Amuua mkewe, na yeye kujiua kisa mzozo mume kuuza vitu vya ndani

Amuua mkewe, na yeye kujiua kisa mzozo mume kuuza vitu vya ndani

Rashidi Hussein Mkayala Mkazi wa Mtaa wa Gemu Kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji amejinyonga kwa kutumia kilemba chake cha kichwani muda mfupi baada ya kumuua Mke wake, Bernadeta Cosmas(33) kwa kumnyonga chanzo kikitajwa kuwa ni mgogoro ndani ya ndoa yao.

Mwenyekiti wa Mtaa huo, Buswalu Mulumbu Mkama amesema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro uliotokea siku za nyuma ambapo Mke wa marehemu alifika kwa Mwenyekiti na kutoa taarifa ya vitendo vya Mume wake kuchukua vitu vya ndani na kuuza ambapo mara kadhaa kesi zao zilikuwa zikipelekwa kwake kwa ajili ya usuluhishi.

Mwenyekiti huyo amesema siku moja kabla tukio Mwanamke huyo alilala nyumbani kwake baada ya kukimbia nyumbani kwa Mume wake kufuatia kipigo alichopata kutoka kwa Mume wake ambapo katika tukio hilo alidai kunusurika kuuawa baada ya kukabwa shingo na waya wa umeme na alipopata nafasi ya kuchomoka alikimbia na kukimbilia kwa Mwenyekiti wa Mtaa.

Uchunguzi wa awali wa tukio hilo umeonesha kuwa Rashidi Hussein alimnyonga Mke wake kwa mikono hadi kumuua na baadaye kutoka nje ambapo alifunga mlango kwa nje na kurudi ndani kupitia dirishani ambapo alifunga milango yote na madirisha na yeye kujinyonga kwa kitambaa cha kichwani.

Source: Millard Ayo.
 
Duh!!wanawake viumbe wa ajabu sana,ukishaona mume wako anaaza kukupiga na wakati mwingine kukuacha hoi bin taabani ni bora ukachukua hatua.

Ona huyu mama sijui alitaka agundue nini toka kwa mme wake ikiwa taa nyekundu ilikuwa imeshawaka tayari lakini bado hakuaamini.
 

Janabi aachane na vyakula tushaelimika sasa ahamie na upande wa afya ya akili.
 

Janabi aachane na vyakula tushaelimika sasa ahamie na upande wa afya ya akili.
Nimecheka balaa
 
Back
Top Bottom