Bakariforever
JF-Expert Member
- Aug 30, 2017
- 510
- 511
Mim ni mkulima nina muda wa miaka minne katika kilimo cha mpunga, mkoa wa Morogoro wilaya ya Mvomero, tarafa ya Turiani, na ndipo shamba lenyewe lilipo ukubwa wa heka nne (4) na nusu. Kwa msimu huu unaokuja nguvu imepungua hivyo nikaona nitafute mshirika tunaeweza kuweka misingi ya miongozo kama tukikubaliana ( memorundum of understanding) ili kila mmoja ajue atashiriki vipi na kufaidika vipi kwa tutaeafikiana.
Kama mwaka wa kwanza tukienda vizuri tunaweza tukaendelea hadi mpunga wa kiangazi unaoitwa ( kilimo shadidi) . Kwa msimu huu ulioanza ambao ni mpunga wa mwaka huwa tunategemea mvua ya mwaka ( masika) lakini kiangazi tunatumia kilimo cha umwagiliaji na huanza mwezi wa saba hadi 12.
Shamba la heka nne na nusu ninalolizungumzia lina rutuba ya kutosha na limekaribia na mfereji ya kampuni ya kiwanda cha sukari hivyo hata mvua zinapokuwa chache kuna uwezekano wa kuingiza maji
Katika makubaliano hayo ni lazima tuafikiane kwanza kwa kutambua mchanganuo wa gharama zote kuanzia maandalizi ya shamba hadi mavuno na usafirishaji.
Baadhi ya picha kwa misimu iliyopita naweza kuziweka na shughuli nzima za msimu uliopita kuanzia mwaka 2018 kurudi nyuma