Anakaribia kurithi 300M, hajui biashara ya kufanya, je, ushauri niliompa ni sawa?

Anakaribia kurithi 300M, hajui biashara ya kufanya, je, ushauri niliompa ni sawa?

Aweke 200m treasury bonds za Serikali kwani Serikali haifilisiki labda mabwege Ugiriki walibugi mahali,kwani kwa mwezi hakosi kama kamshahara vile cha takribani 1.7m,iliyobaki anunue hizi bajaj zote,haina shida,ila usimamizi wa karibu ni muhimu
 
Kama ana nyumba na gari atulie aweke benki awe anajilipa 1•5m kwa mwezi maisha yanaenda kama hana nyumba ajenge anunue gari inayobaki awe anajilipa monthly, kama anataka cha kumkeep busy afungue banda la kuonesha mpira limchangamshe
 
Mkuu nachofahamu kwa Treasury bills ambazo ni za muda mfupi, atachagua kulipwa baada ya siku ngapi zinakuwa au 35,91,182,364. Mfano hapo chini angeweka milioni 200 (kwa bei ya mnada uliopita) atakachopata kimeainishwa hapo kwenye (Net gain)

Kama ni Treasury Bonds ambazo ni kwa muda mrefu, kama angeweka milioni 200 ((kwa bei ya mnada uliopita) kiasi atakachopata kimeainishwa hapo kwenye (Total Gain)
Ndio nimejua leo wana kikokotoo na nimetoka kukitumia muda si mrefu.

nmeingia kwenye kikokotoo cha BOT, faida ya kuweka mzigo wa milioni 300 si kitoto

ukiweka kwa miaka 10, kila mwaka unapewa 34,647,558.01 (Yearly Coupon) kwa miaka 10 mfululizo.

baada ya miaka 10 utakuwa umelipwa jumla ya 349,338,849 (Total Gain) na unaenda kuuchukua mzigo wako uliowekeza sio kwa hela ile ile uliyoweka miaka 10 iliyopita, wata rekebisha kidogo angalau mzigo uongezeke thamani, utapewa 302,863,269.35 (Amount at Maturity)


1627410227196.png


kikokotoo >> Bank of Tanzania
 
Kuna biashara nyingi zisizohitaji pressure na uwekezaji mkubwa ... Akiwekeza 50M tu ndani ya mwaka ana 50 nyingine.. Ni biashara ya kukusanya malighafi fulani na soko lake ni hakika
Na mimi nitakutafuta mtani wangu
 
Akiwa anafikiria kitu cha kufanya, aangalie benki nzuri afungue"fixed account" kila mwezi ana uhakika wa kupata pesa nzuri.
 
Ndio tujuzane mkuu, kumbuka huyu rafiki hajui sana mambo ya biashara, yeye labda nlichoona kitamfaa ni kuweka hela na kusubiri mapato ya uhakika ndio nikamshauri hizo bondi maana hazina mambo mengi, nlitaka kumshauri kufungua gym ila bado nikaona huki anaweza kufeli

Ika mkuu tueleezane hio biashara
Taja basi mkuu inaweza kuwa ni fursa kwa wengine pia.
Ni biashara mpya kabisa halali ngoja niipange vema tutashirikishana hata kwa PM
 
Kuna biashara nyingi zisizohitaji pressure na uwekezaji mkubwa ... Akiwekeza 50M tu ndani ya mwaka ana 50 nyingine.. Ni biashara ya kukusanya malighafi fulani na soko lake ni hakika
Duh shiling inazaa shiling mbona hiyo biashara nzuri
 
Tuingie nae mkataba kila mwezi namlipa 10 mln na baada ya miaka miwili na nusu namrejeshea pesa yake 300m
 
Akanunue bonds za serikali Kuna mnada mwezi October, Tena anunue ile ya miaka 25 ya interest rate kwa 15.94%

Aweke milion 200 tu atulize kichwa

200,000,000 x 15.94/100 = 31,000,000 Tsh kwa mwaka.

Utakuwa unapewa milion 31 kwa miaka 25. Na baada ya miaka 25 utarudishiwa Principal yako ya milion 200,000,000.

Nimekupata huu ushauri kwasababu anahitaji biashara yenye low risks kams hii.
 
30 milion appartment za vyumba viwili na choo ndani sebule pia.
30 milioni nyingine aje kkoo.. afungue duka la nguo. Hapa unatunza mtaji unawekeza faida. Akitulia… anakua bosi kabisa.
NASEMAJE HELA NYINGINE INAYOBAKI AWEKE TU BANK. mpaka apate kitu cha ujuzi.
 
Akanunue bonds za serikali Kuna mnada mwezi October, Tena anunue ile ya miaka 25 ya interest rate kwa 15.94%

Aweke milion 200 tu atulize kichwa

200,000,000 x 15.94/100 = 31,000,000 Tsh kwa mwaka.

Utakuwa unapewa milion 31 kwa miaka 25. Na baada ya miaka 25 utarudishiwa Principal yako ya milion 200,000,000.

Nimekupata huu ushauri kwasababu anahitaji biashara yenye low risks kams hii.

Exactly
 
Wasikuambie habari nyingine. Hilo wazo la kununua hisa,hasa NMB bank nenda kawaone haraka. Ili hiyo pesa isiingie kwenye mzunguko usio rafiki kwa mtu asiejua biashara,bora mara mia kuweka bond. Uzuri wake baadae mkifikiria biashara nzuri yenye mnaweza mkaachana na bond mkataba ukiisha. Ila kwa sasa hiyo ya bond ni the best
 
Back
Top Bottom