VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Wana-JF,nikiri kuwa ni mara yangu ya kwanza kuandika kwenye jukwaa hili.Suala hili linamhusu rafiki yangu wa karibu aitwaye Eddock.Eddock alikuwa na mahusiano na msichana mmoja hapa jijini Dar es Salaam.Mahusiano yao ya kimapenzi yalidumu kwa miaka miwili;2010-2012(mnamo mwezi Aprili).
Nilivyokuwa nawaona,walikuwa wanawezana(naogopa kusema walikuwa wanapendana).Msichana wa Eddock alikuwa na mipango ya kusoma.Walitaarifiana.Wakakubaliana.
Ghafla bin vuu,Eddock akapokea simu ya msichana wake akimuomba wakutane ili waongee kuhusu suala moja muhimu kwao.Wakakutana.Msichana bila kusita akamwambia Eddock kuwa ameamua kuachana naye Eddock.Sababu zikaulizwa.Msichana akasisitiza kuwa ameshaamua na hana sababu zozote.Akamtaka Eddock atafute mchumba aoe ili amsahau kabisa kuwa waliwahi kuwa pamoja.
Eddock akakubali matokeo.Akaendelea na zake.Siku si nyingi,akapokea simu ya yule msichana akiomba amkopeshe laki moja.Akamkopesha.Halafu,msichana akaanza tabia ya kupiga simu mara kwa mara,kubeep,kusms na kumtafuta hata kwa rafiki zake Eddock ili amwone.Tabia hizo ndizo zimetawala hadi leo.
Sasa waungwana,kwa wanaoweza kutafsiri matendo haya,huyu msichana anamaanisha nini hasa?