Anachokosea Mbowe ni kutowaambia Wenzake kinachojadiliwa lakini ni kweli CHADEMA haina option nyingine zaidi ya Maridhiano

Anachokosea Mbowe ni kutowaambia Wenzake kinachojadiliwa lakini ni kweli CHADEMA haina option nyingine zaidi ya Maridhiano

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Angalia CCM walichofanya;

1. Wanafunzi wa vyuo karibia wote wanapewa kadi za UVCCM kwahiyo ni wanaccm

2. Machinga na Wafanyabiashara ndogo ndogo kwa asilimia zaidi ya 90 wanapaita mikopo ya vikundi kupitia Council na kigezo kimojawapo cha kudhaminika ni kadi ya CCM

3. Bodaboda Vijiwe vyote unavyovijua ni vitengo vya CCM kwenye tawi husika

4. Wakulima wamesajiliwa kupata mbolea ya Ruzuku kwa dhamana ya Serikal ya mtaa ambazo kwa 100% zinaongozwa na CCM

5. Vyama vya Wafanyakazi vyote vina uwakilishi bungeni kupitia UWT - CCM

Katika mazingira kama haya Chadema itampata wapi " mtu mjinga" wa kuandamana

Freeman Mbowe ana Pweinti kwamba Katika jambo lolote hauwezi kufanikiwa Bila ridhaa ya CCM

Na hata Mwenyekiti wa CCM mh Rais Samia amesema wazi CCM milango ya Maridhiano iko wazi ila Wapinzani wakumbuke CCM ni chama tawala kimepewa ridhaa ya Kuongoza nchi na Wananchi

Christmas njema!
 
Maelezo makini yenye kuakisi ukweli, lakini ngoja tukubeze mpaka ujichimbie chini ya ardhi, huwa hakuna hoja inayotushinda, nasema haipooo!
 
Katika maisha yangu nilishaapa kutomnenea Mtu yeyote uongo.

Kusema Mbowe hawaambii wenzake kinachojadiliwa ni kumnenea uongo na si Jambo zuri.

Mjadala Kati ya CCM, CDM na serikali unawakilishwa na timu zenye wajumbe Sawa. Kwa maana nyingine CDM inawakilishwa na timu ya majadiliano na si Mtu mmoja. Miongoni mwao zaidi ya Mbowe yumo John Myika, Heche, Mwalimu na wengine.

Kama Mbowe hawaambii wengine kinachojadiliwa, hao wengine Kwa nini wasiseme? Wiki iliyopita wote tulisikia CDM wakisema timu ya majadiliano inapeleka ripoti Kamati Kuu mwezi huu. Huu kwao ndio utaratibu wa Chama. Sasa unamlaumu Mbowe Kwa lipi?
 
Katika maisha yangu nilishaapa kutomnenea Mtu yeyote uongo.

Kusema Mbowe hawaambii wenzake kinachojadiliwa ni kumnenea uongo na si Jambo zuri...
Kwa katiba ya Chadema Mh Mbowe ndio msemaji mkuu wa chama.
 
Siasa zetu labda wazungu waingilie Kati. CCM hawapendi kabisa time huru au katiba mpya wanajua kwa level ya ugumu wa maisha na level ya umasikini wa wananchi,ikiwa kura zitakuwa halali watashindwa vibaya sana.
 
Ndio, sisi tunawakilishwa na mzee Wassira

Wanachokifanya CCM nafananisha na mwanaume anayechunwa. Unanunua mahitaji yote ya mwanamke lakini unakuta hakupenda anampenda mwanaume mwingine.

Hii ndio inayosababisha wakati wa uchaguzi CCM kutegemea zaidi wizi wa kura, maana wanajua watu hawana mapenzi ya dhati kwao.
 
Angalia CCM walichofanya;

1. Wanafunzi wa vyuo karibia wote wanapewa kadi za UVCCM kwahiyo ni wanaccm

2. Machinga na Wafanyabiashara ndogo ndogo kwa asilimia zaidi ya 90 wanapaita mikopo ya vikundi kupitia Council na kigezo kimojawapo cha kudhaminika ni kadi ya CCM

3. Bodaboda Vijiwe vyote unavyovijua ni vitengo vya CCM kwenye tawi husika

4. Wakulima wamesajiliwa kupata mbolea ya Ruzuku kwa dhamana ya Serikal ya mtaa ambazo kwa 100% zinaongozwa na CCM

5. Vyama vya Wafanyakazi vyote vina uwakilishi bungeni kupitia UWT - CCM

Katika mazingira kama haya Chadema itampata wapi " mtu mjinga" wa kuandamana

Freeman Mbowe ana Pweinti kwamba Katika jambo lolote hauwezi kufanikiwa Bila ridhaa ya CCM

Na hata Mwenyekiti wa CCM mh Rais Samia amesema wazi CCM milango ya Maridhiano iko wazi ila Wapinzani wakumbuke CCM ni chama tawala kimepewa ridhaa ya Kuongoza nchi na Wananchi

Christmas njema!
ACHA UONGO CCM INA WAJUMBE NA CHADEMA INA WAJUMBE Sio mbowe Pekee yake
 
Back
Top Bottom