Ana miaka 12 bila kuugua,,je kuna madhara ya kiafya?

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,189
^^
Jana nimepata mgeni aliyekuja kunitembelea.Lakini alikuja kunijulia hali alipopata habari kuwa naumwa,na nipo naendelea na dozi.
Lakini jambo moja lilinishangaza pale aliposema '...nakuonea wivu,walau hata unaugua,mimi sikuwahi kuugua tangu 2001,yani hata kusikia homa wala kichwa kugonga.."
...
Awali nilidhani utani lakini mkewe na shangazi wa Bwana huyu walithibitisha hili.Na mwenyewe anasema "..watu wanasema siku nikiugua ndio kifo changu,,jambo hili linanitia hofu sana.."
...
Jamani wataalam wetu,jambo hili lina madhara ya kiafya? Au ni jambo la kawaida tu?
...
Kwa JF DOCTORS
CC: mimi49 MziziMkavu BAOTISTA
^^
 
Last edited by a moderator:
pole sana Himidini! Ni jambo jema hakuna madhara ya kutougua huende kinga za mwili wake ziko vizuri na wema wa Mungu.
 
ukiwa na lishe nzuri utaugua mara chache, ila ikatokea unaugua, upo hatarini, lazima utaugua sana
 
Immune defence(white blood cells) ndio zinazotuzuia kupata infections na zinatukinga na magonjwa tofauti.
Sidhani kama kuna tatizo mtu asipougua muda mrefu ni ishara kwamba ana immune defence madhubuti,ila kuna hatari ya kwamba akija kuugua ataumwa sana kwasababu immune defence yake haijakuwa callenged kwa muda mrefu..Jinsi tunavyopata infections tofauti haswa viral infections ndivyo tunavyopata antigens ambazo zitazuia kupata infection ileile upya...
 
its all about body immunity
kma kinga iko vizuri magonjwa utayaskia kwa jirani
on contrary ukiona magonjwa hayaishi
either your immunity is compromised au una upungufu wa kinga mwilini( immune deficiency)
 
Wengine wanaugua bila kujijua.

Kibongobongo mtu anaweza kukuambia hajaugua miaka 12 wakati hajawahi kufanya checkup hata ya blood pressure tu au kupima uzito miaka yote hiyo.

Na ana permanent malaria hata hajijui maana kashaizoea.

Kuugua anataka mpaka ashindwe kutembea.

Mtu hata blood group hajijui, hajaenda kwa dentist in 12 years, hajui uzito wake, ngwengwe hajapima naye anaweza kukuambia hajaugua vile vile.

Huku kila siku anabanja!
 
Nasikia watu wa namna hiyo ujue wana blood group O.

Mkuu inawezekana.. kwani kuna Mjomba angu inasemekana hajawahi kuugua tangu Mwaka 1972, hadi hii leo mm na umri wangu sijawahi kumsikia akiumwa na ugonjwa wowote na yeye pia ana blood group 0.
 
Kawaida sana, baba yangu ana miaka 67 lakini sijawahi kumuona anaugua, yeye ni mwendo wa whisky tu on daily basis na ameturishisha watoto wake wote na tunafanyiwa check-up kila baada ya miezi miwili na wote ni group o plus. Lakini mafua ndo yanatutesa sana. Maana hata wife na mwanangu mafua yanawalaza kabisa.
 
Mkuu Himidini jibu la swali lako ameshakujibu Mkuu mimi49 ninaongezea ukitaka kuwa na afya vizuri pendelea kula vyakula visivyokuwa na mafuta mengi wala chumvi nyingi ,kula matunda na mboga mboga za majani kunywa sana maji ya uvuguvugu, fanya mazoezi au tembea kwa miguu, pata usingizi wa kutosha usiwe na Stress basi hutaweza kuuguwa tena.

Mkuu Bigbro kuhusu hayo mafua jaribu kila siku asubuhi kabla ya kula kitu pendelea kula punje 1 ya kitunguu Saumu Mafua yako yataondoka . Na ukitaka usiumwe jaribu kuwa kila siku unakula hiyo punje ya kituu samu ni dawa tosha ya kukinga na kila maradhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…