Habari wana JF,
Naomba kusaidiwa kujua jibu la swali langu, ni vigezo gani vinazingatiwa wakati wa kuchapishwa pesa?
Kwa mfano Tanzania ikitaka idadi ya noti za shilingi 10,000 zichapishwe 1,000,000 ni vigezo au masharti yepi inabidi itimizwe au wanatoa tu idadi ya noti?
Au idadi ya noti za kila nchi ni sawa?
Utafiti ninavyoelewa mimi idadi ya pesa/noti sio issu kama unavyodhani! Thamani ya pesa ndio kila kitu!thamani ya pesa inawekwa na Benki kuu inayohusiana na utengenezaji wa hela!
Wanazingatia uchumi wa nchi kudetermine thamani ya hela, either uchapishaji wa noti (kufanya minoti iwe mingi) sijui wanatoa requirement gani but kwao wao sio tatizo kuchapisha minoti inayohitajika na nchi husika! Wanachozingatia wao ni ukuaji wa uchumi wa nchi!
Kwa mantiki hiyo, ningependa utambue kuengeza minoti kwa nchi sio maendeleo but ni kuifanya pesa ya nchi husika isiwe na thamani!
Kazi za kuifanya pesa iwe na thamani na kuchapisha or kubadilisha noti iko chini ya banki kuu ya Taifa husika, kwa hapa Tz ni BOT.
Kazi kubwa/kuu ya BOT ni kuhakikisha wanadhibiti mfumuko wa bei (inflation) Jee wanafanyaje kuhakikisha hilo? Hapo kunamaelelezo mengi sana, sitoweka but ukitaka nitakuwekea!
BOT kama BOT imeshindwa na jukumu hilo na ndio sababu hela ya Tanzania kila siku zikisonga hela inashuka thamani!
Na sababu kuu ya BOT kushindwa jukumu lake ni Kutokua huru na kujiendesha yenyewe! BOT ni moja kati ya wizara za serikali, ambapo head of BOT anachaguliwa na raisi na anabadilishwa kila baada ya miaka 5!
Kosa kuu la serikali ni kuiendesha BOT! Kumbuka issue ya kuengeza mishahara kwa wafanyakazi wa serikali!
Mara nyingi mishahara hupanda kutokana na mfumuko wa bei! Kitendo cha kupandisha mishahara kwa sababu ya mfumuko wa bei ni kuifanya pesa isiwe na thamani na vile vile ni kufanya maisha ya waliowengi (wasiofanya kazi serikalini) kuwa na maisha magumu
Kazi nyengine ya BOT ni kucontrol mzunguko wa pesa na kutambua kiwango/idadi ya hela iliyopo nchini!
Thus why kunapotokea wizi mkubwa wa hela or endapo watashindwa kujua idadi ya hela iliyopo nchini wanabadili noti ili kuzishika hela zilizoibiwa au kupata thamani ya hela iliyopo!
...
So kuchapishwa kwa minoti hakuna faida na badala yake ni kuifanya pesa isiwe na thamani! Thus why wale wanaotengeneza pesa hawaoni tatizo kuengeza minoti kwa nchi iliyoomba kufanyiwa hivyo!
Nadhani nimekujibu Utafiti, na uko huru kuniuliza swali!