Yani sioni chochote kinachofanyika zaidi ya kuwatia hasara wamachinga, wanawavunjia vibanda vyao alafu hawafuatilii mana ake nini ss, mwishowe wanajenga tena vibanda, leo asubuhi nimekuta apo kariakoo wamejaa, kwenye njia za watembea kwa miguu wamejaza bidhaa zao, yn hovyo hovyo, huyu makala hawezi kazi eti amebuni mbinu ya kuvunja usiku vibanda, wewe serikali unawaogopa raia? Una kila kitu cha kufanya raia wakaelewa kwamba ni makosa kufanya biashara barabarani na ikiwezekana jeshi litumike kuwaondoa kinguvu ili watu wazoee kutoweka biashara kwenye road reserve.
Tumejenga masoko makubwa lkn watu hawataki kuyatumia, pale kkoo kwa mfano lile machinga complex kama litajaa wachuuzi mana ake asilimia kubwa ya wachuuzi wataondoka barabarani, lile kisutu market pia likijaa litapunguza hii kero, tatizo Wamachinga hawataki kuamini kwamba sisi wateja ndio tunapaswa tuwafuate wao na co wao kutufuata cc, yn cc wateja na wao machinga tunapaswa tukutane sokoni na co barabarani.
Cha mwisho ni kwamba huyu mkuu wa mkoa hamna kitu na hatoshi kabisa kabisa kwenye hiki cheo cha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, huyu jamaa hana sifa za uongozi, hatoshi hata kwenye cheo cha mjumbe wa nyumba kumi achilia mbali cheo cha mkuu wa wilaya hapa Dar.
Sent using
Jamii Forums mobile app