MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 65
- 81
Amosi Makalla
Tangu kuteuliwa kwa Amos Makala kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi, Uenezi na Mafunzo akichukua nafasi ya Paul Makonda baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii na hata miongoni mwa wana CCM maeneo mbalimbali wameonekana kutokubaliana na uteuzi wake na kuona hakuwa chaguo sahihi kwa nafasi hiyo.
Naomba nitofautiane kidogo na mtazamo huo kwa kusema kwamba kwanza Amos Makala amekua ndani ya CCM kwa muda mrefu kuliko mtangulizi wake kwa nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya tawi, kata mpaka Taifani ndani ya UVCCM na CCM yenyewe. Hivyo anauelewa wa kutosha kuhusu siasa za CCM. Aidha, amepata kutumikia nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali kuanzia ubunge, ukuu wa mkoa katika mikoa mbalimbali hapa nchini hadi uwaziri hali inayompa uzoefu na uelewa wa masuala mbalimbali ya uendeshaji wa serikali pamoja na siasa za Nchi yetu.
Kwa kueleza hayo napenda kushauri tumpe Ndg Makala nafasi, muda na ushirikiano ili aweze kutekeleza kwa weledi majukumu yake. Naamini anaweza kuwashangaza wengi kwa kufanya vizuri zaidi katika nafasi hiyo.
Kila la heri Ndg Makala, huna mzigo mzito mabegani mwako hivyo tulia kama mtoto wa mjini kama tukujuavyo Papaa Makala utupe ladha mpya ya Uenezi.
Pia Soma:
- Amos Makalla Mwenezi mpya CCM Taifa, Ally Hapi Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi