Mwanaume wa kweli haulizi maswali mengi,swali ulilouliza linatosha kabisa,muulize mara ya mwisho shida ni nini? Akiendelea kukaa kimya au kutoa majibu ya kipuuzi nenda next step....
......ambayo ni usimuulize tena, mwanaume habishani na mwanamke,fanya mambo yako kama kawaida usivuruge ratiba yako kwa namna yoyote, ondoka nyumbani kama unavyotoka siku zote rudi kama ratiba yako ya siku zote,kama kuna maagizo yoyote mpe,kwa kifupi wewe jitahidi kwa namna yoyote kujifanya kama hakuna kinachoendelea.
Labda kama hajapika,kula njiani usilale njaa sababu ya mwanamke,usimgombeze utaonyesha udhaifu,fanya mambo yako mwenyewe,amka nenda kazini,akipika kula usisuse, asipopika pia sawa,nakuahidi hapitishi siku tatu atakuambia shida ni nini.
Usibishane na mwanamke akiwa kwenye hali kama hiyo,we muache ahangaike mwenyewe,tafuta siku yako ambayo unaona amekuwa vizuri kisirani kimeisha,ongea naye yale unayoyataka kumwambia kwa upole kabisa.
Wanawake wanatabia ya kutaka kucheza na akili za wanaume,we fanya vyovyote asicheze na akili yako,hata kama inakuumiza jikaze usimuonyeshe hata kidogo,mana hilo ndo lengo lake.