kanali mstaafu
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 4,318
- 4,105
Ni zaifu kama ndugai
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dada ipumzishe Ccm Sasa!Mnambebesha Amunike gunia la misumari sasa baada ya team CCM awamu ya tano kulamba flat
Wacha kumzingizia Amunike nuksi ni kwa ccm kutaka kutekeleza ilani ya chama kupitia bashite hadi kwenye mpira timu ya taifa.Wakuu,
Kocha wetu ni dhaifu mno kusoma mchezo na kubadili mbinu. Timu inacheza vile vile hata wapinzani wanapobadili mbinu. Mbaya zaidi kilema kikuu ni kocha kutojua namna ya kutumia viungo wetu. Hivi unamtumia kiungo kama Himid asaidie nini? Yule ni mkabaji tu na hawezi kuchezesha timu.
Badala ya kuingiza mtu wa kutuliza timu au kuongeza kasi ya mashambulizi unaingiza mkabaji tu na kufanya timu ielemewe. Nyoni aliomba sub mapema lakini haikufanyika hadi akalala chini na bado hawakufikiri haraka namna ya kujaza lile gap muhimu.
Amunike anafaa kuwa mkufunzi wa TFF kuendeleza program za soka lakini si mwalimu mzuri kabisa. Hakuna mechi aliyofanya sub za maana na akifanya ni too late damage inakuwa imeshakuwa kubwa na habadiliki haraka kwa kuwasoma wapinzani.
Wachezaji wanapambana wenyewe bila mbinu za ziada. Kwa timu hii hii angepatikana kocha anayewajua vizuri wachezaji wetu na anayeweza kubadilika kutokana na mchezo miujiza ingetokea.
Zambia walichukua hili kombe wakiwa hawana mastaa wa kutisha kulinganisha na wapinzani wao wengi. Technical bench ni msingi muhimu sana kabla hata ya timu yenyewe.
Wachezaji wetu wamepambana kwa uwezo wao wote lakini benchi la ufundi limewaangusha sana. Wasisingizie uzoefu mdogo, akina Okwi wana uzoefu gani? Jana tulihitaji uzoefu gani? Tatizo ni mbinu za kimichezo hatuna.
Hapana mlisema team ya Taifa inachezea ila I ya chama cha mapinduzi.Dada ipumzishe Ccm Sasa!
kula tano Tonge!Tatizo sio amunike tatizo Ni ccm
under total control of bashiteKocha wa Kenya alisoma game mapema na akafanya sub dakika ya 32 huku watu wakishangaa how come anafanya sub "mapema" hivyo. Baada ya hapo game ilichange kabisa. Kocha wetu yeye alikuwa amekunja mikono tu. Sijui ndio yalikuwa maagizo ya Prince DAB?
Dada ipumzishe Ccm Sasa!
Huyu hata challenge cup hawezi kuchukua. Simba wamemuacha Kotei sababu za kucheza kama Himid. Kiungo mkabaji ambaye hawezi kuchezesha timu inafanya timu ilemewe tu. Bora angeingia Fei Toto angeongeza pressure kwenye kiungo.