JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
“unachokipanda ndicho unachokivuna wenzetu wameanza kulalamika tulitegemea haya mana hawakujipanga Sisi Viongozi wote kuanzia wa kitaifa mpaka ngazi ya chini tulienda kutoa hamasa ya kujiandikisha leo hii wenzetu wameanza kutafuta vijisababu watulie wafuate sheria sisi tumejipanga” alisema
Soma Pia: Makalla: Hatuhitaji mbereko yoyote Tutashida Uchaguzi kwa haki
MWENEZI CPA AMOS MAKALLA AJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAKAAZI LA WAPIGA KURA.
Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa CPA Amos Makalla ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wakaazi kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Ofisi ya Serikali za Mitaa TPDC Kata ya Mikocheni Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salam.leo tarehe 16 Octoba 2024.
Akizungumza na wakazi wa Mtaa wa TPDC Mikocheni mara baada ya kujiandikisha CPA Makalla amesema zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ni muhimu sana na amefurahi kutimiza haki yake ya msingi ya kujiandikisha na ameridhishwa na utaratibu wa zoezi hilo.
Amewataka Watanzania bila kujali tofauti za kiitikadi kujitokeza kwenye zoezi hilo kwani ni muhimu katika kuweka msingi wa maendeleo ya wananchi.
Aidha Katibu Mwenezi huyo ameongeza kuwa CCM inaridhika na jinsi zoezi hilo linavyoendelea.