#COVID19 Amnesty International wanajaribu kuishinikiza Tanzania kununua chanjo ya Covid-19

Shilika la WHO lilikuwa la kwanza kumpongeza mama kuwa rais, unaelewa nn ktk hili na unadhani walimpongeza bure? Nchi yetu ina vibaraka wa kutosha kutimiza hili la msingi ni kuomba Mungu awatie upofu ili wasiweze kuleta uchafu wao huu
 
Kuna nchi kibao kama India zenye uhitaji wa chanjo kwanini wasianze huko?
India wako mbali sana na hili swala. Am telling you, muda si mtefu tutapata tu akili. Mwaka huu watu hakuna kwenda hija bila Chanjo. Itafika wakati tutabaki peke yetu ndio akilia itakaa sawa
 
Hatusemi kuwa hakuna aliyeathirika, bali tunasema Mungu ametuponya na kama Taifa take vizuri mara elfu nyingi ukilinganisha na mataifa mengine! Hilo halina ubishi!
Madhara hayajakuwa makubwa lakini kusema tumeponywa wakati kuna watu wamepoteza mpaka 6 members wa familia ni kuwa insensitive
 
Hakuna aliyesema hatutaki dawa wala chanjo nyingine. Ila hi ya corona haijafanyiwa utafiti wa kutosha na madhara yake tayari yameanza kuonekana! Hakuna ajuaye madhara ya muda mrefu ya hii chanjo! Uk
Ulitaka dunia isubiri miaka 7 kutafuta chanjo ya ugonjwa ambao umeshaua millions. Risk benefit analysis inasema benefits ni kubwa kuliko risks
 
Mlishatabiri Sana na BADO HAYAJATOKEA
India wako mbali sana na hili swala. Am telling you, muda si mtefu tutapata tu akili. Mwaka huu watu hakuna kwenda hija bila Chanjo. Itafika wakati tutabaki peke yetu ndio akilia itakaa sawa
 
Ila Watanzania kwa ujinga tumo sana. Aliyekwambia chanjo inazuia usiumwe au kufa nani? Hizo chanjo ziko kwenye majaribio. Zinaua, zinatoa mimba zinaharibu mzunguko kwa akina mama. Hayo ni madhara yanayojulikana. Kwa sababu ni za majaribio hakuna anayejua madhara yake kesho au baada ya miaka 10.

Nawashangaa sana Watanzania kulilia chanjo ambazo hata Food and Drug Authority y Wamarekani ambao ni wanasayansi pia hawajaipitisha.

Kila anayetaka kuwageuza Watanzania kama Guinea Pigs, lab rats kufanyia majaribio ni mpumbavu. Rais wetu asiangukie kwenye mtego wa hawa wahuni wanaotaka kutugeuza panya wa majaribio. Wapiga mapambio wengi hawajui hata composition ya hizo chanjo, achilia mbali madhara yake leo na vizazi vijavyo. Wanarudia tu yaliyosemwa kama kasuku!
 
Rais Samia ajue kwamba maamuzi anayoyafanya yakileta madhara watendaji wake wengi watakuja kumruka. Tumeona walivyofanya kwa Rais Magufuli.

Kwa hiyo, mimi raia wake, ninayemtakia mema na mafanikio, akijisikia kufuata ushauri wangu, namsihi aachane tu na hii chanjo. Risk yake ni kubwa mno na hakuna faida tangible. Aache tu kila mtu aishi namna anayoona sawa. Kwa wanaotaka kuchanjwa ziwekwe chanjo za kuuza wakanunue wachanje. Wawekewe vituo maalum waende huko. Wakichanja wakafa ni wao walichagua. Na serikali isizipigie debe kukwepa liability. Watanzania wawe na uchaguzi na asilazimishwe mtu!

Ni huo tu ushauri wangu!
 
There are many humu kwenye jamii forum ambao wanasapoti chanjo ya korona as if they don't see and understand what is going on sad.
 
Hakuna aliyesema hatutaki dawa wala chanjo nyingine. Ila hi ya corona haijafanyiwa utafiti wa kutosha na madhara yake tayari yameanza kuonekana! Hakuna ajuaye madhara ya muda mrefu ya hii chanjo! Uk
Tengenezeni yenu
 
ukiwa na nafasi:

 
Kwenye hili la Covid, ni Mungu pekee kusimama hakuna cha sanitizer, barakoa wala chanjo hapo. Uhindini pamoja na kuwa na chanjo bora kabisa ila mdudu kawatikisa vibaya mno sisi ni kina nani kama sio Mungu kuwa pamoja nasi?.
 

Unapendekeza Amnesty International watupe fedha za kumalizia miradi ya SGR na Stieglers Gorge? Ndio hao waliopiga vita mradi wa JNHPP? Na sasa wanatulazimisha chanjo?

Au unachukulia Amnesty International kama mwakilishi wa nchi za Magharibi? Wale mnaowaita mabeberu? Ni muhimu uwasilishe hoja yako vizuri tusijeonekana Watanzania kama watu hamnazo!

Hata taasisi za UN tunazishambulia kama ni za mabeberu! Tunasahau kwamba kuna wakati pia zinapambana na hizo nchi: kumbuka US vs WHO.
 
kiukweli hata ikija iwe ni chaguo la mtu na sio lazima,corona ipo ila Mungu ni mwema...hivi unajua India ndio nchi inayoongoza kuwa na dini nyingi na hasa za kuabudu sanamu na wanyama!
 
Hizo chanjo ni wizi kwa Sasa
Makampuni makubwa yanahonga wanasiasa na makundi ya kijamii kulazimisha nchi za Afrika zinunue chanjo ili wapate faida
Watanzania tupo milioni 60,wakipewa chanjo watanzania milioni 15 tu zidisha kwa Bei ya chanjo 13,000 unapata Bilioni 195!
 
Hizi kauli ongea kama Covid haijapita na mtu wako wa karibu.
Peleka chato ukazike huo Ukinjenketile Ngwale wako! Hupimi, huna takwimu utawezaje kusema tumenusurika kwa kiasi gani?! Tumbafyuu kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…