Anaeweza tukafanya Partnership kwenye kilimo cha mpunga

Bakariforever

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2017
Posts
510
Reaction score
511
Mim ni mkulima nina muda wa miaka minne katika kilimo cha mpunga, mkoa wa Morogoro wilaya ya Mvomero, tarafa ya Turiani, na ndipo shamba lenyewe lilipo ukubwa wa heka nne (4) na nusu. Kwa msimu huu unaokuja nguvu imepungua hivyo nikaona nitafute mshirika tunaeweza kuweka misingi ya miongozo kama tukikubaliana ( memorundum of understanding) ili kila mmoja ajue atashiriki vipi na kufaidika vipi kwa tutaeafikiana.
Kama mwaka wa kwanza tukienda vizuri tunaweza tukaendelea hadi mpunga wa kiangazi unaoitwa ( kilimo shadidi) . Kwa msimu huu ulioanza ambao ni mpunga wa mwaka huwa tunategemea mvua ya mwaka ( masika) lakini kiangazi tunatumia kilimo cha umwagiliaji na huanza mwezi wa saba hadi 12.
Shamba la heka nne na nusu ninalolizungumzia lina rutuba ya kutosha na limekaribia na mfereji ya kampuni ya kiwanda cha sukari hivyo hata mvua zinapokuwa chache kuna uwezekano wa kuingiza maji
Katika makubaliano hayo ni lazima tuafikiane kwanza kwa kutambua mchanganuo wa gharama zote kuanzia maandalizi ya shamba hadi mavuno na usafirishaji.
Baadhi ya picha kwa misimu iliyopita naweza kuziweka na shughuli nzima za msimu uliopita kuanzia mwaka 2018 kurudi nyuma
 

Attachments

  • IMG_20180527_155004.jpg
    623.1 KB · Views: 117
  • IMG_20180514_160145.jpg
    340.6 KB · Views: 111
  • IMG_20171225_095535.jpg
    413.6 KB · Views: 120
  • IMG_20180216_155739.jpg
    478.2 KB · Views: 119
Heka NNE kiongozi n chache sana kaka! Hapo ungekuwa Na zaidi hata ya heka 30-50 ingefaa boss! Jua kuwa unafanyakaz kwa lengo LA kibiashara! Hivyo ongeza eneo chief
 
Heka moj huwa unapata magunia mangapi kwa heka moj? Na unapanda mbegu gani huko
 
Heka NNE kiongozi n chache sana kaka! Hapo ungekuwa Na zaidi hata ya heka 30-50 ingefaa boss! Jua kuwa unafanyakaz kwa lengo LA kibiashara! Hivyo ongeza eneo chief
Ok shukrani kwa ushauri kiongozi
 
wazo zuri sana. mpambanaji lkn umeishia njiani. haitoi. picha ya ulicholenga. mimi kama msomaji sikati kiu kwamba nitashiriki vipi/hatua gani. nakadiria tu kuwa nitahusika kifedha kudhamini kodi, vibarua, trekta la kulima, mbegu, dawa, mifugo n. k lkn angalau ungetoa uchanganuzi wa hekari moja ili mtu ajipime muanze na hekari ngapi.

pia waliohoji udogo wa eneo pia ni vema, sipishani sana na mawazo yao lkn ifahamike tunatofautina mtaji. ma ninavyoelewa wajuzi wa kilimo na hususani mnaokaa huko mashambani mkiamua kukodi hata hekari 200 zitapatikana.

tusaidie kwa hili kwanza la gharama za hekari moja. mengine tutajiongeza.
 
Kwa uzoefu Wangu heka moj maeneo ya Bahi-dodoma ni kama ifuatavyo!

Kukodi 1@150000tsh
Kulima kwa trekta @1@55000-70000tsh
Kumwaga mbegu kwenye vitalu 1debe (20kg)@5000tsh
Kupandikiza miche 1@70000tsh
Kuvuna Na kupaki kwenye magunia (1 gunia @4000tsh) inategemea umepata magunia mangapi!

Gharama zote ni za wakati huu, sio za mwaka Jana wapendwa!

Sijajua kwa huko Morogoro ,maana nasikia huwa wanamwaga mbegu shambani, tofauti Na hapa lazima upande ili uweze kupata mazao mengi!
NB: heka moj unaweza kupata magunia 25-35 inategemea Na aina ya mbegu Na utunzaji wa shamba lako!
 
Aisee!! Nilikuwa natafuta connection na mtu wa Bahi. Nataka kulima mpunga Bahi. Tafadhali, naomba mawasiliano yako bro pm
 
OI UNATUMIA JINA GANI INSTAGRAM
 
Mkuu na0mba mawasiliano yak0!
 
mkuu ukifanikiwa karibu tunazo mashine manual na automatic za kupandia mpunga kwa mda mfupi sana kwa ratio ya eneo kubwa karibu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWa kilimo cha muda wa miaka minne na shamba unalo heka nne na unahitaji partnership
Hapana mkuu nadhani hapo utauwa unacheza karata garasa
Pambana wewe mwenyewe tu
kachukue hata mkopo weka shamba lako lehani nadhani itakuwa vizuri zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…