Akizungumza kwenye kipindi cha uchambuzi pale clouds TV &FM.
Aliyewahi kuwa kiungo wa simba,azam,na team ya taifa amri kiemba amefichua wazi kwamba maandalizi ya mechi ya yanga na azam,wao azam huwa wanafanya kama finali tofauti na simba sababu kubwa anaijua yeye..
"Mimi nimecheza mpira azam na simba, nilipokuwa azam maandalizi ya mechi na yanga yalikuwa makubwa yaani kama finali, ila tukiwa tunacheza na simba basi inakuwa kawaida tu kama mechi zingine tu. Hivyo ingekuwa ni yanga na azam inapigwa basi kungekuwa na promo na maandalizi mengi"
Amehitimisha mchezaji huyo mkongwe..
Je, hii inakupa picha gani? Kwamba simba na azam ni kama mtu na mkewe? Ama azam ilianzishwa kumpa upinzani yanga?
Napata mashaka sana na mechi hiyo azam lazima wataachia wafungwe, hivi mara ya mwisho azam kuwafunga simba lini?
Hapa mechi hii inabidi ichunguzwe sana kiuhalisia simba hii mbovu na azam mbovu hapo azam anatakiwa ashinde laknil utaona wanaaachia wafungwe makusudi..