Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hyo ni tupatupa imeanza kutisha sasa, bt labda kwa mdau wameangalia ukarbu uliopo lushoto na moro na dar na pwan so kuwekwa tanga si mbal na mikoa hyo.
Mkuu kama vipi tubadilishane mi niko kigamboni napenda kuhamia huko... Nicheki kama vipi tujue cha kufanya..
Naweza kukaa popote pale. Nimezaliwa kijijini, nimesoma primary to form 2 kijijin hata mafuta ya taa kuyapata shida. Maji ya bwawa na kisima ndo yalonikuza,, umeme nimeanza kuona niilpohamia shule nyingine kidato cha 3.
Duh nakumbuka nilikesha 2 days napiga msuli just kwa mzuka wa Mwanga.. Maji ya bomba nikayakuta Advance,, tena ya magumashi kule SHY BUSH (MWADUI)... Hewalaaaa nikaangukia Morogoro chuo cha ualimu(MOTCO).
Hapa nilipaona kama Paradiso maji 24HRS, umeme wa uhakika, bwen + madarasa Gorofaa dah nilihisi nasoma masters kumbe diploma,, baada hapo nikaingia 833kj oljoro Jkt,, sikuwah kuwaza kutoroka huko pamoja na shida zote... Hadi muda huu nipo kijijini kwe2 huku mkoa wa Geita, wilaya ya Nyang'wale, kata ya kharumwa, kijiji cha Busengwa.. Nalima mchicha tu!.. KAMBI POPOTEE BANAH,,,
Kuna milima huko balaa, ukutoka Mombo tu unapanda bonge la muinuko na pamekaa kishamba shamba kama Sumbawanga hivi ingawa watu huwa wanapasifu