Anachofanyiwa Dangote na Serikali ya Nigeria kinanipa wasiwasi na utimamu wa akili zetu

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
2,748
Reaction score
5,112
Anachofanyiwa Dangote na serikali ya Nigeria na viongozi wake ni masikitiko. Napata mashaka juu ya utimamu wa akili zetu.

Baada ya kutokea mkombozi wa kiteknolojia [Huawei] China serikali ya China ilisimama na Huawei na kuhakikisha kwa namna yoyote Huawei inasimama hata pale ilipopata tishio la kuangamizwa na Marekani wakomunisti wale hawakusita kuipa support ya ndani na nje Huawei isiangushwe.

Wachina walijitoa kuilinda Huawei kuanzia kukamatwa kwa Boss wa mtoto wa Huawei Canada mpaka wakamrudisha China cases zote China walisimama bako kwa bako na Huawei.

China wamepigana na wanapigana Giant huyu wa teknolojia asianguke maana yeye ni moja ya National symbol kubwa ya China kiteknolojia huwezi kutaja mafanikio ya teknojia China bila kuigusia Huawei naweza hata kuiita Huawei ni kampuni ya nchi kutokana na mchango na nafasi yake katika mafanikio na maendeleo ya China kiteknolojia.

Kinacho nishangaza ni nini? Ni hiki anacho pitia Dangote kuhusu uwekezaji wake wa refineries nyumbani kwao Nigeria ili kutibu tatizo la mafuta lakini uwekezaji huo unageuka msiba kwake.

Hakuna wakati muhumi serikali ya Nigeria ilipaswa kuibeba kampuni ya Dangote kama kampuni ya nchi kushinda sasa.

Walipaswa kwa namna yoyote kuhakikisha Dangote group haianguki au kuangushwa na yoyote ila kwa yanayo endelea napata mashaka juu ya utimamu wa akili.
 
Na alichotufanyia wabongo namna vile alivyoingia na kuwa mwekezaji hatutakaa tusahau..Alisha mkono na chama chawala akapita shortcut akakatq fungu nene mambo yakaenda
 
Anacho fanyiwa Dangote na serikali ya Nigeria na viongozi wake ni masikitiko.

Napata mashaka juu ya utimamu wa akili zetu.

Baada ya kutokea mkombozi wa kiteknolojia [ Huawei] China serikali ya China ilisimama na Huawei na kuhakikisha kwa namna yoyote Huawei inasimama hata pale ilipopata tishio la kuangamizwa na Marekani wakomunisti wale hawakusita kuipa support ya ndani na nje Huawei isiangushwe.

Wachina walijitoa kuilinda Huawei kuanzia kukamatwa kwa Boss wa mtoto wa Huawei Canada mpaka wakamrudisha China cases zote China walisimama bako kwa bako na Huawei.

China wamepigana na wanapigana Giant huyu wa teknolojia asianguke maana yeye ni moja ya National symbol kubwa ya China kiteknolojia huwezi kutaja mafanikio ya teknojia China bila kuigusia Huawei naweza hata kuiita Huawei ni kampuni ya nchi kutokana na mchango na nafasi yake katika mafanikio na maendeleo ya China kiteknolojia.

Kinacho nishangaza ni nini ? Ni hiki anacho pitia Dangote kuhusu uwekezaji wake wa refineries nyumbani kwao Nigeria ili kutibu tatizo la mafuta lakini uwekezaji huo unageuka msiba kwake.

Hakuna wakati muhumi serikali ya Nigeria ilipaswa kuibeba kampuni ya Dangote kama kampuni ya nchi kushinda sasa.

Walipaswa kwa namna yoyote kuhakikisha Dangote group haianguki au kuangushwa na yoyote ila kwa yanayo endelea napata mashaka juu ya utimamu wa akili.
inashangaza sana, wakati wikii japo nigeria ni mzalishaji mkubwa wa mafuta ghafi kulikuwa na uhaba wa mafuta.
walikuja kwamba mafuta yake yana impurities nyingi, vipimo vikaonyesha kuwa refineries zake zina kiwango kidogo cha impurities kuliko mafuta wanayonunua nje.
yani afrika ni balaa na nadhani anajuta kuwekeza pesa nyingi kufanya hivyo.
 
Nigeria ni nafuuu.kwa hapa Tanzania magumu wanayopitia wafanyabiashara unaweza kunywa sumu.
 
Anacho fanyiwa Dangote na serikali ya Nigeria na viongozi wake ni masikitiko.

Napata mashaka juu ya utimamu wa akili zetu.

Baada ya kutokea mkombozi wa kiteknolojia [ Huawei] China serikali ya China ilisimama na Huawei na kuhakikisha kwa namna yoyote Huawei inasimama hata pale ilipopata tishio la kuangamizwa na Marekani wakomunisti wale hawakusita kuipa support ya ndani na nje Huawei isiangushwe.

Wachina walijitoa kuilinda Huawei kuanzia kukamatwa kwa Boss wa mtoto wa Huawei Canada mpaka wakamrudisha China cases zote China walisimama bako kwa bako na Huawei.

China wamepigana na wanapigana Giant huyu wa teknolojia asianguke maana yeye ni moja ya National symbol kubwa ya China kiteknolojia huwezi kutaja mafanikio ya teknojia China bila kuigusia Huawei naweza hata kuiita Huawei ni kampuni ya nchi kutokana na mchango na nafasi yake katika mafanikio na maendeleo ya China kiteknolojia.

Kinacho nishangaza ni nini ? Ni hiki anacho pitia Dangote kuhusu uwekezaji wake wa refineries nyumbani kwao Nigeria ili kutibu tatizo la mafuta lakini uwekezaji huo unageuka msiba kwake.

Hakuna wakati muhumi serikali ya Nigeria ilipaswa kuibeba kampuni ya Dangote kama kampuni ya nchi kushinda sasa.

Walipaswa kwa namna yoyote kuhakikisha Dangote group haianguki au kuangushwa na yoyote ila kwa yanayo endelea napata mashaka juu ya utimamu wa akili.
Labda mgongano wa maslahi...mbona unataka tumuonee huruma ilihali hatujui KINACHOMZUNGUKA?!!
 
Utaumiza kichwa kwa siasa za nijeria , hakuna kitu utaelewa kinachoendelea pale ..Jaribu kufuatilia wamainaijeria wenyewe ni watu wa makundi , hawawezi kusimama pamoja .

Dangote alikuwa salama chini ya Buhari nafikiria kuna picha ushapata hapo , wanaijeria wanabaguana kwa dini na majimbo(ukanda).
 
Hakika...

Wajanja wajanja...

Namshukuru Mungu nimeumbiwa Tanzania [emoji7]
 
Alafu bado Diamond Platnumz anataka kuiba na jina anajiita simba la masimba dangote
 
Wameshazama topeni...

Hawana salama tena...

Eee Allah mrehemu MWENYE HERI baba yetu wa taifa El Commandante mwalimu J.K.Nyerere ,aaamin aaamin aaaamin[emoji7][emoji7]
We acha tu, inapofikia sisi waTZ kua kitu kimoja kama nchi bila kujali dini, kabila na ukanda hapo ndipo utakapoiona taswira ya Nyerere akilini mwako. Rip JK Nyerere
 
Anachofanyiwa Dangote na serikali ya Nigeria na viongozi wake ni masikitiko. Napata mashaka juu ya utimamu wa akili zetu.

Baada ya kutokea mkombozi wa kiteknolojia [Huawei] China serikali ya China ilisimama na Huawei na kuhakikisha kwa namna yoyote Huawei inasimama hata pale ilipopata tishio la kuangamizwa na Marekani wakomunisti wale hawakusita kuipa support ya ndani na nje Huawei isiangushwe.

Wachina walijitoa kuilinda Huawei kuanzia kukamatwa kwa Boss wa mtoto wa Huawei Canada mpaka wakamrudisha China cases zote China walisimama bako kwa bako na Huawei.

China wamepigana na wanapigana Giant huyu wa teknolojia asianguke maana yeye ni moja ya National symbol kubwa ya China kiteknolojia huwezi kutaja mafanikio ya teknojia China bila kuigusia Huawei naweza hata kuiita Huawei ni kampuni ya nchi kutokana na mchango na nafasi yake katika mafanikio na maendeleo ya China kiteknolojia.

Kinacho nishangaza ni nini? Ni hiki anacho pitia Dangote kuhusu uwekezaji wake wa refineries nyumbani kwao Nigeria ili kutibu tatizo la mafuta lakini uwekezaji huo unageuka msiba kwake.

Hakuna wakati muhumi serikali ya Nigeria ilipaswa kuibeba kampuni ya Dangote kama kampuni ya nchi kushinda sasa.

Walipaswa kwa namna yoyote kuhakikisha Dangote group haianguki au kuangushwa na yoyote ila kwa yanayo endelea napata mashaka juu ya utimamu wa akili.
Huijui Nigeria bado. Kama kuna Taifa Mafia Afrika kuliko Nigeria hakuna. Ndio maana Dangote anawekeza sana nje ya Nigeria.

Dangote hawezi kupitia njia nyepesi uwekezaji wowote Nigeria bila ya kuwahakikishia asilimia fulani (ya maisha) watawala ambao ni lukuki. Ni kama vile wawe na gawiwo bila kutoa hata senti tano. Ni ngumu.
 
Anachofanyiwa Dangote na serikali ya Nigeria na viongozi wake ni masikitiko. Napata mashaka juu ya utimamu wa akili zetu.

Kinacho nishangaza ni nini? Ni hiki anacho pitia Dangote kuhusu uwekezaji wake wa refineries nyumbani kwao Nigeria ili kutibu tatizo la mafuta lakini uwekezaji huo unageuka msiba kwake.

Walipaswa kwa namna yoyote kuhakikisha Dangote group haianguki au kuangushwa na yoyote ila kwa yanayo endelea napata mashaka juu ya utimamu wa akili.
Kama alivyosema JPM, vita vya kiuchumi ni vita mbaya sana. Baadhi ya biashara fulani fulani hutawaliwa na mabeberu, ukigusa interest zao, huna maisha kabisa!, hivyo Dongote anahesabiwa tuu siku!.
Kosa la Gadafi ni kupiga jumla ya rasilimali za nchi 54 za bara la Afrika, akasema tuanzishe Bank of Afica, tuachane na WB, na IMF!. Akarusha satelite angani akashauri nchi za Africa tuachane na ITU!, kosa !, wakaamua he had to go!, wakamtafutia sababu!.

JPM alipozuia makinikia na akanzisha sheria mpya ya madini, na kuamua hakitoki kitu na kesi zote ni hapa nchini kwa sheria za Tanzania!, niliuliza humu Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts? nikaja kushauri US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali? nobody cared!, we couldn't protect him!, gone!.

Africa ndio wazalishaji wakubwa wa gold lakini hakuna gold smelter hata moja!. Japan ambayo haina hata punje moja ya dhahabu inazo gold smelter 3!. Kanchi ka Uswiss hakana hata punje moja ya dhahabu, wana gold smelter 7!.

Uganda amegundua mafuta, haruhusiwi kujenga refinery, anatakiwa kuyasafirisha yote, kisha kueundelea ku import fuel!. Mafuta hayo yanapitia Chongoleani, Tanzania haturuhusiwi kutengeneza refinery, tunalazimishwa lazima tuendelee kuagiza mafuta ya mabeberu hata kama sasa yanapatikana Uganda.

Kitendo cha Dangote kujenga refinery ni tishio kwa maslahi ya mabeberu!.
His days are numbered!.
Tukiwaambia Waafrika tumelogwa, watu hawaamini!. Umasikini wa Afrika, Je tumelogwa?. Licha ya Kuongoza kwa Utajiri, Tuna Bilionea 1 tu kwenye Top Hundred Mabilionea wa Dunia. Ni Aliko Dangote Pekee!
P

P.
 
Back
Top Bottom