BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wakati Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla akisema kuna mabasi 200 yaendayo haraka yanayoyotarajiwa kuanza kazi katika barabara ya Mbagala, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Dk Athuman Kihamia amesema hayo ni maelekezo ya Serikali.
Makalla ameeleza hayo leo Alhamisi Agosti 29, 2024 akiwahutubia wananchi wa Mbagala katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Maturubai wilayani Temeke, baada ya kufanya ziara ya siku 10 katika wilaya tano za Mkoa wa Dar es Salaam.
"Hii miundombinu ya barabara imekalimilika muda mrefu tangu nikiwa mkuu wa mkoa wa hapa (Dar es Salaam), nimefuatilia, niseme nisiseme? Mwenezi wenu nina habari nimefuatilia na wamenihakikishia wapo katika hatua ya mwisho kuleta mabasi 200 Desemba ili yaanze kufanya kazi," amesema Makalla.
Ameongeza kuwa, chama hicho tawala, kimezungumza na Serikali kuhusu mwenendo wa mradi huo na kuhakikishia kuwa utaanza Desemba kwa mabasi 200 ya kuanzia akiwataka watumiaji wa barabara hizo kuwa watulivu.
Hata hivyo, Mwananchi lilipomtafuta Dk Kihamia na kumuuliza kuhusu kauli hiyo, amesema kwa kuwa imetolewa na kiongozi wa juu wa CCM, ndiyo maelekezo ya Serikali.
MWANANCHI
Pia soma:Meneja BRT : Mradi wa Mwendokasi Mbagala-Gerezani umefikia 99%, kukamilika