Mkuu 'Rabbon', naomba msamaha kwanza kwa swali hili ninalo kuuliza hapa; kwa sababu mara nyingi sana nimetatizwa na jambo hili.
Je, mkuu, nimeona umepewa alama ya "LIKE" kwa hayo uliyo andika kwenye bandiko hili nilililo 'quote' hapa. Hii 'LIKE' uliyo pewa na 'raraa reree' inahusu nini hasa?
Huyu mtu siku hizi namchukulia kama "mchafuzi wa mazingira".
Haiwezekani kamwe mtu ukawa unaingia JF kwa nia ya kuweka tu alama hiyo hiyo kila bandiko bila hata ya kusoma bandiko linaeleza jambo gani.
Nimeona nipitishie swali langu kwako, maana yeye siwezi kumuuliza chochote, maanake haandiki kitu humu, yeye kazi ni kuweka hiyo alama moja tu ya 'like' kwa kila bandiko, bila kujali lina ujumbe gani.
Sitashangaa kamwe nami hapa nikikuta tayari 'like' yake.
Nitashukuru nikipata jibu.