Anakohoa hasa ikifika jioni,Masada ndugu

Anakohoa hasa ikifika jioni,Masada ndugu

Jambo Tz

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
670
Reaction score
203
Ndugu zangu naomba msaada wenu wa kimawazo na tiba mke Wangu anaujauzito Wa miezi mitatu kila ikifika joini anapatwa na kikohozi cha ajabu muda Wa dk 35-45 na baada ya hapo anapata ahueni na kupona Kabuisa.

Ametumia dawa kadhaa bila ya mafanikio natumai kupitia Jf kwa uwezo wake Muumba atapatikana mtaalam Wa kunipa maelezo murua yatalayo msaidia wife
 
Sina nia mbaya lkn godoro lako kama ni la sponge lina zaidi ya miaka miwili ? au jumbani iko karibu nza barabara ? mchana anashinda hapo hom au kwa ofic
 
Hakikisha anaweka kakipande cha Tangawizi iliyomenywa maganda mdomoni.asitafune bali awe anameza mate tu.Afanye hivyo ikikaribia ule muda kikohozi kinapo anza.Anaweza akalala nayo ikiwa mdomoni.Hiyo inasaidia sana
 
Atakuwa ana allergy ya kitu kwa mfano sabuni ya unga mnayotumia kufulia shuka. Kwanza hakikisha hilo suza nguo zote kwa maji bila sabuni halafu uone. Poleni
 
Hakikisha anaweka kakipande cha Tangawizi iliyomenywa maganda mdomoni.asitafune bali awe anameza mate tu.Afanye hivyo ikikaribia ule muda kikohozi kinapo anza.Anaweza akalala nayo ikiwa mdomoni.Hiyo inasaidia sana

Mkuu we UNATAKA KUUA!!

USITHUBUTU kumwambia mtu ALALE NA KITU CHOCHOTE MDOMONI. NI HATARI SANA.!

Wakati mtu kapitiwa usingizi ANAWEZA KUPALIWA NA KITU CHOCHOTE KILICHOMO MDOMONI.

wakati wa kulala usithubutu kuweka chochote mdomoni.!
 
Nyumba ndogo yako inamjua mkeo ? Au kuna siku nyumba ndogo imekuja hapo hom kulala au hata kutembea waqt mkeo hayupo ?Nyumba ndogo yako ni mtu wa wapi. Mchunguze sana nyumba ndogo na kipindi hiki cha ujauzito usipende sana kuspend time na huyo kicheche nyumba ndogo. au home wreacker
 
Kila siku nikifungua ukurasa wa kwanza wa tovuti hii habari ni zilezile hakuna mpya!.

Je, huyo mzee wetu Simba alikuwa akitufunga kamba?

Naungana na wewe. Kwani hata mm nilisumbuka sana na chanzo kilobainika ni minyoo
 
Nyumba ndogo yako inamjua mkeo ? Au kuna siku nyumba ndogo imekuja hapo hom kulala au hata kutembea waqt mkeo hayupo ?Nyumba ndogo yako ni mtu wa wapi. Mchunguze sana nyumba ndogo na kipindi hiki cha ujauzito usipende sana kuspend time na huyo kicheche nyumba ndogo. au home wreacker

Unamaanisha kamati ya ufundi imehusika?
 
Nyumba inatakiwa kuwa safi namaanisha iwe inafutwa mavumbi na kudeki. Pia kipimo kinahitajika aende akamuone docta for check up
 
Unamaanisha kamati ya ufundi imehusika?

Haya mambo yalikuwepo toka enzi za mababu. Kama huamini mambo ya kamati ya ufundi uliza mwanamke mjamzito tena tafuta msomi kabisa au aliyekulia Mwananyamala. tandika au temeke hata Vingunguti ukimpata
 
ndiomaana naipenda Jf kwa kuwa kituo kizuri cha kupeana mbili tatu,ila kuna watu hawako siriaz na mambo ya watu
 
Inategemea na maeneo uliyopo,sasa sifahamu kama upo maeneo yenye hali ya hewa ya baridi! au maeneo ya hali ya hewa joto! mara nyingi ifikapo jioni jua huwa limeshazama na kinaanza kibaridi kiasi fulani, kwahiyo kubadilika kwa heli ya hewa inaweza changia kwa yeye kusumbuliwa na kikohozi.

Swali, Mkeo hatumii udongo? Si unajua hawa wenzetu wakiwa kwenye hali ya ujauzito huwa wanamumunya udongo/michanga.
Hiyo nayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusababisha kikohozi
 
Hii inaweza kusababishwa na ujauzito, maana baadhi ya wanawake wakiwa wajawazito hutokea baadhi ya magonjwa ya ajabu ajabu.. Cha kufanya ni kumuona DK wa wanawake au mkunga watakupa ushauri wa maana.
 
Pole sana ndugu yetu
mm ushauri wangu, kwa wakati huu wa Ujauzito hebu ajaribu kuhama au kutembelea Ndugu zenu wa Mji mwingine
  • Kama kitatulia ndio ung'amue kuwa ni Eneo manaloishi huenda jioni kuna moshi wa vitu vinavyochomwa (takataka) Chips (kwa mafuta ya transfomer) mavumbi ya magari hapo kwenu arudipo kazini
  • pia Kamati ya ufundi km walivyosema wengine ni hao majirani na small house
  • IKIZIDI UONE DR
 
ushauri uende Hospitali ukamuona DR sababu ziko nyingi mno zinazoweza kusababisha hali hiyo.:smow:
 
Back
Top Bottom