sijui nini
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 2,553
- 1,291
Nawashukuruni wana Jf woote kwa michango mbalimbali mnayotoa...baada ya kufatilia kwa kina juu ya michango inayotolewa na wadu mbalimbali nimeona leo na mimi nitoa langu lililo moyoni..OK, mimi nina mwanamke naishi naye (hatujafunga ndoa bado ila tunatagemea kufanya hivyo haraka iwezekanavyo) na tayari taratibu zoote zimeshaanza...tunapendana sana na tunaishi kwa furaha ukizingatia tunatarajia kupata mtoto mda si mrefu ujao..
Tatizo linalonikera ni kuna binti mmoja ambaye nilishawahi kuwa na mahusiano nae zamani (enzi tunasoma) lakini akawa ananiletea nyodo sana na baadae kunitema (alikuwa anaonyesha dalili zote kuwa kuna mwanaume mwingine alikuwa nae ingawa alikuwa anakana sana) na kweli baada ya kama mwaka mmoja hivi kupita nikjasikia kuwa amepata ujauzito kwa huyo mwanaume niliyekuwa namhisi..kipindi chote hicho tangu kanipiga chini tulikuwa hatuna mawasiliano yoyote mpaka alipokuja kujifungua ndo siku moja akanipigia simu na kujiongelesha pale yakaisha(enzi hizo mi niko zangu bize na chuo napiga mzigo)..baada ya muda tena kupita kimya kimya mamaake tena akanipigia simu kuniomba nimsaidie mwanae(huyo msichan aliyejifungua) kuhusumambo ya form za mikopo kwani alikuwa anataka kuendelea na chuo(wakati huo mi ndo nilikuwa namaliza so akajua nitakuwa nafahamu process zake)...basi mi sikuwa na kinyongo chochote..nikamsaidia mpaka akakamilisha na kwenda zake chuo huko Moro (mi nilikuwa UD).
Kuanzia hapo akawa anataka sana tuwe tunawasiliana kama marafiki wa kawaida (na kwa vile mi nilishaanza mipango yangu ya kumfukuzia huyu niliye nae saiz sikuona ishu maana moyo wangu ulishahama kabisa kwake) so tukawa tunawasiliana fresh tu ingawa mara chache alikuwa anajaribu kuchomekea mambo ya love ishuz lakini mi nikawa napotezea tu..kuna kipindi tukawa hata tunakutana nae kitaa (tunakaa karibu ofcoz na kozi aliyochukua chuoni inafanana na niliyochukua mimi so akawa anajaribu kuwa karibu sana ili nimsaidie - mi ndo nilivyokuwa naona) na pale nilipoweza kumsaidia nilifanya hivyo na pale niliposhindwa nilimpa live kuwa siwezi!
Sasa bwana tatizo likawa kila nikitoka kuwasiliana naye hivi mfano kwa simu basi baada ya muda huyo mshakaji wake anapiga au kutuma sms za matusi kwamba mi ni nani na natafuta nini kwa mkewe!? anatukana sana yaani mpaka nakereka..kuna kipindi niligoma kabisa kupiga/kupokea wala kumtumia sms yule msichana..siku moja akaja home nikampa ukweli na kumwambia mimi saiz nina mtu ambaye natarajia kuwa mke wangu pia so usumbufu huu sitaki..akapanick sana yule dada baada ya kujua nina mtu..akawa mara kwa mara anataka tuwasiliane(bahati nzuri nilishamueleza mwenzangu juu ya huyu msichana)..na sasa ikafika kipindi akawa ananionyesha wazi kuwa anataka turudiane(wakati nilishamueleza nina mtu)..wakati huo jamaa yake nae matusi kama kazi...siku moja ilibidi nimkalishe chini na kumuuliza juu ya huyo mtu anaenitusi vile, akasema ki ukweli na yeye amechoka na tabia yake hiyo na anafanya hivyo kwa kila mtu na anajuuuta kwa nini alizaa nae kwani hakuwa chaguo lake na mimi ndo chaguo lake..mi nikamwambia its too late kwanza nategemea kuitwa baba soon na hata ningekuwa bado nipo single kwa ulichonifanyia sidhani kama ningekupenda kama mwanzo..lakini yeye bado hataki kuelewa...kila siku meseji na simu(ingawa sipokei wala kujibu) lakini kialakituma sms mwanaume wake akiona tu ugomvi na nilisha mkataza sana kuhusu kuwasiliana na mimi lakini yeye anadai bado ananipenda...mke wangu(ninaeishi naye) anajua yoote hay lakini kuna kipindi huwa namuonea huruma kwa wasiwasi anaouonyesha (ingawa anadai ananiamini...ofcoz tunaaminiana sana na mke wangu) ila hii inazidi kipimo...naomba ushauriwenu...nim\fanyaje binti huyu jamani...!??