Ana B.A Ed lakini mwalimu wa shule ya msingi

ng'wanankamba

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
346
Reaction score
120
Wadau, nina ndugu yangu alisomea ualimu Marangu T.T.C na kuhitimu mwaka 1989, aliajiriwa kuwa mwalimu wa shule ya msingi grade A, baada ya muda alijiendeleza na kusoma diploma ya ualimu na akawa Mratibu wa elimu kata. Baada muda, alipata nafasi ya kwenda kusoma shahada ya elimu yaani B.A Ed katika Chuo Kikuu cha Mwenge kilichoko Moshi. Amehitimu mwaka juzi na aliporipoti kwa mwajiri, kapangiwa kwenda kufundisha shule ya msingi! Kweli Tanzania tumefikia level ya kuwa na walimu wa shule ya msingi ambao ni wahitimu wa chuo kikuu au ni fitna tu? Amejaribu kufuatilia kuhusu suala hilo lakini jibu alilopata ni kuwa yeye ni mwajiriwa wa Wizara ya Elimu kurugenzi ya elimu ya msingi na hapo kwenye ualimu wa shule ya msingi ndo stahili yake hata kama atakuwa na Phd! Wadau, kama kuna mdau yeyote anayejua kuhusu hilo kama ni kweli au la, naomba anisaidie.
 
Yawezekana mwajiri hana nafasi nyingine kweli, au labda ni fitina - la msingi ni kwamba kama huyo ndugu yako haridhiki atafute ajira mahali pengine aachane na mwajiri huyo.
 
Mkuu, napata shida kuamini kuwa Wizara ya Elimu haina nafasi kwa mhitimu wa Chuo kikuu zaidi ya ualimu wa shule ya msingi! Suala la kutafuta ajira sehemu nyingine kwake kidogo linakuwa gumu akifikiria sula la mafao yake ya baadae kwani amekuwa mwajiriwa wa Wizara ya elimu toka 1990.
 
kikubwa hapo mnachopaswa kuangalia ni stahiki ya mshahara, je analipwa scale ambayo ni equivalent kwa graduate au analipwa ya cheti? binafsi nlianza kazi kama mwalimu wa cheti but this tym ni graduate ninalipwa TGTS E ambayo ni daraja moja mbele la entry salary kwa graduate........, kikubwa MSHAHARA WA SERIKALI HAUTOSHI, GRADUATE PAMBANA UTAFUTE PART TIME , SEKONDARI KIBAO ZINATAFUTA WALIMU!!! Unadhani viongozi wa wilaya wana Diploma watakuachia nafasi zao kirahisi???????? Halmashauri yetu ina Graduates zaidi ya hamsini tupo zetu Msingi na maisha yanasonga!!!!!
 
Hivyo ndo inavyotakiwa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hakuna shida kwani ajira yake ndo iko huko. Kwani si amepunguziwa kazi.? We unadhani mambo ya kufundisha virai na vishazi ni rahisi. Mitoto yenyewe inakula bangi inaweza kukupiga bure! Wa kike ndo kabisaaaa, we unafundisha wao wanafikiria: yule mwalimu atanitosha kweli!! Tena wanajadiliana na wenzake.
 
Hii imetokea kwa wengi tu, ingawa ni kinyume cha sera ya elimu ya mwaka 1995. Binafsi nilikutana na hili mwaka 2004, lakini baadaye nilitoka huko. Mwambie nduguyo, ni muhimu kwake kwanza kuhakikisha anapata kile anachokistahili na anatoa huduma ipasavyo. Pili, asisite kufuatilia kwa afisa elimu wa wilaya aliyomo, ili kuona uwezekano wa kuhamishiwa katika elimu ya sekondari au kwingine anakoweza kutumia vizuri zaidi kiwango cha taaluma alichonacho. Aidha, adumishe moyo wake wa kujiendeleza zaidi kielimu.
 

tatizo c kufundisha primary tatizo ni je analipwa mshahara kutokana na kiwango chake cha elmu.? Na jee kwan uliambiwa kuwa mwl wa degree hawez kufundisha primary?
 

wewe ndio unajua.
 
ili kukuza kiwango cha elimu nchini, ilikuwa inatakiwa waalimu wote wa shule za msingi wawe na elimu ya kiwango cha shahada ya kwanza. Sambamba na ajira hiyo, waalimu hao wapewe mishahara mizuri na maslahi mengine yaendanayo na kiwango chao cha elimu na kazi. Tukifanya hivyo, tutaweza kukuza ubora wa elimu. Katika nchi ya Finland, huwezi kuwa mwalimu wa shule ya msingi kama huna Masters degree!! Hawa wenzetu ndio wanaongoza kwa kutoa elimu bora katika nchi za Ulaya.
 

Chukueni ushauri huu kutoka kwa Mwalimu Kahangwa!
 

Well said mkuu, sijui kwanini walio wengi tunapenda kuhusisha kupata shahada ya ualimu na kufundisha sekondari (specifically A-level) and sorts. The underlying principles ni zilezile, so long as unayo degree (BED, BAED, etc.) na unapata mshahara stahiki kwa kiwango chako cha elimu na uzoefu, sidhani kama ina-make any difference kufunza shule ya msingi, sekondari au chuo.

Na ninaamini njia pekee ya kuinua kiwango cha elimu nchi hii ni pale tutakapokuwa na walimu 'wataalamu wabobezi' kwenye fani yao kitaaluma. Shule ya MSINGI (emphasis), inapaswa kuendeshwa na wataalamu hasa. Hapa ndipo matatizo yote ya kimfumo ya uendeshaji wa mfumo wa elimu (rasmi na usio rasmi) yanapochukua mkondo. Msingi ukiandaliwa na watu wasiokuwa na utaalamu stahiki utapelekea hata mwendelezo wa juu kuwa wa tabu na usiokuwa na tija.

Tatizo ni aina ya mfumo tulionao ambao unamweka mwenye digrii juu zaidi (hata kama ni digrii moja tu), unamfanya aonekane na 'kujisikia' wa hali ya juu na kujiondoa katika hata kusaidia yale ya MSINGI.
 

Maslahi mengine ya msomi mwenya degree ni gari ya kutembelea ya kifahari, nyumba nzuri hasa ghorofa, mshahara unaozidi ule wa mbunge. Maana ni aibu kwa graduate kutembelea baiskeli au pikipiki au gari chakavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…