Hilo la kusafiri na kupeana likizo la muda linaweza kuwa sehemu ya ufumbuzi, lakini kutowacha matumizi..... tukumbuke kuwa wana mtoto. Si haki kwa huyu mtoto kuteseka kwa sababu ya migogoro ya wazazi wake.
:focus:Tatizo huyu jamaa laini sana, hawezi hata kukaa na kuzungumza na mkewake? Kama tu tungelikuwa na utamaduni wa kuongea matatizo yetu, "pros and contra", tungefika wakati tunachukua misimamo ya kati na kufikia maelewanao. Inavyoonesha huyu jamaa hawezi kufanya lolote, kwa hiyo hata kama ataenda kwa wazazi, washenga, atapata ushauri wa marafiki na wataalamu... ikiwa hatajinasua na mtindio wake wa maamuzi, hakuna litakalobadilika. Ni juu yake kushika hatamu.