SoC01 Amri kumi (10) za mafanikio zitakazokutoa jehanamu ya umasikini na kukupeleka pepo ya mafanikio

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Sep 6, 2021
Posts
24
Reaction score
111
Habari zenu wanafamilia wa JamiiForums? Ni imani yangu kuwa mu bukheri wa afya na mnaendelea kushiba chakula cha maandishi kinachopikwa asubuhi, mchana na jioni na waandishi chipukizi kwenye jukwaa letu pendwa la uandishi wa mtandaoni wenye kuleta mabadiliko yaani "Stories of change".

Hakika, jukwaa limepambwa na linavutia kwa makala, insha na habari kemukemu zenye ubora wa maudhui na mitindo.

Ni jambo kubwa sana katika tasnia ya uandishi na hongereni sana JamiiForums kwa fursa na ubunifu uliotukuka. Kweli, nyie ni zaidi ya jamii!

Baada ya utangulizi huo mfupi wa salamu na pongezi, kalamu yangu ya Obama ya shilingi miambili (200) ijielekeze sasa kudadafua na kutathmini kinagaubaga amri kumi (10) za mafanikio zitakazokutoa jehanamu ya umasikini na kukupeleka pepo ya mafanikio.

Kama ilivyo ada, ulimwengu wa kiroho (Sayansi ya kiroho) inazitaja amri kumi (10) za Mungu kuwa ndiyo wakala atakayekupa tiketi ya kuingia peponi/mbinguni. Hivyo, ili mtu aende peponi ni lazima azitii na kuziishi hizo amri kumi za Mungu.

Katika Sayansi ya mafanikio (ulimwengu wa mafanikio) zipo pia amri kumi za mafanikio ambazo zitakupa tiketi ya kutoka jehanamu ya umasikini na kukupeleka pepo ya mafanikio.

Kwa kifupi, amri kumi za mafanikio ni mjumuisho wa mambo kumi mhimu ambayo ukiyafanya na kuyaishi lazima ufanikiwe.

Baada ya kukupa tafsiri ya amri kumi za mafanikio, niukaribishe ubongo na macho yako kuzisoma na kuzielewa amri kumi (10) za mafanikio nilizoziandaa kwa ajili ya afya ya mafanikio yako.

Moja, afya thabiti ya mwili na akili. Huu ndiyo uti wa mgongo wa mafanikio yote Duniani. Mafanikio yote ya mwanadamu huchagizwa na afya iliyo thabiti ya mwili na akili. Kama huna afya njema ya mwili huwezi kwenda shambani, kama huna afya njema ya mwili na akili huwezi kucheza mpira, kama huna afya njema ya mwili na akili huwezi kwenda kiwandani au sehemu yoyote ya kutafuta riziki na mkate wa kila siku, matokeo yake hutaingiza chochote na utakufa njaa. Kwa mifano hiyo michache, utakubaliana na mimi kuwa afya njema ya mwili na akili ndiyo amri namba moja ya mtu kufanikiwa.

Hivyo, ni jukumu lako kuilinda afya yako ya mwili na akili kwa virutubisho, vyakula na kanuni za kiafya kwani afya njema ndiyo msingi mama wa mafanikio.

Pili, ujenzi wa wazo ( mipango) thabiti. Kwa mjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa mafanikio, ujenzi wa wazo au mipango thabiti ni amri nyingine ya mafanikio yenye mamlaka na uwezo wa kukutoa jela ya umasikini na kukupeleka pepo ya mafanikio.
Kila mafanikio unayoyaona Duniani yalianza katika mawazo, kila biashara kubwa unazoziona zilianza katika mawazo. Utengenezaji wa ndege na vyombo vyote vya usafiri ulianza katika mawazo. Hata JamiiForums kuanzisha ukurasa na jambo kubwa kama hili msingi wake ni mawazo.

Vipindi vyote vya redio na runinga vyenye kutengeneza pesa, msingi wake ni mawazo.

Jitahidi sana kubuni na kuota mawazo mazuri ya biashara, ya kuongeza kipato, ya kuvuta wateja kwenye biashara na kadhalika kwani mawazo thabiti yana uwezo wa kukupa kipato na kubadili maisha yako.

Tatu, fanya kazi kwa bidii na maarifa. Watu wanaofanikiwa ni wale wanaoweka mawazo (mipango) yao katika matendo.
Hata uwe na mipango mizuri kama Miss Tanzania ila kama mipango (mawazo) hayo hayapo katika matendo, ni ngumu sana kutoka jehanamu ya umasikini.

Mawazo yenye kuleta mafanikio ni yale yaliyo katika matendo na siyo kichwani.

Mipango yenye kuleta pesa ni ile iliyoko katika matendo na siyo kichwani.

Sambamba na ufafanuzi huo, maandiko yanasema "asiyefanya kazi na asile" na wahenga wanasema "fanya kazi kama mtumwa ili uje uishi kama Mfalme".
Hivyo ni wazi kuwa sentensi "fanya kazi" kutajwa na kurudiwarudiwa kwenye vifungu vya bibilia na midomo ya wahenga kunathibitisha kuwa kufanya kazi ni nguzo nyingine mama ya mafanikio ya mwanadamu.

Nne, ukishindwa jaribu tena na tena. Mwanasayansi Thomas Alva Edison aliyegundua taa (bulbu) ya umeme ni mfano wa kuigwa katika amri hii ya mafanikio.

Thomas Alva Edison, alijaribu vifaa (nyenzo) tofauti tofauti elfu mbili (2000) ili kutengeneza hizi taa tunazozitumia leo na zote hazikufanikiwa.

Alijaribu tena na tena na baadae akafanikiwa na kuanzisha kampuni kubwa ya "General Electric Company".

Kata mti, kata kuni, kata umeme ila kamwe usikate tamaa.

Tano, nidhamu ya pesa (kipato) unachokipata. Ukitumia vizuri hicho kidogo unachokipata unaweza kufanya mambo makubwa kuliko hata anayepata kikubwa.

Kuwa na nidhamu ya pesa, usitumie pesa hovyo na ishi kwa bajeti.
Usitumie elfu kumi (10,000) kwa siku wakati unaingiza elfu nane (8,000) kwa siku.

Wakikuita bahili waambie wewe siyo bahili, waambie wewe ni Mchumi mwenye Shahada ya malengo kutoka Chuo Kikuu Cha Kujitambua.

Sita, kuwa na kitega uchumi zaidi ya kimoja. Ni hatari sana kutegemea chanzo kimoja cha mapato. Mfano, usitegemee mshahara tu, fungua vitega uchumi vingine vidogo vidogo vya kukuingizia pesa. Ndiyo maana Serikali haitegemei chanzo kimoja kukusanya mapato.

Vyanzo vingi vya mapato ni akiba itakayokuokoa kwenye dharura.
Kutegemea chanzo kimoja cha mapato ni sawa na mzazi aliyezaa mtoto mmoja pekee, siku mtoto huyo akifa anabaki bila mtoto.
Tengeneza vyanzo vingi vya mapato, utanikumbuka.

Saba, mshike sana mda usimuache aende zake. Mda ni mali, jali sana mda ndugu yangu. Vitu vyote vizuri unavyoviona Duniani ni matokeo ya matumizi mazuri ya muda.

Wanafunzi wote wanaofaulu vizuri mitihani yao ni matokeo ya matumizi mazuri ya mda.
Tumia mda wako vizuri na ishi kwa ratiba.

Muda ni kama pesa iendayo kwa mganga, ikienda hairudi tena.
Mda ni kama jino la ukubwani liking'oka halioti tena. Mda ukienda haurudi tena. Jali sana mda, usishinde kijiweni kubishana vitu vya kijinga. Kumbuka, haya tunayoyapitia ni nusu fainali, fainali kamili ipo uzeeni.

Nane, kuwa na mahusiano mazuri na watu. Maendeleo ni watu, mafanikio ni watu, biashara ni watu, siasa ni watu, mziki ni watu na kadhalika.

Maendeleo na mafanikio yoyote ya mtu, watu, kampuni, taasisi au chama chochote kile hutegemea sana mtaji watu.

Jifunze sana kuishi vizuri na watu kwani hili ndilo daraja utakalolitumia kuvuka kutoka jehanamu ya umasikini kwenda pepo ya mafanikio.

Tisa, itafute sana elimu usikubali ikuache.
Lengo la elimu siyo kupata kazi, lengo la elimu ni kupata maarifa. Kazi ni matokeo ya elimu. Elimu ninayoizungumzia hapa, siyo elimu ya darasani tu. Ninazungumzia elimu yoyote inayoweza kukupa maarifa yatakayokusaidia kupambana na maisha. Mfano, fani mbalimbali kama vile ushonaji wa nguo, ufundi, upishi na kadhalika.
Elimu nyingine ninayoizungumzia ni ile unayoweza kuipata kwa kusoma vitabu, kutembea na kushiriki semina na midahalo. Elimu zote hizi zitakupa maarifa na kukuongezea silaha za kupambana na umasikini.

Kumi, yote hayo yawezekana kwa kumuomba Mungu. Muombe sana Mungu, mtangulize Mungu kwenye mipango yako, yote yanawezekana.

Ahsanteni.
Na ninaomba kura zenu.
 
Upvote 12
Na Elivius Athanas.
0745937016.

Hongera sana kwa adiko hili..barikiwa sana.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
La mwisho lilitakiwa kuwa no 1
 
Back
Top Bottom