Ananiingiza hasara duka langu!!, anatia huruma usoni, sina ujasiri wa kumfukuza, nipeni mbinu kumfukuza!!!

Ananiingiza hasara duka langu!!, anatia huruma usoni, sina ujasiri wa kumfukuza, nipeni mbinu kumfukuza!!!

kila la kheri but cctv sio suluhisho,trust me...kaa nae dukani uone nini haswa kinatolea
Kwangu hio likizo ya wiki siwezi ukipata kwa sasa, naamini CCTV ndio itasaidia maana kila mzigo utaouzwa ntauona na idadi pia ntajua ni kiasi kipi kinatakiwa niwe kimelipwa, ila muhimu zaidi ni kwamba hili eneo kuna wezi kwahio kwa namna moja au nyingine nahisi kuna wezi na kama wapo na CCTV ikawarekodi basi wajiandae na maisha ya gerezani
 
Sitaki kuhukumu mapema, kesho naweka CCTV inarekodi kila kitu Mimi kazi yangu kupitia tu, kuna mmama amenishauri hiki kitu naye alidhani anaibiwa na muuzaji wake kumbe CCTV iliwanasa wezi ambao walikuwa ni wauzaji wa duka jirani.
Ukiweka kamera itakusaidia sana. Ziweke vizuri zichukuwe pich angles zote na ikiwezekena nyingine zifichwe ili zisionekane. Unapofungua biashara mpya haikosi wezi kunyemelea. Kuna mama mmoja alikuwa anaibiwa wenye maduka ya nguo mpaka waje kumgundua ilichukuwa muda mrefu. Kwanza alikuwa anajifanya anatembeza nguo za jumla kuuza. Na alikuwa na nguo kweli anatembeza ila siyo nyingi, inaweza kuwa shati dazani moja nk. Halafu alikuwa anauza bei nzuri sana. Akifika dukani anakuchangamkia na kukuonyesha mali aliyonayo na bei ni yake ni rafiki sana. Ile unafurahi kuwa umepata mali ya nzuri anakuchanganya na kukwapua mali kutoka kwako. Anakuwa amevaa baibui kwa hiyo anaiweka ndani. Ile yake anakuuzia kwa bei nzuri na yeye anaondoka na mali aliyoiba.
 
Ukiendekeza huruma kwenye biashara lazima ufilisike haraka sana

Biashara inahitaji mtu katili Ila Muungwana

Biashara inahitaji ujue kucheza na fitina za sokoni

Biashara inahitaji unjanja wa kuona fursa

Biashara inahitaji watu jasiri sio waoga na goigoi .

Biashara inahitaji commitment nankujitoa sio kufanya imradi tu na wewe una biashara

Mchomoe chap!!

Utakuja jikubali baadae ukifanya maamuzi hayo Sasa .

Huyo anapiga hela hapo dukani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu nmeponea chupuchupu
Kuswekwa stakshar na mtoto wa shangaz
Kisa mambo haya ya kuajiriwa dukan
Nlikoma kabsa na hyo kaz

stidy
 
Kwangu hio likizo ya wiki siwezi ukipata kwa sasa, naamini CCTV ndio itasaidia maana kila mzigo utaouzwa ntauona na idadi pia ntajua ni kiasi kipi kinatakiwa niwe kimelipwa, ila muhimu zaidi ni kwamba hili eneo kuna wezi kwahio kwa namna moja au nyingine nahisi kuna wezi na kama wapo na CCTV ikawarekodi basi wajiandae na maisha ya gerezani
hahaaah mkuu mbona unachimba mkwara utafikiri wezi wenyewe wapo humu
 
Kwangu hio likizo ya wiki siwezi ukipata kwa sasa, naamini CCTV ndio itasaidia maana kila mzigo utaouzwa ntauona na idadi pia ntajua ni kiasi kipi kinatakiwa niwe kimelipwa, ila muhimu zaidi ni kwamba hili eneo kuna wezi kwahio kwa namna moja au nyingine nahisi kuna wezi na kama wapo na CCTV ikawarekodi basi wajiandae na maisha ya gerezani

Kipindi unafunga CCTV camera hakikisha hakuna watu wanaojua unafunga nini ata mfanyakazi wako asijue ikibidi mpe mapumziko ya siku moja ufanye ili jambo lako

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Asikwambie mtu nlikuwa nadhani kufukuza mtu kazi kitu simpo, nshawahi kushuhudia jamaa yangu aliifata bodaboda yake stendi akamnyanganya funguo kijana anaeiendesha mbele ya umati mkubwa nidhani rahisi, Pia nliwahi kushuhudia mjomba wangu alimfukuza kijana aliekuwa akimsaidia kuuza duka, alimfukuwa wazi wazi bila kujali kijana ataenda wapi, nikadhani rahisi.

Nikiri tu maishani sijawahi kumfukuza mtu kwasababu hii ndio biasharara yangu mpya nliyofungua baada ya kushawishika niwe na vimiradi ukiachana na kazi yangu katika shirika la serikalini,

Nimefungua kamradi ka oili za magari zile oili za sevisi na vifaa muhimu vya sevisi n.k

Kila wiki ni lazima nihesabu mzigo na kulinganisha na idadi ya mizigo iliyouzwa na hapo najua idadi inayotakiwa iwepo dukani.

Sasa wiki 3 zilizopita nlikuta utofauti wa mizigo ambayo ilikuwa haipatikani stoo ya kiasi cha elf 58 nikakaa na huyu muuzaji nikamwelewesha kwamba aandike kila kitu anachouza na akiona hela ya mauzo imezidi basi ni kwamba alisahau kuandika asifikiri ni muujiza akaenda kuipigia bata

wiki iliyopita nikaona material price variance (utofauti wa mizigo kwa gharama) ikiwa ni laki na 70, kwa kweli nlichukia sana na kwa vile mshahara wake ni laki 2 nikakata laki 1 nae asikie maumivu hio 70 nikampa onyo akirudia nakata yote.

Leo sasa nmehesabu mzigo nakuta variance imefika tena laki na 20

Nilipatwa na hasira nikawa naongea sauti ya juu kidogo bila kujijua dada akaanza kutoa machozi, nlipanga kumfukuza ila sikudhani itakuwa rahisi kiasi hiki.

Naombeni uzoefu wakuu, nlitaka nisingizie biashara ni yamjomba ili nimkodishe aje kumfukuza ila yup mbali sana

Inawezekana anaibiwa, hakikisha kabisa pasi nashaka kwamba anaiba na sio kwamba bila kujijua anakosea, pasi na Shaka....

Ukithibitisha tafuta namna ya kumpa ka likizo au vipi akifika huko mtext Acha naye, mie siwezi fukuza, ngumu sana, kuna mdada nilitaka mfukuza nikampa mshahara wa six months ili aende zake!

Ni ngumu sana!
 
Mkuu utafunga hiyo biashara muda si mrefu,na huo si huruma ni uzembe unaofanya

Muache; maisha yatamfunza. Hakuna tajiri mwenye roho nzuri. Ila wabongo hatunaga Mental strength, ni tatizo kubwa sana

Mk54
 
Weng hawajui chuma ulete ni janga kubwa sana limenitesa vibaya mno kila nkifikiria nliumia sana ..nlitakiwa niwe mbl sana lait ngemuwek mtu ningesema ananiibia

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu ukiwaambia wanaona Kama Hadithi..au hatuna shule.... lakini wangejua kua kuna wanaume wanapanda ndege kufuata chuma ulete Nigeria na Malawi na izo chuma ulete zinapitia mauzo kila duka na biashara ambazo hazina kinga na kuchukua hela..hii kitu mkuu nlipigwa adi nikaona dunia chungu .Tena nilipigwa hela ya mtaji +faida kubabake
 
Kodi vijana wawili.

Wavalishe minailoni. Wape na madumu ya fummigation.

Waagize waende kuspray.

Sema duka lina corona.

Anatakiwa apumzike.
 
"Nikadamka...." nilijua ni jina tu, kumbe ni kijana kutoka Mlogolo
Mi msichana nliemuweka dukani alifika hatua akawa anafungua duka muda anaotaka yeye.... nikamuonya mara 1, akajirekebisha km siku 2/3 akaanza tena.... nikamuonya mara ya 2... akajirekebisha km siku 2/3 akaanza tena... alijiamini akijua mimi nina kazi yng na duka liko wilaya nyingine huko.... sintajua....

Nilichukua likizo ya dharura ya wk 1 afu nikadamka dukani, nikafungua duka saa 12.45 Asub... saa 4 nikampigia kujua kama ameshafungua duka... akanambia ndio anafungua.... saa 5 anafika... kanikuta niko busy na wateja.... alichoka! Nikamlipa chake.... tukaagana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asikwambie mtu nlikuwa nadhani kufukuza mtu kazi kitu simpo, nshawahi kushuhudia jamaa yangu aliifata bodaboda yake stendi akamnyanganya funguo kijana anaeiendesha mbele ya umati mkubwa nidhani rahisi, Pia nliwahi kushuhudia mjomba wangu alimfukuza kijana aliekuwa akimsaidia kuuza duka, alimfukuwa wazi wazi bila kujali kijana ataenda wapi, nikadhani rahisi.

Nikiri tu maishani sijawahi kumfukuza mtu kwasababu hii ndio biasharara yangu mpya nliyofungua baada ya kushawishika niwe na vimiradi ukiachana na kazi yangu katika shirika la serikalini,

Nimefungua kamradi ka oili za magari zile oili za sevisi na vifaa muhimu vya sevisi n.k

Kila wiki ni lazima nihesabu mzigo na kulinganisha na idadi ya mizigo iliyouzwa na hapo najua idadi inayotakiwa iwepo dukani.

Sasa wiki 3 zilizopita nlikuta utofauti wa mizigo ambayo ilikuwa haipatikani stoo ya kiasi cha elf 58 nikakaa na huyu muuzaji nikamwelewesha kwamba aandike kila kitu anachouza na akiona hela ya mauzo imezidi basi ni kwamba alisahau kuandika asifikiri ni muujiza akaenda kuipigia bata

wiki iliyopita nikaona material price variance (utofauti wa mizigo kwa gharama) ikiwa ni laki na 70, kwa kweli nlichukia sana na kwa vile mshahara wake ni laki 2 nikakata laki 1 nae asikie maumivu hio 70 nikampa onyo akirudia nakata yote.

Leo sasa nmehesabu mzigo nakuta variance imefika tena laki na 20

Nilipatwa na hasira nikawa naongea sauti ya juu kidogo bila kujijua dada akaanza kutoa machozi, nlipanga kumfukuza ila sikudhani itakuwa rahisi kiasi hiki.

Naombeni uzoefu wakuu, nlitaka nisingizie biashara ni yamjomba ili nimkodishe aje kumfukuza ila yup mbali sana
Endelea kumuonea huruma utavuna mabua. Mimi nafukuza kila siku watumishi akikosea tu no mjadala anafungasha.

Usione Rais MagufuliJP ni mbaya kutumbua. Ni kazi ngumu sana kujenga mfumo huwezi jenga mfumo kwa kuonea huruma wazembe.

Ukiendelea naye utafunga biashara kabisa. You better fire and hire the new one Na mpe principles.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfanyakazi humwambii toka wemwambie biashara imekua ngumu alafu umebanwa kazini kwahyo unataka kuifunga keshokutwa kutokana nahii hali ya korona yeye atakuelewa atasepa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom