Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema kuwa baada ya uchaguzi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitageuka kuwa kama jukwaa la harakati kwa sababu wamepoteza muelekeo na malengo ya chama cha siasa ambayo lenho kuu la chama cha siasa ni kushika dola.
Makalla ameeleza hayo Aprili 28,2025 wakati akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Ubungo Dar es salaam akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
“Chadema watabaki kama jukwaa la harakati kwa sababu chama cha siasa lengo lake ni kushika dola na katiba yao ibara ya nne inasema watashiriki uchaguzi na kushika dola kwahicho chadema yaani kuanzia sasa na kuendelea kama hawatafanya uchaguzi kwa miaka mitano litakuwa jukwaa lolote kwa sababu wamepotesa malengo cha chama cha siasa,” amesema Makalla.
Amesema hata wakiulizwa kwa sasa wanataka nini hawana kwa sababu chama chao kimekuwa jukwaa la harakati na hata wanachokifanya sasa ni harakati.
Makalla ameongeza kitendo cha wao kuwaita wananchi mahakamani ni kuonesha hawakuwa na nia nzuri na kuwataka wauache muhimiri wa Mahakama katika kufanya maamuzi kwani mahakama ni chombo huru.