwanza kati ya nyingi ambazo lazima zifuatwe ili kuleta uwajibikaji. Mamlaka sasa lazima zihakikishe kwamba uchunguzi wote unakuwa huru, wa kina na usio na upendeleo. Hakuna anayepaswa kukingwa dhidi ya haki kutendeka: wale waliotoa amri, waliowezesha na kutumia nguvu kinyume cha sheria lazima wawajibishwe bila ya kujali vyeo vyao. Kila familia inayoomboleza inastahili kupata majibu, haki na nafasi ya kulipwa fidia. Jambo lolote pungufu ya hapo litakuwa ni jaribio la kutakatisha uovu,” alisema Agnès Callamard.

Kati ya tarehe 3 na 28 Novemba, Amnesty International ilifanya mahojiano na watu 35, wakiwemo manusura wa kupigwa risasi na majeraha ya kupigwa mabomu ya machozi, mashuhuda, mawakili wanaowatetea waandamaji waliotiwa nguvuni na wahudumu wa afya waliotoa matibabu kwa wahanga waliojeruhiwa, pamoja na ndugu wa waliouawa. Timu ya uchunguzi kwa njia ya kidijitali ya Amnesty International, Maabara ya Ushahidi (Evidence Lab), ilithibitisha video 26 na picha sita zilizorushwa mtandaoni kati ya tarehe 2 na 18 Novemba au kutumwa moja kwa moja kwa wafanyakazi wa Amnesty International na vyanzo vya kuaminika.

Serikali ya Tanzania haikujibu maombi ya Amnesty ya kuomba maoni yao. ‘Kunguru walikuwa wakila miili ya marehemu’ Wahudumu watatu wa afya katika hospitali za umma jijini Dar es Salaam, Arusha na Mwanza waliiambia Amnesty International kwamba mamia ya watu waliokuwa na majeraha ya kupigwa risasi walipokelewa hospitalini kwa ajili ya matibabu kati ya tarehe 29 na 31 Oktoba. Wengi wao walikuwa vijana, lakini majeruhi pia walijumuisha watoto na wanawake. Walikuwa wamepigwa risasi kichwani, kiunoni, miguuni, shingoni, tumboni, matakoni, mgongoni na kifuani.

Wahudumu wa afya wa Arusha na Dar es Salaam walisema mamia ya maiti zililetwa katika hospitali zao, huku nyingine zikiachwa nje kutokana na kukosa nafasi katika vyumba vya kuhifadhia maiti. Maabara ya Ushahidi ilithibitisha video moja ikionesha takribani maiti 70 zikiwa zimerundikwa sakafuni na kwenye machela katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam. Pia ilithibitisha video mbili na picha moja zikionesha takribani maiti 10 zikiwa zimerundikwa kwenye machela tatu nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure jijini Mwanza. “Tangu nianze kazi zaidi ya miaka 15 iliyopita, sijawahi kuona jambo kama hili. Sijawahi kuona watu wengi kiasi hiki wakiwa wamepigwa risasi namna hii, na maiti nyingi hivyo zikiwazimerundikwa na kunguru wakila miili yao,” mhudumu wa afya aishie Dar es Salaam aliiambia Amnesty.
​

Maelezo ya picha: Picha za video ambazo zimethibitishwa na Amnesty International zikionesha takribani miili 70 ikiwa imerundikwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa yaMwananyamala, jijini Dar es Salaam. Chanzo: Amnesty International Matumizi mabaya ya silaha za moto na mabomu ya machozi Maria*, 28, alisema polisi walimpiga risasi mumewe eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam mnamo 29 Oktoba 2025 na akafariki siku mbili baadaye wakati akipatiwa matibabu ya damu kuvuja ndani ya mwili.

“Polisi hawakurusha bomu lolote la machozi. Walitumia risasi za moto tu. Walikuwa wamesimama nyuma ya gari. Baada ya muda mfupi, nilitoka nje na kusikia watu wakipiga kelele, ‘Amemuua, amemuua.’ Niliona kutokea kwa mbali kola ya shati la mtu aliyekuwa amelala ardhini na kugundua alikuwa mume wangu,” alisema.

Paulo Kingi*, 46, alikimbilia Kenya baada ya kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake Goba jijini Dar es Salaam mnamo 29 Oktoba. Anakumbuka kuona watu waliokuwa wamebeba silaha, ambao aliamini walikuwa maafisa wa usalama, wakipita na gari mbele ya nyumba yake.

“Walinilenga na kufyatua risasi; nilisikia maumivu kwenye mguu wangu wa kushoto karibu na kifundo cha mguu. Maumivu hayo yalinifanya nianguke chini, nilipopagusa, niliona damu ikivuja. Hapo ndipo nilipotambua nilikuwa nimepigwa risasi. Nikiwa chini, niliweza kusikia milio zaidi ya risasi,” alisema.

Amnesty International ilipata taarifa kwamba kuwa baadhi ya waandamanaji walirusha mawe, walichoma matairi ili kuziba barabara, waliharibu magari ya serikali, walichoma moto majengo ya utawala, walipora mali au walishiriki katika maandamano wakiwa wamebeba fimbo. Hata hivyo, katika matukio ambayo shirika hili liliyachunguza, waandamanaji au wapita njia ambao hawakuonekana kwamba walikuwa tishio kwa uhai wa maafisa wa polisi au watu wengine, walishambuliwa kwa silaha za moto.

Mashuhuda waliiambia Amnesty International kwamba polisi na maafisa wa usalama waliokuwa wamevaa mavazi ya kiraia waliamua kupiga risasi za moto bila ya kutoa onyo ili kutawanyisha watu, mara tu au muda mfupi baada ya kuwarushia mabomu ya machozi. Shuhuda mmoja alisema kwamba, takribani majira ya mchana mnamo 30 Oktoba, watu waliokuwa katika sare za polisi walirusha mabomu ya machozi barabarani karibu na soko la Sirare na kisha kumimina risasi mbele ya duka, ambapo alikuwa amekaa na rafiki yake. Walimuua rafiki yake papo hapo, huku yeye akipata jeraha la risasi kichwani.

Ushahidi wa kidijitali wa matumizi mabaya ya silaha za moto Maabara ya Ushahidi ya Amnesty pia ilithibitisha video zikionesha dhahiri matumizi mabaya ya silaha za moto. Katika video moja, mwanamke mmoja ni miongoni mwa kundi la watu wanaoonekana wakikimbia pembezoni mwa barabara jijini Arusha wakati milio ambayo inaendana na kufyatua risasi ikisikika. Katika tukio hilo, mwanamke huyo ambaye alikuwa ameshika fimbo anaanguka chini, kisha anajaribu kuinuka kwa kusaidiwa na mtu mwingine kabla ya kuanguka tena. Doa dogo jekundu linaonekana mgongoni kwake, huku doa kubwa zaidi jekundu likionekana kifuani kwake.

View attachment 3518154​
Maelezo ya picha: Picha za video zikionesha mwanamke akipigwa risasi kifuani jijini Arusha.​

Chanzo: Amnesty International Video nyingine tatu zilizothibitishwa zinamuonesha akiwa amelala bila kujitingisha pembezoni mwa barabara wakati milio mingi zaidi ya risasi ikisikika. Katika video hizo, nguo yake
imetapakaa madoa makubwa zaidi ambayo yanafanana na damu nyuma na mbele. Mwanaume mwingine anaonekana akiwa amebebwa, dhahiri amepoteza uhai, akivuja damu kichwani kwake.

Daktari wa utambuzi wa magonjwa na sababu za vifo aliyezikagua picha hizo zilizotolewa na mhudumu wa afya kutoka hospitali moja jijini Arusha na video ya mwanaume aliyejeruhiwa Dar es Salaam alihimitisha kwamba “picha na video … za watu waliojeruhiwa zilionesha ushahidi mzito wa majeraha ya bunduki zenye nguvu kubwa, ambayo yanatokana na bunduki za kijeshi.”

“Kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji wasio na silaha na wapita njia wasio na tishio lolote la dhahiri kwa uhai wa wengine ni ukiukaji wa wazi wa haki ya kuishi. Ushahidi uko wazi: maafisa wa usalama wa nchi walionesha kutojali kabisa uhai wa watu,” alisema Agnès Callamard.

Maafisa wa usalama pia walitumia mabomu ya machozi kwa namna iliyo kinyume cha sheria ili kuzima maandamano ya amani. Katika matukio mengine, walirusha mabomu ya machozi kuwalenga wapita njia au wakazi katika maeneo yaliyokumbwa na maandamano na uzuiaji wake uliofuatia.

Shuhuda mmoja aliiambia Amnesty International kwamba bomu la machozi lilirushwa ndaniya nyumba yake mnamo 29 Oktobaa, wakati mtoto wake wa mwezi mmoja akiwa ndani. Mateso na ukatili mwingine Amnesty International ilithibitisha video sita zikionesha matukio tofauti karibu na shule ya msingi Tabata jijini Dar es Salaam ambapo vikosi vya usalama na wanaume waliovaa mavazi ya kiraia wakifanya vitendo vya utesaji na ukatili mwingine. Wahanga – wote wakiwa wanaume– walilazimishwa kugalagala chini, kuruka kichura, au kuketi pembezoni mwa barabara, hukuwakipigwa kwa virungu, ngumi, viboko, mateke au kuburuzwa kwa kushikwa miguu.
​

Maelezo ya picha: Video zikionesha vikosi vya usalama na wanaume waliovaa mavazi ya kiraia wakiwalazimisha watu kugalagala au kuruka kichura huku wakipigwa kwa virungu, viboko au mateke. Chanzo: Amnesty International Majeruhi wanyimwa matibabu ya kutosha Vikosi vya usalama vya Tanzania viliingilia upatiwaji matibabu wa watu waliojeruhiwa katika baadhi ya mikoa. Mhudumu wa afya aishie Dar es Salaam alisema kwamba askari waliwaamuru wahudumu wa afya kuwakabidhi takribani wagonjwa watano waliokuwa na majeraha ya risasi, wakati wakiwa bado wanavuja damu, kwa madhumuni ya kuwahoji.

Watano hao walikuwa wamevaa sare au fulana za chama cha upinzani cha CHADEMA. Hakuwaona wagonjwa hao tena. Maafisa usalama pia waliwaamuru wahudumu wa afya kutoa kipaumbele kwa baadhi ya
wagonjwa tofauti na wengine na kuwaonya wahudumu wa afya kutoongea chochote au kupiga picha walichokiona kwenye hospitali zao.

Mhudumu mmoja wa afya alielezea kuwepo kwa polisi wengi hospitalini kwao jijini Mwanza, huku maafisa hao wakiwaamuru wauguzi kuacha kuwapatia matibabu baadhi ya majeruhi. “Walichukua watu ambao walikuwa bado wakipumua na ambao wangeweza kuokolewa uhai wao, na kuwapeleka chumba cha kuhifadhia maiti,” alisema. Mhudumu huyo wa afya alisema kwamba afisa mwandamizi wa serikali alikwenda hospitalini hapo mnamo tarehe 2 au 3 Novemba na kuwaamuru wahudumu wa afya kuwaweka wagonjwa wote wenye majeraha ya risasi katika wodi tofauti, ambapo wangefungwa pingu na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi, akieleza kwamba watashitakiwa kwa uhaini kwa sababu ya kushiriki katika maandamano.

Amnesty Internatonal pia ilipata taarifa kwamba waandamanaji na wapita njia waliojeruhiwa ama waliondoka wenyewe hospitalini kabla ya muda au waliepuka kupata kabisa matibabu hospitalini, kwa hofu ya kutiwa nguvuni. ‘Tuliamua kuzika nguo zake na picha yake’ Amnesty International iliwahoji wanafamilia na marafiki wa watu nane waliouawa Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Tunduma, Moshi na Mbeya ambao hawakuweza kupata miili ya wapendwa wao, hata baada ya kuwatafuta katika vyumba mbalimbali vya kuhifadhia maiti, na ambao wana wasiwasi kwamba vikosi vya usalama vilichukua miili yao kuficha ushahidi wa mauaji.

Watu waliomfahamu Stephano China, 19, ambaye mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Tunduma baada ya kuuawa tarehe 29 Oktoba, waliiambia Amnesty kwamba siku iliyofuatia walikwenda kuangalia mwili wake, lakini maiti haikuwepo. “Wao (wahudumu wa hospitali) walisema polisi walikuja kuchukua miili yote. Hatukuweza kufanya lolote.”

Familia ya Daudi Ndone, mwenye miaka 38, aliyepigwa risasi na kufa jijini Dar es Salaam eneo la Manzese mnamo 29 Oktoba, pia haikuweza kupata mwili wake licha ya kutafuta sana katika vyumba mbalimbali vya kuhifadhia maiti kwa zaidi ya wiki moja. “Kulingana na mila zetu, kwa vile hatukapata maiti yake, tuliamua kuzika nguo zake na picha yake,” alisema mmoja wa ndugu zake.

Hata katika kifo, wahanga hawa wa ukatili wa polisi hawawezi kupumzika kwa amani. Amnesty Interenational inatoa wito kwa serikali kukabidhi miili ya wale wote waliouawa katika maandamano na baada ya maandamano kwa ndugu zao ili waweze kuzikwa kwa heshima na kwa taratibu husika,” alisema Agnès Callamard.

Kwa taarifa zaidi au kupanga mahojiano, tafadhali wasiliana na ofisi ya habari ya Amnesty
International:
Simu : +44 20 7413 5566
Barua pepe : [email protected]
X : @amnestypress​
Unasema waliokufa ni 10 tulikuwepo?? Nami nakujibu ndiyo nilikuwepo kwenye msiba wa kijana wa jirani yangu aliyepigwa risasi na mapolisi kule salasala
Ilikuwa hivi, kijana alitoka nyumbani yeye na boss wake. Kwenda kuongeza umeme dukani. Ilikuwa tarehe 30 oct. Tukiwa tumefungiwa ndani.
Wakati wanajiandaa kufunga a ofisi Ili warudi nyumbani. Walikuja watu na Noah nyeusi wakafyatua risasi zikampata kijana kifuani akadondoka chini.
Boss wake akamchukua na kumpeleka zahanati ya karibu.wakamshauri aende mwananyamala. Akasimama katikati ya barabara kuomba msaada. Ikaja Noah ya polisi iliyokuwa inakusanya maiti. Waliopo ndani wakatishia kumua lakini baadae walikuja kumchukia majeruhi na kumpeleka hospital.
Ndani ya gari kulikuwepo na miili mwingine ambayo ilidhaanzq kuoza ( ushahidi wa boss wa marehemu/ jirani yangu)
Alipokwa simu zake. Walizungika sana na kuokota miili mpaka wanafika mwnyamala hali ya kijana ilikuwa mbaya sana akafariki Dunia mchana ule. Ndiyo nilikuwepo.
Tukiwa nyumbani msibani mfiwa alipigiwa simu Toka mortuary mwnyamala kwamba Kuna miili inaenda kuzikwa jioni Ile kwenye kaburila pamoja so awe makini wa. Kwake usitolewe. Walizikwa makaburi ya kondo na mwananyamala.
Mfiwa alitusimulia kwamba alikuta miili mingi sana mortuary wakati.anaenda kuhifadhi kijana wake
Tulikaamsibani kwa siku kadhaa mpaka walipofanikiwa kusafitisha kwenda Tarime kuzika. Wakipata mwili wao kwa urahisi kwasababu Wana ndugu polisi wakubwa ( sitawataj hapa)
Nguo zenye damu ya marehemu zimehifadhiwa na zinaweza kutumika kama ushahidi hapo badae.zipo
Nikisikia mtu anaulizia Nilikuwepo??? Namshangaa na kumdharau sana.
 
Hii ripoti inaunga mkono ripoti ya CNN ya Larry Madowo

Samia kwa kumtumia Gerson Msigwa atakuwa mwendo wa kukanusha tu mwanzo mwisho hadi atakaponyofolewa kwenye ikulu yetu..

View: https://youtu.be/vqXI_Gxqe2E?si=xBezlXbV3Hs-3cQE
 
Unasema waliokufa ni 10 tulikuwepo?? Nami nakujibu ndiyo nilikuwepo kwenye msiba wa kijana wa jirani yangu aliyepigwa risasi na mapolisi kule salasala
Ilikuwa hivi, kijana alitoka nyumbani yeye na boss wake. Kwenda kuongeza umeme dukani. Ilikuwa tarehe 30 oct. Tukiwa tumefungiwa ndani.
Wakati wanajiandaa kufunga a ofisi Ili warudi nyumbani. Walikuja watu na Noah nyeusi wakafyatua risasi zikampata kijana kifuani akadondoka chini.
Boss wake akamchukua na kumpeleka zahanati ya karibu.wakamshauri aende mwananyamala. Akasimama katikati ya barabara kuomba msaada. Ikaja Noah ya polisi iliyokuwa inakusanya maiti. Waliopo ndani wakatishia kumua lakini baadae walikuja kumchukia majeruhi na kumpeleka hospital.
Ndani ya gari kulikuwepo na miili mwingine ambayo ilidhaanzq kuoza ( ushahidi wa boss wa marehemu/ jirani yangu)
Alipokwa simu zake. Walizungika sana na kuokota miili mpaka wanafika mwnyamala hali ya kijana ilikuwa mbaya sana akafariki Dunia mchana ule. Ndiyo nilikuwepo.
Tukiwa nyumbani msibani mfiwa alipigiwa simu Toka mortuary mwnyamala kwamba Kuna miili inaenda kuzikwa jioni Ile kwenye kaburila pamoja so awe makini wa. Kwake usitolewe. Walizikwa makaburi ya kondo na mwananyamala.
Mfiwa alitusimulia kwamba alikuta miili mingi sana mortuary wakati.anaenda kuhifadhi kijana wake
Tulikaamsibani kwa siku kadhaa mpaka walipofanikiwa kusafitisha kwenda Tarime kuzika. Wakipata mwili wao kwa urahisi kwasababu Wana ndugu polisi wakubwa ( sitawataj hapa)
Nguo zenye damu ya marehemu zimehifadhiwa na zinaweza kutumika kama ushahidi hapo badae.zipo
Nikisikia mtu anaulizia Nilikuwepo??? Namshangaa na kumdharau sana.
Ushahidi mzuri sana huu na utatumika panapohusika kwa kuwa utahitajika....

Kwa sasa, ushauri wangu ni kuwa endelea kujificha na kuficha ushahidi huu. Jitahidi kuwa unanimous mpaka hali itakuwa salama, wengi watajitokeza (ukiwemo wewe) ili kutoa ushahidi hii

Mimi nilisimamia uchaguzi hapa Tanganyika. Nilikuwa msimamizi msaidizi wa jimbo mojawapo huku Tanganyika. Ninazo takwimu zote za jimbo kuthibitisha kuwa matokeo yote ya Urais, ubunge na udiwani 29/10 ambayo ndiyo chanzo cha mauaji haya si halisi, ni feki yaliyopikwa na Jaji Mwambegele na Ramadhani Kailima wa inayoitwa Tume Huru ya Uchaguzi na kutupatia sisi wa majimbo ili tuyashushe kwenye kata na kwenye vituo vya kupigia kura na baadaye ndiyo yakatangazwa na kumpa ushindi wa kihuni huyu mama mwenye laana, Samia Suluhu Hassan....

Hali ikitulia, kwa hakika kabisa, nitajitokeza kutoa ushahidi wa matokeo haya feki ya kupika yaliyompa ushindi Samia na wabunge na madiwani wake nchi nzima...!!

Hii vita bado mbichi sana. TUTASHINDA NA KILA MTU ATAPATA HAKI YAKE...!

NOTE:
Usije kupeleka ushahidi huu kwenye ile tume feki inayoongozwa na Jaji Chande iliyoundwa na muuaji mkuu mwenyewe Samia ili kumsafisha na uovu wake. Ukienda huko, jua kabisa kesho hutaliona jua!
 
Huwa ninawashangaa sana wale wote wanaomkingia kifua huyu kimama kwa yale mauaji aliyoyafanya kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu..

Eti "waandamanaji walichoma miundo mbinu sasa polisi wangefanyaje?"..
Mara sijui "waandamanaji walitaka kuipindua serikali hivyo hapakuwepo na njia nyingi ya kuwadhibiti zaidi ya risasi".

Yaani hoja za kipumbavu kweli kuhalalisha mauaji, mpaka unajiuliza hivi haya majitu yameenda shule kweli?

Kama yale mauaji yangekuwa ni sahihi, Samiya wala hata asingeyafanya kwa kificho vile hasa kwa kuzima internet, na asingekuwa ana angaika kuficha ushaidi kila leo, na zaidi ya hapo hadi kufikia leo hii asingeshindwa kutoa idadi sahihi ya watu aliowaua....

...na kma hiyo haitoshi wala hata asingeishi kwa kujificha ficha kama muuza bangi na hizo ziara za kidiplomasia anazomtuma Kombo angekuwa anaenda yeye kwa jinsi anavyopenda kuzurura.

Kwa ufupi tu samiya alijua anachokifanya ni kosa kubwa sana ambalo litamgharimu yeye na serikali yake ila akapuuzia possible outcomes, akitegemea dunia haitajua....

....sasa hawa machawa wanaokuja na hoja za kipuuzi kuhalalisha mauaji sijui wahanga walichoma mwendokasi, mara walichoma maduka, sijui walichoma sheli... huwa nawaona wana funza vichwani mwao.

Nadhani hata wao wenyewe wanajionea jinsi hoja zao zilivyokuwa za kipuuzi, maana taasisi za kimataifa hakuna hata moja inayoongelea kuhusu kuchomwa kwa mwendokasi,sheli na maduka kwenye reports zao... maana hivyo ni vitu very insignificant ukilinganisha na maisha ya watu waliouawa.

Hizo sheli,mwendokasi,mabasi ya Esther na maduka yangeweza kupewa attention na international communities kama kusingekuwepo na vifo vya civilians vilivyotokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi kutoka kwa vyombo vya usalama.

Kama kuna mtu ambaye anaamini eti samiya atapita salama kwenye hili na hatimae kumaliza miaka yake mitano basi anajidanganya.

Huwezi kufanya unyama kma ule kisa tu madaraka halafu utegemee kubaki salama kwenye hayo madaraka yako, huyu atapewa pressure mpaka mpaka atasurrender mwenyewe.

Nahisi Samiya alimuona yule raisi wa madagascar bwana Andry Rojoelina ni mjinga sana kwa kuachia uraisi wakati angeweza kutumia tu vyombo vyake vya dola kuwadhibiti gen-z...
 
Muuaji wa kizimkazi hatokuja kusamehewa kwa alichokifanya.
 
Uyu mama akidondoka tu, familia yake itaandamwa kama mpira wa kona
 
Back
Top Bottom