Ana tezi dume na amekataa kufanyiwa upasuaji. Tufanyeje?

Page 94

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
5,204
Reaction score
15,207
Wasalaam Wakuu wa Kaya,
Moja kwa moja niende kwenye kilinichonituma kujitwika nyuma ya keyboard na kuanza kushusha madude.

Kama wengi tunavyoufahamu ugonjwa huu uliopata umaarufu sana hapa Mjengoni JF baada ya Rais Mstaafu Mh. JK kuumwa na kulazimika kwenda kufanyiwa upasuaji huko majuu.

Ugonjwa huu umempata pia mmoja wa jamaa zangu wa karibu kabisa. Baada ya kufanyiwa vipimo vyote (usiniulize njia ipi imetumika kuutambua) akagundulika kuwa ana ugonjwa tajwa na daktari kumtaka akafanyiwe upasuaji wa haraka.

Jamaa kwa uoga wake au imani yake akakataa katakata kufanyiwa upasuaji ili kuiondoa.

Tukimuuliza nini sababu anadai hawezi kukubali bila sababu yoyote.

Tumekaa na kutafakari,je tumlazimishe kufanyiwa upasuaji bila hiari yake? Je,sheria inasemaje kuhusu hali ya namna hiyo?
Kuna madhara gani kumtibu mtu ambaye hajaridhia?

Je ikishindikana kufanyiwa upasuaji,ni dawa gani inaweza kumsaidia kiumbe huyu?

Ahsanteni sana na nategemea Ushauri makini!
 
Mwacheni tuu
 
Yaani alikubali kupima anakataa kutibiwa?

Kama ni mtu mzima achaneni naye, yakimfika ataenda mwenyewe.
 

Ukiona Mgonjwa nyie mnamwona anaumwa sana halafu mnamwonea huruma lakini yeye wala hajali, mbishi wa kupata matibabu na mkorofi ni dalili tosha kuwa " Israeli " hayuko mbali katika kuja kuichukua " Roho " yake. Kama kwao Kijijini ni mbali anzeni tu kuchangishana muokoe gharama za kumsafirisha pindi Israeli akifanya yake au kama hapo alipo ndiyo mnadhani mtamuhifadhi ni vyema mkaanza tu kufanya taratibu zingine za Mirathi huku mkijua na gharama ya kukodi Maturubai na vikolombwezo vingine vya safari ya mwisho on earth.
 
Kama kakubali kupimwa... Anakataaje kufanyiwa upasuaji.. [emoji57][emoji57][emoji57]..???... Bora angekataa mazima... Ijulikane hajaguswa kabsaaa...!!!!
 
Vidonge vya tamsulosin (Urimax) huwa vinatumika kumanage symptoms.. Daktari amuanzishie wakati negotiation zikiendelea
 
Anione mimi nimpe dawa pasipo na kufanyiwa Operesheni na atapona.Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Kasha tibiwa kama hajapata tiba nicheki kwa whatssap number 0628944712 nitakusaidia bure
 
Subirini afe tu km kakataa. Hamna jinsi
 
Hajaumwa huyo bado, muacheni mwenyew nyie ndio mnaona anaumwa ila yeye bado hajajickia kuumwa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…