ng'wanankamba
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 346
- 120
Wadau, nina ndugu yangu alisomea ualimu Marangu T.T.C na kuhitimu mwaka 1989, aliajiriwa kuwa mwalimu wa shule ya msingi grade A, baada ya muda alijiendeleza na kusoma diploma ya ualimu na akawa Mratibu wa elimu kata. Baada muda, alipata nafasi ya kwenda kusoma shahada ya elimu yaani B.A Ed katika Chuo Kikuu cha Mwenge kilichoko Moshi. Amehitimu mwaka juzi na aliporipoti kwa mwajiri, kapangiwa kwenda kufundisha shule ya msingi! Kweli Tanzania tumefikia level ya kuwa na walimu wa shule ya msingi ambao ni wahitimu wa chuo kikuu au ni fitna tu? Amejaribu kufuatilia kuhusu suala hilo lakini jibu alilopata ni kuwa yeye ni mwajiriwa wa Wizara ya Elimu kurugenzi ya elimu ya msingi na hapo kwenye ualimu wa shule ya msingi ndo stahili yake hata kama atakuwa na Phd! Wadau, kama kuna mdau yeyote anayejua kuhusu hilo kama ni kweli au la, naomba anisaidie.