Ananiingiza hasara duka langu!!, anatia huruma usoni, sina ujasiri wa kumfukuza, nipeni mbinu kumfukuza!!!

Sasa nifanye nini mkuu, ujue kitu unachodhani kwako ni rahisi usifikiri ni rahisi kwa kilamtu
Kulingana na maelezo yako mimi nadhana huyo mfanyakazi wako siyo mwizi ila kuna mawili. 1. Hajui mahesabu vizuri 2. Kuna mtu huwa anamwibia yeye bila kujua. Hili la mahesabu ni rahisi sana kugundua kwani unaweza kufanya zoezi la wewe kujifanya ni mteja unanunua item A na kumpa kiasi fulani na kuona anarudisha kiasi gani.

Fanya zoezi kwa Item moja na nyingi ili uone uwezo wake wa mahesabu. Siku hizi watoto wengi wanamaliza hata form four na six lakini mahesabu ya kutoa na kujumlisha hawawezi... na mbaya zaidi hata kwa kutumia calculator. Hiyo namba 2 ndiyo possibility kubwa i.e.

kuibiwa. Unapofungua biashara yoyote ni lazima kuna wezi wako pembeni wanakuangalia na kusoma ramani, japo wewe huwaoni. Pengine wameshamjulia na unapokuwa hauko wanakuja na kumchanganya kwa kujifanya kununua na kuuliza uliza bei za vitu halafu wanaiba.

Wakati mwingine kuna wateja nao ni wezi wanakuja kununua vitu na hapohapo wanaiba. Au yeye ni mzembe na huwa anaondoka eg kujisaidia na kuomba mtu amwangalizie dukani na huyo aliyeaminiwa anaiba.
 
Nakazia
 
Ww mwambie kuna mambo yameingiliana biashara unafunga kwa muda aende ukimuhitaji utampigia simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hizo hela za mtaji uliokota ama?
Mtu ana kutia hasara halafu unamchekea? Endelea tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo wako alikuwa mvivu kwa maksudi, Huyu Wangu ni mchana kazi na sijataka kumhukukumu kwa nataka kumbe ikawa mtoto wa watu anaibiwa na wezi wenye ujuzi, inabidi nifatilie kwa kina hiki kitu
 
Kwa sasa nlichoamua nikemsamehe huenda labda kuna matatizo ambayo ntamsaidia kurekebisha, uamuzi nliochukua nafunga kesho CCTV camera inayorekodi kila kitu nipeleleze nini tatizo
 
Nimeamua nifunge CCTV kesho, kama kuna wezi wanafanya nimuone Huyu Binti mwizi hakika watakipata, ila kama ni yeye mwizi itajulikana tu....asante kwa ushauri ntaanza kumfanyia majaribio namtuma mtu anunue bidhaa flani alafu jioni kwa maksudi nairudisha namwambia anioneshe alipouza
 
Unakwama wap ww bosi unamuoea huruma ya Nini wakati mwizi piga chini ukizubaa a utapigwa mbaka ulie
 
Unakwama wap ww bosi unamuoea huruma ya Nini wakati mwizi piga chini ukizubaa a utapigwa mbaka ulie
Sitaki kuhukumu mapema, kesho naweka CCTV inarekodi kila kitu Mimi kazi yangu kupitia tu, kuna mmama amenishauri hiki kitu naye alidhani anaibiwa na muuzaji wake kumbe CCTV iliwanasa wezi ambao walikuwa ni wauzaji wa duka jirani.
 
Kwa sasa nlichoamua nikemsamehe huenda labda kuna matatizo ambayo ntamsaidia kurekebisha, uamuzi nliochukua nafunga kesho CCTV camera inayorekodi kila kitu nipeleleze nini tatizo
kila la kheri but cctv sio suluhisho,trust me...kaa nae dukani uone nini haswa kinatolea
 
Fukuza huyo.
Naamini binadamu tumepewa akili ya kutohukumu MTU kwa haraka sana, kizazi hiki cha teknolojia nimejiona na Mimi nlikuwa mzembe kutokuweka CCTV ,

Yawezekana ni binti mwenyewe anaiba maksudi au ni Bahati mbaya bila hiari ama kuna wezi wanamlaga timing mfano akienda chooni,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…