Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao wanajamii na ndugu kumfahamu haihalalishi kua huyo ni mumeo. Kwanza unapata wapi guts za kuishi na mume wa mwenzako hadi unamtambulisha kwa ndugu, mbona unamkosea heshima mwanamke mwenzako mwenye mume wake.
Wewe utabaki kua mchepuko/ baby mama.
Hapo kama huna ndoa utaachiwa manyoya labda uende ustawi wa jamii.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ninyi hua ni wanawake wapumbavu sana. nasema WAPUMBAVU kwa macho makavu maana hiki kilinitokea,baada ya kumpa ujauzito mwanamke ambaye alikua anajua kabisa mimi ni mume wa mtu na sikumlaghai, nilimuweka wazi kua nina mke na tukazungumza kua asije kuzaa mtoto tukakubaliana maana kwanza kabisa alinipenda yeye mwenyewe tukiwa kazini huko mkoani...
Anajikosea heshima mwenyewe wala sio mke wa jamaa. Nduguze watamuona Hana adabu na kashindwa kupata mwanaume wake amuoe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha wewe Mzee upo?
Heshima yako Baba. Kule kwetu mwanaume anaamkiwa shkamoo kubwa kabisa (tuko kimkakati zaidi).
Nimefurahi kukuona hapa.
Kwahiyo wewe ukitaka kuzaa na mtu lazima uweke makubaliano...[emoji3][emoji3]Ulichemka sana kumzalia mtoto bila mapatano.kwa sasa usimtibue kabisa maana hutaamini kitakachofuata.cha msingi ukitaka uendelee na jamaa ni kuhakikisha unamlindia ndoa yake kwa kila hali.
Mtu anayechepuka usidhani haipendi ndoa yake.Yoyote anayechepuka akigundua mahusiano yenu yanaelekea kuharibu ndoa yake. Anachofanya ni kukuacha na kutafuta mchepuko mwingine...
Hayo umewaza wewe huenda ndio unayofanyaga wewe....na katika quote yangu sijaconfirm kama hatozaa tena au milele yoteKwanini unaconfirm kwa kujiamini kabisa kwamba mkewe hana uwezo wa kupata ujauzito, ushamuendea kwa babu nini?
Wewe ni MPUMBAVU..amini hivyo na si mimiKwa maoni yangu, mpumbavu ni wewe kwa kuwa hukutaka kutumia kinga.
Hapo alipata mimba tu lakini hujiulizi ingekuwaje angekuambukiza ukimwi?
Endapo una mke, ridhika naye na ukishindwa, please condomize.
Samahani kwa kutumia lugha kali ingawa kwenye sentence yako ya kwanza umetumia lugha hiyo kwa huyo mwanamke.
Kambaku umemaliza. Hii tabia ya mleta mada kujilengesha ili apate mimba alafu eti adai kutunzwa na mwanae ikome kabisa.Kwa jinsi unavyosema eti mwaka jana ukafanikiwa kupata ujauzito maana yake ni kitu ulikuwa unakitafuta kwa jamaa, umejilengesha. Hii ni mbaya sana, wewe unajijua ni mchepuko na jamaa ana mke we unajibebesha limimba. Na hakika ndani ya akili yako ukawaza kwa kuwa mkewe hajazaa basi tayari kwa wewe kuzaa na jamaa umejihalalisha na bila haya unauliza eti haki zako...
Hyo comment yangu haikuwa hvo moderator aliedit comments nyingi kwenye Uzi huu na nyingine kufuta ambazo zingemsaidia huyu dada, so my comment were edited na nyingine kufutwa maana Mimi sikumshauri hata kwenda ustwai nilimwambia a relax akifikiria mke wa ndoa kujua ndo atapendwaWanawake huwa mnashauriana vibaya.
Cha muhimu ulipaswa kumwambia azidishe mapenzi kwa baba mtoto wake ili mzee amkubali na ikibidi a pay attention zaidi kwake. Suala la kuzaa na mume wa mtu ni kosa ila kosa kubwa zaidi ni kuwa na mahusiano naye. Sasa hilo limeshatokea, finding solution sio kwenda ustawi wa jamii kwa vile hajasema amenyimwa matumizi.
Huyo mtoto atakosa matunzo na mapenzi ya baba endapo huyo mwanamke ataanza mambo ya ustawi wa jamii au dawati la jinsia.
Uvumilivu hulipa.
Missing you.
Kulikuwa na wimbi kubwa sana la watoto waliingia humu JF nilikuwa nawasubiri wakue, naona wengi wameshakuwa wakubwa kiakili sasa.
Thread ilikuwa inaharibiwa within a minute!
Swali lako limekaa upande mmoja, jiulize ukifa wewe mwanaume atakua na haki ya kurithi chochote chako kisheria?