Anaandika mchambuzi Moshi Jr

Anaandika mchambuzi Moshi Jr

The introvert

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2023
Posts
701
Reaction score
1,522
PERFORMANCE YA KUFYEKA VICHAKA!!!!

✍🏻Hii ndio Total Dominance iliyokamilika kwa Yanga kufanya vitu vingi kwa usahihi kuanzia filimbi ya kwanza hadi 90 mins , CBE SA kwa namna walivyokuwa wakicheza wangeweza kuokota wavuni hata 8 , 9 au 10 easily. Yanga walikuwa wanafanya vitu vipi kwa usahihi ?

1: Pasia mpira kwa usahihi sana
2: Walihakikisha kuna movements nyingi ili kumpa options mwenye mpira mguuni ( FBs , CBs , MFs , CF )
3: Walihakikisha mpira unatoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa haraka sana kwanini ? Ili kuvunja mistari miwili ya nyuma ( Walifanikiwa sana )
4: Pale walipokuwa wakipora mipira wanakuwa na idadi kubwa kuelekea golini kwa mpinzani ili kutafuna spaces zilizo wazi
5: Kushinda mipira ya pili ( Second balls )
6: Hapo ilikuwa ni kuangalia ni kwa namna gani watakuwa wafanisi golini , aisee Yanga ni wakatili sana yani bang! Chuma 6 kambani . Timu kubwa zinafanyaga hivi

✍🏻CBE SA waliingia na kuzuia na midblock ( yenye sifa ya lowblock ) ili kuwa compact kweli kweli yani kubana zaidi / kuwa finyu kwa kufunga spaces katika nyakati mbili muhimu ( attack and defend ) , lakini walishindwa kuifanya / kuidumisha kwasababu walikuwa hawapo aggressive kushinda mipambano yao ( ukislow down unakutana na adhabu ) ndicho kimewakuta CBE SA . GAME OVER

NOTE

1: Mudathir aisee amecheza sana , tanki la mafuta lipo la kutosha 🔥

2: Chama anadhihilisha kuwa ni bonge la player wa michuano mikubwa 🔥

3: Bacca + Job , kazi nzuri sana ( nafikiri CBE hawajapata on target ) aisee🤔🔥

4: CBE watakuwa wamepata funzo " ni muhimu kuzingatia space na distance " tena dakika zote bila kusinzia hata kidogo

5: Aziz Ki unaweza kumuelezea vile unataka aisee 🔥

6: Yani wachezaji wote wa Yanga wamemwaga jasho la kutosha / wamefanya kazi nzuri sana 🔥

7: Hao Makundiiiiiiiii " CAFCL " 😀🔥

FT: Yanga SC 6-0 CBE SA
1726948308853.jpg
 
Back
Top Bottom