Amuua Baba yake kwa deni la Tsh. 2,297

Amuua Baba yake kwa deni la Tsh. 2,297

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Jeshi la polisi nchini Kenya, linamsaka mwanaume mmoja mkaazi wa kijiji cha Wina, Elburgon, Kaunti ya Nakuru kwa kosa la kumuua baba yake mzazi kwa madai ya kushindwa kumlipa deni la Ksh. 100 (Sh. 2297 za Tanzania).

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na familia hiyo, kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 aliingia kwenye malumbano na baba yake, mzee Wilson Chepkicho Yegon, akimdai Ksh. 200 alizomkopesha.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa Mzee Yegon mwenye umri wa miaka 66 alimlipa mwanaye Ksh. 100 na kuahidi kumalizia kiasi kingine hapo baadaye.

Mwanafamilia mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Kobilo Chepyegon aliyezungumza na Citizen ya Kenya, alisema kuwa baada ya kutoridhishwa na kiasi alichopewa, alianza kumshambulia baba yake kwa ngumi na mateke, na mwisho alimpiga na shoka hadi kufa.

Kwa mujibu wa majirani, mtuhumiwa huyo alikuwa na tabia ya kuwapiga wazazi wake wote wawili mara kadhaa.

Akithibitisha tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Nakuru, Naftali Korir ameeleza kuwa jeshi hilo limeanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo, na kwamba mwili wa marehemu umepelekwa hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.

Kaimu Kamanda Korir amesema msako wa Jeshi hilo utamnasa mtuhumiwa huyo; na amewaasa wananchi kutojichukulia sheria mikononi.


=======


Police in Molo, Nakuru County are probing an incident where a 30-year-old man allegedly killed his father over Ksh.100 debt owed to him at Lawina village in Elburgon.

According to Kobilo Chepyegon, the altercation started after their son demanded Ksh.200 owed to him but his father,Wilson Chepkicho Yegon, gave him Ksh.100.

The infuriated son then started assaulting the father before picking an axe and hacking him to death.

The assailant then fled after committing the act but was later cornered by irate residents who lynched him.

According to neighbours, the accused had, on several occasions, been involved in incidents that allegedly include beating up his parents.

While confirming the incident, Deputy County Commissioner Naftali Korir said that investigations are underway adding that the culprits behind the mob justice will be arrested.

The body of the 66-year-old man was moved to the Elburgon hospital mortuary while the son’s body was still at the scene hours after he was lynched.

The Citizens Kenya
 
Back
Top Bottom