Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Amos Makalla, anazungumza na wananchi kupitia Vyombo vya Habari kutokea Ofisi za Makao Makuu Dodoma.
Updates
Makalla asema maandalizi ya ya uchaguzi ndani ya chama yanaendelea vizuri na Wagombea watulie wakati wanaendelea na mchakato, uteuzi wa mwisho ni tarehe 28 Julai, 2025.
Amesisitiza kuwa wagombea waendelee kuwa watulivu hadi tarehe Julai 28 kwani pia mchakato huo unahitaji utulivu na wagombea ni wengi na haki inabidi itendeke.
"Watulie wali relax mpaka tarehe 28, sasa uteuzi wa mwisho utakuwa umefanyika na baada ya hapo kwenda kwenye kura za maoni" - Amos Makalla
Alipoulizwa sababu ya kufanya uamuzi huo Makalla ameeleza kuwa ni kutokana na uwepo wa watu wengi walioomba nafasi hivyo lazima wafanye mchakato huo vizuri ili kupata wagombea wazuri. Amesema waliomba udiwani ni 27,000 na ubunge 10,000.
Makalla amewataka pia watu wawe na utulivu kwa sababu bado hakuna mtu aliyekatwa wala kufyekwa hadi orodha itakapotoka Julai 28. Makalla amejibu hili akirejelea tukio la wananchi lilitokea hivi karibuni kushinikiza kukataa uteuzi wa mgombea.