Amvumiliee??

Amvumiliee??

Helow Helow MMU, kuna shost angu ana boyfriend wake na wamedumu kwa muda wa miaka miwili sasa ila shida ya huyo bf hamjali in all aspect, shost keshavumilia mpaka maji yamefika shingoni. Ameshajaribu kumshape huyo bf wake na kila mara anakiri kosa na kuhaidi kubadilika ila haoneshi matendo... Sasa kaniomba ushauri jee aendelee kumvumilia make kuna mkaka mwingine anakuja kasi sana na keshaanza kumjali hata kabla ya mahusiano ila anachooogopa ni kwamba kuna marafiki wa bf wake wanafahamiana na mkaka wa pili anayekuja kwa kasi. Na hao marafki wanajua kabisa shost na mkaka wa kwanza ni wachumba ila vituko vya mkaka wa kwanza hawavijui kama mjuavyo "siri ya mtungi aijuaye kata". Anaogopa kuitwa kicheche afanyeje????

huyu dada lazima ajaribu kumjua huyo jamaa yake kabla hajaanza kulaumu hamjali.tumelelewa kutoka mazingira tofauti jamani.wengine mazingira tuliyolelewa hata kambi ya jeshi ina afadhali.so tafsiri ya neno "kujali" lazima itatofautiana.wengine utotoni tu unakaa mwezi hujaongea na baba wala mama wa kambo wakati unaishi nao nyumba moja.unamaliza matatizo yako kwa njia mbadala, sasa mtu kama huyu lazima awekwe sawa kwa muda mrefu kabla hajasimama na kuonesha anajali
 
helow helow mmu, kuna shost angu ana boyfriend wake na wamedumu kwa muda wa miaka miwili sasa ila shida ya huyo bf hamjali in all aspect, shost keshavumilia mpaka maji yamefika shingoni. Ameshajaribu kumshape huyo bf wake na kila mara anakiri kosa na kuhaidi kubadilika ila haoneshi matendo... Sasa kaniomba ushauri jee aendelee kumvumilia make kuna mkaka mwingine anakuja kasi sana na keshaanza kumjali hata kabla ya mahusiano ila anachooogopa ni kwamba kuna marafiki wa bf wake wanafahamiana na mkaka wa pili anayekuja kwa kasi. Na hao marafki wanajua kabisa shost na mkaka wa kwanza ni wachumba ila vituko vya mkaka wa kwanza hawavijui kama mjuavyo "siri ya mtungi aijuaye kata". Anaogopa kuitwa kicheche afanyeje????

pole sana mleta mada...naomba uweke details za kujaliwa anazolalamikia huyo shosti wako ili tuweze kujua kweli hajaliwi au she demands more than that na analazimisha kudekezwaa???...

pili.. mwambie shost wako sifa kubwa ya mwanaume sio kujali ni kupenda ndio maana watu wa musoma wakurya ili aamini kuwa mtu wake anampenda inabidi awe ana-mchapa na kumpigapiga kuonyesha wivu alonao juu yake( ikumbukwe mpaka sasa wivu ndio kipimo cha penzi la dhati mtu alokuwa nalo juu ya mwenzi wake) hakuna kipimo kipya cha penzi kilichogunduliwa duniani so far zaidi ya wivu.

tatu...mwambie shosti wako so far by 90% of my critical analysis inaonyesha yeye ni kicheche sababu ana-date kisiri na rafiki wa rafiki za bf wake..."adui wa adui yako ni rafiki yako ila rafiki wa rafiki wa bf wake ni rafiki wa bf wake pia...."....mwambie ajiongezee na aache kulialia kumtia shombo bf wake na kumsingizia hamjalii..kicheche plussssss.
 
Asiogope Kuitwa kicheche na mwanadamu, Bali amuogope Mungu anayempa uhai Bure na yeye anamlipa Madhambi
 
tatizo ni nini ? wote awape tu,siku wakifumaniana atakayekuwa wa kwanza kusamehe ndo waoane maana huyo atakuwa amefaulu kupita kwenye tanuru la moto na wataishi kwa amani daima dumu.
 
pole sana mleta mada...naomba uweke details za kujaliwa anazolalamikia huyo shosti wako ili tuweze kujua kweli hajaliwi au she demands more than that na analazimisha kudekezwaa???...

pili.. mwambie shost wako sifa kubwa ya mwanaume sio kujali ni kupenda ndio maana watu wa musoma wakurya ili aamini kuwa mtu wake anampenda inabidi awe ana-mchapa na kumpigapiga kuonyesha wivu alonao juu yake( ikumbukwe mpaka sasa wivu ndio kipimo cha penzi la dhati mtu alokuwa nalo juu ya mwenzi wake) hakuna kipimo kipya cha penzi kilichogunduliwa duniani so far zaidi ya wivu.

tatu...mwambie shosti wako so far by 90% of my critical analysis inaonyesha yeye ni kicheche sababu ana-date kisiri na rafiki wa rafiki za bf wake..."adui wa adui yako ni rafiki yako ila rafiki wa rafiki wa bf wake ni rafiki wa bf wake pia...."....mwambie ajiongezee na aache kulialia kumtia shombo bf wake na kumsingizia hamjalii..kicheche plussssss.

Kwanza, katika mawasiliano ambayo ndio nguzo pekee katika mahusiano rem"wapo mikoa tofauti. Shost amekuwa ni mtu wa kwanza kumtafuta jamaa kila mara kama asipofanya hivo jamaa kimya cku inapita akimuuliza anasema alikuwa busy "jamani ubize gani inamaana hapati hata muda wa kula akatext sms yenye maneno mawili tu"??? Shost amekuwa akimtumia zawadi mbalimbali lakini jamaa hajawahi hata kumletea handkachif na huwa anammshirikisha katika mambo yake hata ambayo hawezi mwambia mzazi wake au kuomba ushauri kwa mzazi wake lakini anampa jamaa kipaumble kuanza kumuuliza na kuomba ushauri ila jamaa huwa hamshirikishi chochote. anaweza safiri kwenda wilaya nyingine asiseme hata mkoa mwingine kimya kimya baddae akimuuliza upo wapi ndo anasema nipo morogoro shost anastuka moro umekwenda lini jamaa anamtell nimekuja juzi ama jana means hamjali wala kumpenda thats y hamshirikishi... hufanya mambo yake kimya kimya yaan haoni umuhimu wa shosht...

Pili: jamani kama mtu unamjali automatic utampenda sasa atasema anakupenda bila kukujali how comes, jamaa hana wivu hawezi hata onesha dalili ya wivu kila ambacho shost anafanya ye kwake aona sawa tu sasa hapo upendo upo wapi mkuu???????

Tatu: Sio kwamba tayari anadate na huyo mkaka wa pili ila mkaka wa pili kaonesha nia sasa anajipanga kujibu ndio au hapana na bado hajawa na mahusiano ya kimapenzi. Ni kwamba rafiki wa rafiki wa bf wake ndo amtaka yaan anaonesha nia ya kumtaka kimapenzi na hawajaanza kudate........

Mwisho: Shost hujitahidi kumtext sms nzuri za mapenzi lakini jamaa respond yake utafikiri anachat na man mwenzie, sasa kama mpenzi wako humwandikii maneno matamu unategema ataandikiwa na nani? aweza mtext i love jamaa anajibu thnx tena inshort hapo utasema shost anapendwa?? Wakiwa pamoja jamaa anakomaa tu kumwita jina lake "happy" hakuna maneno ya mahaba wala nini kha!
 
Ni Maalum Kwa Wadada Hasa Waliopo Kwenye Mahusiano Ila Bado Hawajaolewa Na Wana Mpango Endelevu Na Wenza Wao

Wadada Wengi Wanashindwa Kutambua Wapi Wanapendwa Na Wapi Wanadanganywa. Vigezo Vifuatavyo Vitakusaidia Kutofautisha Mwanaume Anayekupenda Na Mwenye Mpango Wa Kukuoa Na Yule Anaekutumia Tu Ila Hana Mpango Na Wewe.

1. Mawasiliano:
...
Mwanaume Anaekupenda Hawezi Kumaliza Siku Bila Kuwasiliana Na Wewes (Kama Hakuna External Factors Zinazosababisha Mawasiliano Yawe Mabovu). Kama Wewe Ni Mtu Wa Kupiga Simu Kila Siku, Kutuma Emails Lakini Mwenzio Haoneshi Ushirikiano Ujue Hapo Kuna Utata.

2. Ushirikishwaji:

Anaekupenda Ni Lazima Atakushirikisha Mambo Yake Mengi Yawe Makubwa Au Madogo. Unaweza Shirikishwa Kwa Namna Ya Kuombwa Ushauri Au Kupewa Taarifa. Kama Upo Kwenye Uhusiano Ila Unashangaa Mambo Yanafanyika Tu Bila Kuelewa Ujue Haupo Myoni Mwake, Haoni Kama Waweza Mshauri La Maana Na Haoni Kuna Umuhimu Wa Wewe Kujua.

3. Utambulisho.

Jiangalie Kama Unatambulika Kwa Ndugu, Rafiki Na Jamaa Zake Wa Karibu. Kama Muda Wa Kutambulishana Rasmi Kwa Wazazi Haujafika, Vipi Kwa Marafiki, Wafanyakazi Wenzie Au Makaka Na Madada!!. Unawafamu Marafiki Zake Wawili Wakati Anao 30? Utambulisho Huwa Ni Swala Gumu Kama Mwanaume Hakupendi Na Hajivunii Kuwa Na Wewe. Mwanaume Ambae Tayari Ana Mpenzi Mwingine Na Anatambulika Kwa Watu Wake Wa Karibu Ni Mzito Kukutambulisha Na Wewe. Inabidi Ustuke Hapo.

4. Mazingira.

Unapafahamu Anapoishi? Anapofanya Kazi? Maeneo Anayopenda Kutembelea? Kama Jibu Ni Hapana, Unahisi Ni Kwa Nini? Kuna Sababu Nje Ya Uwezo Wenu Zinazosababisha Usifahamu Hayo Ulishamwomba Ufahamu Ila Alikataa? Hapa Nakuachia Utafakari Mwenyewe.

5. Anakufahamu Kiasi Gani?

Kama Upo Na Mpenzi Lakini Haoneshi Interests Za Kutaka Kukufahamu Zaidi Inabidi Ujiulize Mara Mbili Mbili. Kwa Mfano, Mpenzi Wako Anajua Jina Lako Na Mahali Unapoishi Tu. Hajui Mazingira Unayoishi, Kazi Unayofanya, Hajui Ndugu Zako Hata Kwa Kuwasikia Ujue Huyo Mwanaume Hakupendi. Anaekupenda Ataandika Kitabu Kizima Kukudescribe Lakini Asiyekupenda Hata Page 1 Haitojaa.

6. Ubahili/Ubinafsi

Hapa Ni Kwa Wenye Wapenzi Wenye Uwezo Mzuri Kifedha. Angalia Kama Anasikiliza Shida Zako Na Kujaribu Kuzitatua. Inawezekana Hakujali Na Hakuhudumii Kipesa Kwa Sababu Ana Mpenzi Mwingine Ambae Ameelekeza Huko Matumizi Yake. Pengine Hakuamini, Anahisi Hata Akikuhudumia Utamtosa; Ila Kama Anashindwa Kukuamini Anawezaje Kukupenda? Mtu Wa Hivyo Hata Upendo Wake Ni Wa Mashaka. Kama Hana Uwezo Kifedha Je Anakuwa Na Wewe Bega Kwa Bega Unapokuwa Na Shida? Anayekupenda Atakujali Wakati Wa Shida Na Raha

asante sana mkuu kwa kunifungua macho.
 
Iwapo shosti wako ni wa kizamani hajaenda na wakati kwa kutowa mchezo hana haja ya kuwa na wasiwasi. iwapo kaenda na wakati basi mshauri aachane na kwenda na wakati kwani kila ajae ataendana na wakati halafu awe habadiliki kama huyo wa mwanzo.Wanaume wana tabia ya kutosheka na hichohico hasa iwapo hakuna mkataba. Kwa wengine uchumba ni kodi ya muda kufaidi hadi utakapoamua kukodi kwengine!
 
dah la kuvunda halina ubani mwambie atupe kule asonge mbele simba hafugiki ati.
 
aisee, mapenzi ya tamthiliya yana kazi sana... hivi kumbe kupitisha siku bila kum- call au text mpenzi ni issue sana eeh..
 
Kama ameshindwa kumrekebisha na hawezi kumvumilia bora abwage manyanga.
 
sasa kuna umuhimu gani wa kuwa kwenye uhusiano na mtu asiyekujali?

kutomjali kivipi,kifedha,kimapenzi au kingono.be specific.kuna wasichana wengine huwa wanapokuwa kwenye relatioship huwageuza wenzao ATM machine.
 
Amwambie ukweli huyo anayekuja kwa kasi uhusiano wa huyu kaka na kuwa ameshampiga chini, maana hata huyo rafiki wa mchumba akipeleka habari zitakuwa old news.

Otherwise amove on...life is too short.
 
Back
Top Bottom