Anachokifanya huyu Dada sheria inasemaje?

Anachokifanya huyu Dada sheria inasemaje?

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Wakuu salama,

Iko hivi kuna kigrosari jirani kabisa na home jioni baada ya heka heka za kutwa nzima huwa napenda kwenda hapo napiga zangu maji kidogo kisha naenda zangu kujipumzisha.

Sasa basi kwenye hicho kigrosari kuna dada mmoja mremboo kweli kweli tumetokea kuzoeana maana na yeye yupo njema kwenye kupiga maji.

Tarehe 29 siku moja baada ya uchaguzi nilikosa raha sana sasa nikiwa hapo grosari napiga zangu maji huku machozi yakinitiririka shost alivokuja akanikuta katika hali hiyo na yeye bila kuuliza nini shida nae akaanza kulia, baada ya wote kulia sana na hasira zikaisha akaniuliza " Vip best kwanini unalia" nikamuuliza Ina mana hadi sasa hujasikia habari za matokeo ya Urais na Ubunge yakitangazwa?

Tayari moja kwa moja akajua mimi Nipo mrengo gani.

Akanibembeleza sana na kuninyweshwa bia taratibu huku akisema Dawa yao ipo jikoni., hayo machozi tuliyoyamwaga hapa kuna watu watayalipia. Tulikunywa kuliko siku zote huku akiniambia kesho atanionyesha jambo.,Tukaagana vizuri kila mtu akaenda kwake.

Kesho yake kama kawaida huku nikiwa bado na huzuni nikamkuta shost yangu keshafika pale muda tu ananisubiri huku akiwa na hasira kali sana kwa hali alioniona nayo Jana, alivoniona akanipa pole tukakaa.

tulivofikisha bia ya nne kila mtu akaniambia hivi" shost yangu kuna jambo sijawahi kukuambia huku akifungua pochi yake na kutoa cheti fulani hivi na dawa, akaniambia uzuri wote huu nilio nao utaamini mimi nina ukimwi? Moyo wangu ukafanya paaah akanionyesha vyeti vyake na vidonge vya Arv anavyotumia,

Akaniambia wanaume wengi huwa wanamtongoza lakini kutokana na hali yake anaona bora awaepushe na magonjwa na huwa anawakatalia.

Akasemaa ila kuanzia leo hii kutokana na wanavyonisumbua na hivi na wewe Umekosa furaha juu ya mwelekeo wa siasa hizi sasa wataisoma namba, na wala sitaki matumizi ya mpira watajijua wenyewe huko na familia zao.

Jana jioni nikiwa nae akaniambia kuwa tangu aanze hiyo game wameshatimia wanaume 28 hadi sasa na hatoacha hadi kifo kimkute

Sasa mtu kufanya hivyo makusudi jamani hakuna sheria inayowabana watu kama hawa?
 
ungemalizia... na umeme ukakatikaaaa...kiza kikatanda
 
Wazee wa humu JF sijui wanatukana matusi gani baada ya kusoma huu uzi kama mimi tu nimetoa sonyo na tusi heavy.
 
Back
Top Bottom