PreGE2025 Amos Makalla: Hata ungepost Mamilioni ya post 'No Reform, No Election' haisadii, Uchaguzi uko pale pale

PreGE2025 Amos Makalla: Hata ungepost Mamilioni ya post 'No Reform, No Election' haisadii, Uchaguzi uko pale pale

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi CPA Amos Makalla amesema uchaguzi mkuu mwaka huu utafanyika kwa mujibu wa katiba na sheria kama ilivyopangwa, hivyo hata watu wakichapisha (kupost) na kutuma ‘No Reform No Election’ haisaidii.

Makalla ameeleza hayo Juni 8, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja Manyema Wilaya ya Moshi Mjini Mkoani Kilimanjaro akiendelea na ziara yake ya Kanda ya Kaskazini.

Akizungumza kujibu sekeseke linaloendelea katika mitandao ya kijamii Makalla amesema machapisho yanayochapishwa yakiandikwa ‘No reform no election’ hayana maana yoyote na haiwezi kuwa sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi.

"Kwahiyo hata yale yanayoendelea kwenye mitandao hata wakichapisha machapisho mamilioni na mamilioni ya ‘No Reform no election’ uchaguzi upo pale pale haisaidii we njoo tu weka pale tukiweka post weka(comment) haisaidii, uchaguzi hausogezwi utafanyika kama ulivyopangwa."

file_00000000a19c61f7a8a31c72919aef6b.png
 
Na sisi tunamjibu kilaza bwana mdogo makala kwamba hata kama atasema uchaguzi uko pale pale mara milioni,ss tunamwambia huyu bwana mdogo makala kwamba NO REFORMS NO ELECTION Iko pale pale.Aelewe hivyo muda haugandi.ila asikimbie hilo ndio la msingi maana ss tumechoka sana kuibiwa na tunasema imetosha.
Nyie mabwege hamzidi 5% wapiga kura wa kweli hawamo humu wako kwenye shughuli zao
 
CCM Wamekuwa wajinga mno, wanafikiri hii nchi ni mali yao, kwamba wanaweza kufanya chochote, na hizo post mnazosema mama kafanya, kafanya nini, ni kodi zetu bwana zimefanya, tena mmeiba sana. hatutaki mauongo ya 1970+ kuwa serikali hivi, serikali vile, upinzani ukichukua dola vita itakuja.
Utakufa na stress ww acha siasa km huiwezi
 
Kuelekea uchaguzi mkuu CCM haijapata anayejibu hoja za wapinzani. Wapi Makonda, Polepole hata Shaka.
Naona miwani na kitambi tu. Sioni hoja
 
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi CPA Amos Makalla amesema uchaguzi mkuu mwaka huu utafanyika kwa mujibu wa katiba na sheria kama ilivyopangwa, hivyo hata watu wakichapisha (kupost) na kutuma ‘No Reform No Election’ haisaidii.

Makalla ameeleza hayo Juni 8, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja Manyema Wilaya ya Moshi Mjini Mkoani Kilimanjaro akiendelea na ziara yake ya Kanda ya Kaskazini.

Akizungumza kujibu sekeseke linaloendelea katika mitandao ya kijamii Makalla amesema machapisho yanayochapishwa yakiandikwa ‘No reform no election’ hayana maana yoyote na haiwezi kuwa sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi.

"Kwahiyo hata yale yanayoendelea kwenye mitandao hata wakichapisha machapisho mamilioni na mamilioni ya ‘No Reform no election’ uchaguzi upo pale pale haisaidii we njoo tu weka pale tukiweka post weka(comment) haisaidii, uchaguzi hausogezwi utafanyika kama ulivyopangwa."

Hii ni hatari sana; SAAAANAAAAA!
Ukitazama umati huo anaouhutubia Makalaa; tena asili mia kubwa inaonekana ni CCM..., Umati ule hauna uhai hata kidogo. Ni umati usiokuwa na matumaini kabiiiisa!

Samia Suluhu Hassan, anayo kazi ya ziada mwaka huu.

Hata bila ya kuwepo CHADEMA uchaguzi huu utakuwa ni tofauti kabisa na chaguzi nyingine zote zilizowahi kutokea.

Ni hivi: hata katika mazingira ya uchaguzi anayoyataka Samia Suluhu Hassan; na bila kuwepo kwa CHADEMA kwenye uchaguzi huo, wananchi wenyewe watabuni njia inayofaa kumkataa Samia Suluhu Hassan.
Hakuna polisi atakaye weza kuzuia hilo, na hata hiyo tume ya uchaguzi haiwezi kulizuia hilo.
 
Kuelekea uchaguzi mkuu CCM haijapata anayejibu hoja za wapinzani. Wapi Makonda, Polepole hata Shaka.
Naona miwani na kitambi tu. Sioni hoja
Atajibu nini kwenye hoja iliyo wazi kabisa, na inayoeleweka na kila mtu: HAKI ya mtu kupiga kura na kura ikahesabiwa bila mizengwe yeyote, na mshindi akatangazwa bila shinikizo toka kokote. Ni mtu wa wapi huyo asiyeweza kuelewa kitu rahisi namna hii, isipokuwa Samia na Genge lake tu basi?

Ni nani mwenye uwezo wa kuielezea hoja hiyo ionekane haina maana yoyote katika uchaguzi ujao? Hao unao wataja hapo juu, akina Makonda, Polepole, wataugeuza vipi ukweli huu uonekane kuwa uongo?

Tena hata unamtaja Makonda?
 
Nyie mabwege hamzidi 5% wapiga kura wa kweli hawamo humu wako kwenye shughuli zao
Unaruhusiwa kuota ndoto mchana hasa ukiwa ww ni mgonjwa.hivyo nimekuruhusu ww uliye mgonjwa endelea na ndoto na mtu yeyote akikuuliza mwambie nimeruhusiwa kuota ndoto mchana.
 
Back
Top Bottom