Amzika mwanawe akiwa hai apate ‘kudanga’

JESHI la Polisi mkoani Geita linamshikilia Oliver Meshack (19), mkazi wa kitongoji cha Mapinduzi, kata ya Buselesele wilayani Chato kwa tuhuma za kumzika mwanawe akiwa hai, ili apate nafasi ya kuhangaika na wanaume kwa masuala ya ngono (kudanga).

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Safia Jongo ametoa taarifa hiyo leo alipozungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake na kumtaja mtoto aliyezikwa alijulikana kwa jina moja la Queen akiwa na umri wa wiki mbili.

Kamanda amesema mtuhumiwa alitenda ukatili huo Desemba 2, 2022, majira ya saa nane usiku, ambapo taarifa zilifikishwa kituo cha polisi Desemba 6 na wananchi walidai kushangazwa na kupotea ghafla kwa kichanga huyo.

“Walisema wanajua kuna binti amejifungua mtoto, lakini wana siku zaidi ya tatu hawamuoni huyu binti akiwa na huyo mtoto, kwa hiyo wana wasiwasi na wanatamani wajue huyo binti amepeleka wapi huyo mtoto.

“Jeshi la polisi lilimchukua huyo binti na kufanya naye mahojiano, ambapo alikiri kwamba ni kweli alijifungua huyo mtoto ambaye alimzika akiwa na umri wa wiki mbili,” amesema na kuongeza:

“Kutokana na yeye kazi yake ni kuuza baa na pia anajiuza mwili wake, kwa hiyo yule mtoto akawa ni kero kwake, akawa anashindwa kwenda kufanya biashara yake hivo akaamua kuchimba shimo, na kumfukia huyo mtoto akiwa hai.”

Chanzo: Habari Leo
Mimba miezi Tisa alikuwa anaishi vipi?
 
Aisee
 
Huyo ni kichaa,jela ni halali yake pia apitie milembe kwanza kukazwa nati,hiv jamani ule uchungu wa leba unavouma,hauelezek,[emoji26] mpaka unajifungua na unapewa mtoto ,ile furaha huwa hailezeki pia unavombeba mtoto kwa mara ya kwanza kifuani tena first born(km huyo aliouwawa na mamaake I hope alikuwa ndo first born kwa mamaake) yaani unakua na mapenzi na mtoto wako kuliko kitu chochote duniani especially zile wiki za mwanzo ndo upendo unazidi , sasa nashangaa huyu aliye ua wiki za mwanzo(za upendo mwingi)japo upendo upo siku zote,kwa mama na mtoto, ila hizo wik huwa upendo unazidi, ambazo mtu unalala kwa kushtuka shtuka kumcheck mtoto asije lala vibaya, akalalia pua akakosa hewa akafa,..ukija suala la miaka huyu binti bado ni mdogo, lakini ana roho ngumu km GAIDI.Mungu ampokee malaika aliyekufa kwa mateso makubwa bila kosa lolote,,[emoji120]The world is not fair
 
Nawalaum sana vijana wapiga mimba na kusepa.
watoto wenu wanauawa kikatili, na damu yao iko juu yenu pia.

mwanamke huna malengo nae yoyote, kwanini unamzalisha?
kwanini upige mimba kisha uikatae?

bikira zipewe thamani kubwa sana×2

na haya hayatakuwepo tena ..najua huwezi kunielewa upesi.
 
Huyo ni kichaa,jela ni halali yake pia apitie milembe kwanza kukazwa nati,hiv jamani ule uchungu wa leba unavouma,hauelezek,[emoji26] mpaka unajifungua na unapewa mtoto ,ile furaha huwa hailezeki pia unavombeba mtoto kwa mara ya kwanza kifuani tena first born(km huyo aliouwawa na mamaake I hope alikuwa ndo first born kwa mamaake) yaani unakua na mapenzi na mtoto wako kuliko kitu chochote duniani especially zile wiki za mwanzo ndo upendo unazidi , sasa nashangaa huyu aliye ua wiki za mwanzo(za upendo mwingi)japo upendo upo siku zote,kwa mama na mtoto, ila hizo wik huwa upendo unazidi, ambazo mtu unalala kwa kushtuka shtuka kumcheck mtoto asije lala vibaya, akalalia pua akakosa hewa akafa,..ukija suala la miaka huyu binti bado ni mdogo, lakini ana roho ngumu km GAIDI.Mungu ampokee malaika aliyekufa kwa mateso makubwa bila kosa lolote,,[emoji120]The world is not fair
Kumbuka Ilitabiriwa kuwa Katika karib na siku za mwisho "UPENDO WA WENGI UTAPOA"
 
Ndo maana nishasema mbegu zangu siwezi kumwagia mwanamke mshenzi mshenzi.

Heri ni vae condom mbili ila sio nimwagie mwanamke mbegu ambaye sio mke wangu.
 
Mambo mengine yanatuathiri kisaikolojia hata tuliokuwa mbali na tukio. Binadamu tupunguzeni ukatili, tutajibu nini siku ya mwisho?!
 
Back
Top Bottom