Anahitaji msaada wa kisaikolojia

Anahitaji msaada wa kisaikolojia

Wakuu naombeni mnipe mawazo ya kiushauri niweze kumshauri huyu ndugu yangu, Nahisi hayupo sawa kisaikolojia.

Ni mtoto wa mjomba wangu alimaliza diploma ya clinical officer mwaka 2020 akiwa na G.P.A ya 3.1, Kwa wakati wote tokea amalize hakuwahi bahatika kupata ajira ya kudumu zaidi ya kazi za vijiwe ambapo walikuwa wakimlipa kati ya laki mbili hadi laki mbili na nusu.

Sasa tokea amalize alikuwa ana lengo la kujiendeleza kielimu ila kwa jinsi ushindani ulivo mara zote alizoomba maombi hakuwahi pata chuo ili asome M.D

Sasa juzi kwenye kikao cha ukoo kijana amekuja na idea iliyotuchanganya ndugu hata tukahisi labda ameanza kuvuta bangi mbichi.

Anasema aliapply diploma kwenye kozi ya mionzi chuo kimoja cha dini na anataka akasome hivi karibuni , Wana ndugu tumemshangaa sana yaani anataka awe na diploma mbili tofauti.Kiukweli sisi kama ndugu tumemkatalia hilo suala maana tunaona anapoteza muda, Yeye anadai hiyo kozi ndio habari ya mjini kuliko hii diploma yake ya C.O

Kama ndugu tumemshauri sana hatusikilizi anang'ang'ania lakini tunahisi hayupo sawa kisaikolojia,Nahitaji msaada wa ushauri wenu au kama kuna mtu ni mwanasaikolojia naombeni mniunganishe nae aweze kumshauri huyu dogo.
Dogo yuko sawa ila tatizo ndugu hamkumuelewa, na labda ni kwa sababu hamna uelewa wala exposure katika soko la ajira la Afya.

Dogo ana Hoja msikilizeni
 
Sitaki kuamini kwamba ukoo mzima hamna uelewa wa mambo kasoro yeye peke yake!
Sio hivo ndugu hata hiyo C.O sisi ndio tulimshauri asome, hii ya mionzi imetushangaza sana ukizingatia hatujui hata inahusiana nini tukahisi kijana ana msongo wa mawazo wa kukosa ajira
 
Ndio kukosa uelewa kwenyewe huko, eti kwasababu nyie hamjui mnafikiri na yeye hajui.
 
Wakuu naombeni mnipe mawazo ya kiushauri niweze kumshauri huyu ndugu yangu, Nahisi hayupo sawa kisaikolojia.

Ni mtoto wa mjomba wangu alimaliza diploma ya clinical officer mwaka 2020 akiwa na G.P.A ya 3.1, Kwa wakati wote tokea amalize hakuwahi bahatika kupata ajira ya kudumu zaidi ya kazi za vijiwe ambapo walikuwa wakimlipa kati ya laki mbili hadi laki mbili na nusu.

Sasa tokea amalize alikuwa ana lengo la kujiendeleza kielimu ila kwa jinsi ushindani ulivo mara zote alizoomba maombi hakuwahi pata chuo ili asome M.D

Sasa juzi kwenye kikao cha ukoo kijana amekuja na idea iliyotuchanganya ndugu hata tukahisi labda ameanza kuvuta bangi mbichi.

Anasema aliapply diploma kwenye kozi ya mionzi chuo kimoja cha dini na anataka akasome hivi karibuni , Wana ndugu tumemshangaa sana yaani anataka awe na diploma mbili tofauti.Kiukweli sisi kama ndugu tumemkatalia hilo suala maana tunaona anapoteza muda, Yeye anadai hiyo kozi ndio habari ya mjini kuliko hii diploma yake ya C.O

Kama ndugu tumemshauri sana hatusikilizi anang'ang'ania lakini tunahisi hayupo sawa kisaikolojia,Nahitaji msaada wa ushauri wenu au kama kuna mtu ni mwanasaikolojia naombeni mniunganishe nae aweze kumshauri huyu dogo.
Mbona kama nyie ndo mnavuta bangi badala yake mkuu 🤣🤣 mtoto yuko sahihi kupambania maisha yake anapoona kuna upenyo !!
Kama mnamkatalia basi ongeeni nae awaeleze ni kitu gani anatamani kukifanya ili atimize ndoto zake iwe biashara , elimu n.k ! Halafu changishaneni mmwekeeni mazingira apambane !
 
Asante sana mkuu kwa mchango wako nimekuelewa
 
Back
Top Bottom