sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Habarini wadau, Nina rafiki yangu ambae bahati ipo upande wake maana kiukweli linapokuja kwenye swala la uchumi wapo vizuri sana.
Familia yao kiufupi wapo vizuri, kaka na dada zake wanajitegemea na wapo vizuri kiuchumi ila sasa huyu rafiki yangu kwa bahati mbaya shule ilimshinda na biashara kwake ni ngumu, kiufupi ni mtu wa nyumbani ila wazazi wake wanajali, ana gari na pesa anapewa, hana fujo na ni muungwana tu.
Mwezi wa pili walipata msiba mama yao alifariki, sasa amebaki mzee peke yake nae kiufupi maisha yamekuwa magumu baada ya kuondokewa na mkewe, Mzee wao ni mtu msomi akaamua tu aanze kuweka mambo sawa mapema, kuanzia mwezi wa sita alianza kuwapa ramani watoto wake wa kila mali aliyonayo, pamoja na kushughulikia mambo ya mirathi, kuna baadhi ya mali ifikapo mwezi
zitaenda kwa watoto wake hata kama bado yupi hai, na hizi ndizo nazozizungumzia hapa.
Sasa huyu rafiki atachopata ni takribani milioni 320, hizi ni anazipata miezi michache ijayo, mzee wake ndio kaamua kumpa kiasi hicho kama urithi wake wa mwisho kwake, akifeli ni game over.
Kabla sijampa ushauri nilimwambia yeyea anafikiria kuwekeza wapi akaniambia kafikiria mawazo kama kufungua bar kubwa, kujenga sehemu ya kuogelea, kununua bajaji nyingi, nk ni mawazo mazuri lakini nikamwambia yanahitaji mtu awe ana uzoefu kidogo wa biashara.
Sasa binafsi nimemshauri kwavile hajui biashara na hana elimu ni vema akanunue treasury bonds,
Ila na mimi nimempa taarifa juu juu tu, naombeni taarifa za ziada kuhusu hatua za kununua bondi hapa nchini, katika hio milioni 320 je aweke kiasi gani , mambo gani ya kuzingatia, kutambua matapeli, n.k
Na pia kama kuna wazo mbadala itakua vizuri ukiliweka ila sio linalohitaji sana skills za biashara ambazo rafiki yangu huyu kwake ni changamoto