Nimehangaika sana kutafuta mke na hiyo ilikua sababu kubwa kuniingiza humu ndani baada ya kushindwa kumpata mwanamke wa kuishi nami huko nje.nimetumia several gears kujaribu kuattract warembo wanaohitaji mume mwenye upendo wa dhati kama mimi to no avail.
Baada ya attempt zangu kugonga mwamba nikakumbuka natakiwa kupiga magoti kumuomba Mungu anipe mwanamke wa kuishi nae for the rest of my life.Wiki ilipoisha tangu nianze maombi hayo na hatimaye Mungu kajibu maombi yangu.
Ilikua kama ndoto,nilipotoka kanisani niliamua nijipumzikie maeneo ya kwa Kakobe kuna sehemu inaitwa kwa mama Kamche.Nilipoketi kwenye viti vilivyo pembezoni mwa barabara ya Samnujoma huku nikimtafakari aina ya mwanamke nitakayempata toka kwa Mungu (kwa imani niliamini yeyote ntakayempata atatoka kwa Mungu)
Mara nikaona gari aina ya platz new model inapiga indicator kama inakuja karibu na nilipoketi. Gari hilo nililikua likiendeshwa na mrembo akionekana na yeye alitokea kanisani nakuja kukaa meza moja na mimi. Akanisalimia with a broad smile na sauti yake nyororo. Moyo wangu ghafla ukawa na amani tele kana kwamba bila hata ya kuongea chochote moyoni nikajua Mungu amejibu maombi yangu.
Kwakua nilikua nakunywa soda aina ya fanta nikaamua kumuuliza anakunywa kinywaji gani bila hesitation akajibu kama ya kwangu. Tukaulizana maswali ya kawaida kwa watu wanaokutana kwa mara ya kwanza na response yake ikawa kana kwamba Mungu aliamua tukutane tulivyokutana. Hii ilijihidhirishisha pale nilipoamua kujitoa muhanga kumuuliza kama amekuja pale kumsubili mwenza wake,jibu nililopata likaniongezea imani kwamba yeye ndo mke ninae muhitaji maishani. Alijibu "Mungu ajanipa wangu labda kwanzia sasa".
Baada yasikia hiyo sentence nikaamua nianze kujiongeza kama mwanaume.Nikafunguka ipasavyo kama mwanaume na kujionyesha kuwa mimi ndo mwanaume anayestahiri kuwa naye. Mda ulipozidi kwenda tukabadilishana namba kwa ajili ya mawasiliano na kwakua na yeye alikuja pale kwa mapumziko akasema anaondoka nakuniuliza kama ntapenda kupata lift kwakua wote tunaelekea maeneo ya mbezi beach.
Tulipokua tu narudi nikaanza kujiskia usingizi mzito na baadaye nikaskia vibration ikiambatana na wimbo nibebe nibembeleze nibebe. Nikashka kumbe nilikua naota.