PostGE2025 Amnesty International: Nguvu kupita kiasi ilitumika Oktoba 29

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Yaani wanaona kama tukio la October 29 ni la kawaida,LAA HASHAAA...muda ukifika,mtawajibika
 

Kitenfo cha Wambura na Muliro kuendelea kuwepo kwenye nafasi zao mpaka sasa ni ujumbe tosha kuwa walifuata maelekezo tu.
 
Kitenfo cha Wambura na Muliro kuendelea kuwepo kwenye nafasi zao mpaka sasa ni ujumbe tosha kuwa walifuata maelekezo tu.
Wahalifu wakirudia kufanya walichofanya 29/10 akina wambura na muliro watafanya vilevile tena
 
Wahalifu wakirudia kufanya walichofanya 29/10 akina wambura na muliro watafanya vilevile tena

Akili zenu ni zile zile.

Damu haishibishi wala kutoa kiu. Endeleni tu na Ushetani wenu. Hata kabla ya MO 29 wamekuwa wakiyafanya na bado wanaendelea kuyafanya.
 
Tanzania: Vikosi vya usalama vilitumia nguvu kinyume cha sheria katika ukandamizaji wa maandamano ya uchaguzi na ‘kuchukua’ maiti.

Vikosi vya usalama vya Tanzania vilitumia nguvu zisizo za lazima au zisizo na uwiano, ikiwa ni pamoja na nguvu za mauaji, kukandamiza maandamano ya uchaguzi kati ya Oktoba 29 na 3 Novemba 2025, yakionyesha kutozingatiwa kwa kushangaza kwa haki ya kuishi na uhuru wa kukusanyika kwa amani huku mamia ya watu wakiripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kote nchini, Amnesty International imesema leo.

Tanzania: Security forces used unlawful lethal force in election protest crackdown and ‘took away’ dead bodies
 
Unasema waliokufa ni 10 tulikuwepo?? Nami nakujibu ndiyo nilikuwepo kwenye msiba wa kijana wa jirani yangu aliyepigwa risasi na mapolisi kule salasala
Ilikuwa hivi, kijana alitoka nyumbani yeye na boss wake. Kwenda kuongeza umeme dukani. Ilikuwa tarehe 30 oct. Tukiwa tumefungiwa ndani.
Wakati wanajiandaa kufunga a ofisi Ili warudi nyumbani. Walikuja watu na Noah nyeusi wakafyatua risasi zikampata kijana kifuani akadondoka chini.
Boss wake akamchukua na kumpeleka zahanati ya karibu.wakamshauri aende mwananyamala. Akasimama katikati ya barabara kuomba msaada. Ikaja Noah ya polisi iliyokuwa inakusanya maiti. Waliopo ndani wakatishia kumua lakini baadae walikuja kumchukia majeruhi na kumpeleka hospital.
Ndani ya gari kulikuwepo na miili mwingine ambayo ilidhaanzq kuoza ( ushahidi wa boss wa marehemu/ jirani yangu)
Alipokwa simu zake. Walizungika sana na kuokota miili mpaka wanafika mwnyamala hali ya kijana ilikuwa mbaya sana akafariki Dunia mchana ule. Ndiyo nilikuwepo.
Tukiwa nyumbani msibani mfiwa alipigiwa simu Toka mortuary mwnyamala kwamba Kuna miili inaenda kuzikwa jioni Ile kwenye kaburila pamoja so awe makini wa. Kwake usitolewe. Walizikwa makaburi ya kondo na mwananyamala.
Mfiwa alitusimulia kwamba alikuta miili mingi sana mortuary wakati.anaenda kuhifadhi kijana wake
Tulikaamsibani kwa siku kadhaa mpaka walipofanikiwa kusafitisha kwenda Tarime kuzika. Wakipata mwili wao kwa urahisi kwasababu Wana ndugu polisi wakubwa ( sitawataj hapa)
Nguo zenye damu ya marehemu zimehifadhiwa na zinaweza kutumika kama ushahidi hapo badae.zipo
Nikisikia mtu anaulizia Nilikuwepo??? Namshangaa na kumdharau sana.
 
Hii ripoti inaunga mkono ripoti ya CNN ya Larry Madowo

Samia kwa kumtumia Gerson Msigwa atakuwa mwendo wa kukanusha tu mwanzo mwisho hadi atakaponyofolewa kwenye ikulu yetu..

View: https://youtu.be/vqXI_Gxqe2E?si=xBezlXbV3Hs-3cQE
 
Ushahidi mzuri sana huu na utatumika panapohusika kwa kuwa utahitajika....

Kwa sasa, ushauri wangu ni kuwa endelea kujificha na kuficha ushahidi huu. Jitahidi kuwa unanimous mpaka hali itakuwa salama, wengi watajitokeza (ukiwemo wewe) ili kutoa ushahidi hii

Mimi nilisimamia uchaguzi hapa Tanganyika. Nilikuwa msimamizi msaidizi wa jimbo mojawapo huku Tanganyika. Ninazo takwimu zote za jimbo kuthibitisha kuwa matokeo yote ya Urais, ubunge na udiwani 29/10 ambayo ndiyo chanzo cha mauaji haya si halisi, ni feki yaliyopikwa na Jaji Mwambegele na Ramadhani Kailima wa inayoitwa Tume Huru ya Uchaguzi na kutupatia sisi wa majimbo ili tuyashushe kwenye kata na kwenye vituo vya kupigia kura na baadaye ndiyo yakatangazwa na kumpa ushindi wa kihuni huyu mama mwenye laana, Samia Suluhu Hassan....

Hali ikitulia, kwa hakika kabisa, nitajitokeza kutoa ushahidi wa matokeo haya feki ya kupika yaliyompa ushindi Samia na wabunge na madiwani wake nchi nzima...!!

Hii vita bado mbichi sana. TUTASHINDA NA KILA MTU ATAPATA HAKI YAKE...!

NOTE:
Usije kupeleka ushahidi huu kwenye ile tume feki inayoongozwa na Jaji Chande iliyoundwa na muuaji mkuu mwenyewe Samia ili kumsafisha na uovu wake. Ukienda huko, jua kabisa kesho hutaliona jua!
 
Huwa ninawashangaa sana wale wote wanaomkingia kifua huyu kimama kwa yale mauaji aliyoyafanya kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu..

Eti "waandamanaji walichoma miundo mbinu sasa polisi wangefanyaje?"..
Mara sijui "waandamanaji walitaka kuipindua serikali hivyo hapakuwepo na njia nyingi ya kuwadhibiti zaidi ya risasi".

Yaani hoja za kipumbavu kweli kuhalalisha mauaji, mpaka unajiuliza hivi haya majitu yameenda shule kweli?

Kama yale mauaji yangekuwa ni sahihi, Samiya wala hata asingeyafanya kwa kificho vile hasa kwa kuzima internet, na asingekuwa ana angaika kuficha ushaidi kila leo, na zaidi ya hapo hadi kufikia leo hii asingeshindwa kutoa idadi sahihi ya watu aliowaua....

...na kma hiyo haitoshi wala hata asingeishi kwa kujificha ficha kama muuza bangi na hizo ziara za kidiplomasia anazomtuma Kombo angekuwa anaenda yeye kwa jinsi anavyopenda kuzurura.

Kwa ufupi tu samiya alijua anachokifanya ni kosa kubwa sana ambalo litamgharimu yeye na serikali yake ila akapuuzia possible outcomes, akitegemea dunia haitajua....

....sasa hawa machawa wanaokuja na hoja za kipuuzi kuhalalisha mauaji sijui wahanga walichoma mwendokasi, mara walichoma maduka, sijui walichoma sheli... huwa nawaona wana funza vichwani mwao.

Nadhani hata wao wenyewe wanajionea jinsi hoja zao zilivyokuwa za kipuuzi, maana taasisi za kimataifa hakuna hata moja inayoongelea kuhusu kuchomwa kwa mwendokasi,sheli na maduka kwenye reports zao... maana hivyo ni vitu very insignificant ukilinganisha na maisha ya watu waliouawa.

Hizo sheli,mwendokasi,mabasi ya Esther na maduka yangeweza kupewa attention na international communities kama kusingekuwepo na vifo vya civilians vilivyotokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi kutoka kwa vyombo vya usalama.

Kama kuna mtu ambaye anaamini eti samiya atapita salama kwenye hili na hatimae kumaliza miaka yake mitano basi anajidanganya.

Huwezi kufanya unyama kma ule kisa tu madaraka halafu utegemee kubaki salama kwenye hayo madaraka yako, huyu atapewa pressure mpaka mpaka atasurrender mwenyewe.

Nahisi Samiya alimuona yule raisi wa madagascar bwana Andry Rojoelina ni mjinga sana kwa kuachia uraisi wakati angeweza kutumia tu vyombo vyake vya dola kuwadhibiti gen-z...
 
Samia hataweza kuchomoka kwenye hili. Anawanga sana lakini haya mauaji aliyoidhinisha hachomoki.
 
Muuaji wa kizimkazi hatokuja kusamehewa kwa alichokifanya.
 
Uyu mama akidondoka tu, familia yake itaandamwa kama mpira wa kona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…