Anaepajua wilaya ya Lushoto

Anaepajua wilaya ya Lushoto

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Nimejulishwa na mdau wangu toka Tamisemi nimepangwa huko. Naombeni mnitajie shule nzuri za Sekondari zilizo karibu na mjini na jinsi ya kufika huko. Nauli ni sh. ngapi kutokea Dar?
 
Kuna milima huko balaa, ukutoka Mombo tu unapanda bonge la muinuko na pamekaa kishamba shamba kama Sumbawanga hivi ingawa watu huwa wanapasifu
 
Kuna milima huko balaa, ukutoka Mombo tu unapanda bonge la muinuko na pamekaa kishamba shamba kama Sumbawanga hivi ingawa watu huwa wanapasifu

Mbona unantisha mkuu? baridi lipoje huko?
 
Kunajamaa alipangwa huko alikaa miezi mitatu akaamua kuacha kazi, sahiv anasubiri ajira mpya.
 
mimi napajua vizuri usiku na mchana almost kila baada ya siku tatu nakuwaga huko kufata mzigo, nenda shambalai secondary
 
Kuna milima ya kutosha na kona za Mlima Kitonga cha mtoto, baridi ipo. Ila kama kiulaya ulaya hivi, si unajua wazungu wazungu
 
Lushoto ni wilaya yenye hali nzuri sana ya hewa.Usitishike na milima.Hongera kwa kupata ajira.
 
Hahahhahahahaa nimekulia Lushoto wewe acha kuwapiga watu Sound. Lushoto ni sehemu nzuri ajabu. Nikifa nitaenda kuzikwa kule I tell.

Ukipangiwa Shambalia, Yogoi, Ubiri, Ngulwi, sijkui na waoi tena, ndio shule ambazo ziko Mjini kidogo. Ngoja kuna thread niitafute nikuwekee hapa kulivyo
 
Ni pazuri sana, andaa makoti ya baridi tu. Utakutana na Mh Mkapa huko, mnywe wishky kutoa baridi, milima kwa mtoto wa kiume haitishi.
 
Kuna milima huko balaa, ukutoka Mombo tu unapanda bonge la muinuko na pamekaa kishamba shamba kama Sumbawanga hivi ingawa watu huwa wanapasifu

Ww vp tena? Lushoto kubaya nani kakudanganya, kule sio TZ sema tu watu hawajaelimika sana ila kwa mazingira na hali ya hewa Lushoto ni pazuri mnoo. Muulizeni Mzee Mkapa alipakubail akafanya makazi yake huko.
 
Naweza kukaa popote pale. Nimezaliwa kijijini, nimesoma primary to form 2 kijijin hata mafuta ya taa kuyapata shida. Maji ya bwawa na kisima ndo yalonikuza,, umeme nimeanza kuona niilpohamia shule nyingine kidato cha 3.

Duh nakumbuka nilikesha 2 days napiga msuli just kwa mzuka wa Mwanga.. Maji ya bomba nikayakuta Advance,, tena ya magumashi kule SHY BUSH (MWADUI)... Hewalaaaa nikaangukia Morogoro chuo cha ualimu(MOTCO).

Hapa nilipaona kama Paradiso maji 24HRS, umeme wa uhakika, bwen + madarasa Gorofaa dah nilihisi nasoma masters kumbe diploma,, baada hapo nikaingia 833kj oljoro Jkt,, sikuwah kuwaza kutoroka huko pamoja na shida zote... Hadi muda huu nipo kijijini kwe2 huku mkoa wa Geita, wilaya ya Nyang'wale, kata ya kharumwa, kijiji cha Busengwa.. Nalima mchicha tu!.. KAMBI POPOTEE BANAH,,,
 
Lushoto pazuri ndgu usidanganywe, subir upangwe hyo shule then takutafta nami nkijua nmepangwa wapi.,, but Lushoto utafrahia, sema jifunze maisha ya kiulaya, full maswetaa.
 
Mdau, Lushoto ukitokea Tanga mjini, nauli ni sh 6000. Nadhan tokea Dar itakua kwenye 15 hivi kama skosei maana Dar to Tanga mjini ni elf 15...

Sasa embu nisaidie jambo moja; ulijaza mikoa gani ya kufanya kazi??? P.O.Box je ulijaza ya mkoa gani??

Nataka nifahamu ili nijue kama walizingatia machaguo pamoja na masanduku ya posta... Katika kupanga majina!!
 
Back
Top Bottom