Kwa songea si mwenyeji sana ila ingekuwa mimi huku nilipo ningefungua moja wapo kati ya haya.
1.Duka la maji la jumla(sio zile godown)
na kuuzia wafanyabiashara na wachuuzi wa hapo town.
2.Boxer/TVS pikipiki used kwa 1.5 million na kuanza kupiga mzigo na kuweka 300,000 Kwa mwezi.(Pia ukichoka unauza chombo mana ni asset)
3.Naweka Tigopesa na Mpesa Tu.huku nikiacha mitandao mingine pembeni kwanza ili nikuze mtaji,chenji unaweka kibanda hapo.( ila unaangalia na hapo ulipo mtandao gani unatumika sana)
4.Kupakia dumu za alizeti Singida au dodoma na kuleta na kufungua fremu hapo ulipo na kuuza huku ukisupply kwa masoko ya hukohuko.
5.Gold Fisher ll. ningenunua hichi kifaa cha kupimia dhahabu(tena songea kuna machimbo).
Kwa siku ukiitwa ni laki 1 tena umekaa unafuatwa.
-Tengeneza connections na wachimbaji kila wiki hukosi 400,000 narudia kwa wiki.
6.Biashara ya Mini Kiosk
Watu wanaidharau ila ina hela.Unauza vitoko na viroba na sigara (smart gin, na takataka zingine)
Kuna jamaa namfahamu anauza kwa siku 30,000 faida ni pasu pasu peleka stendi au machimboni au sokoni.
Asante