Binti mtaa wa 10 hivi toka hapa napoishi...mzuri na akili mkichwa si haba................Nimemuona mara kadhaa na kumtamani ingawa najua kidogokidogo naelekea kumpenda.
Hayo yote tisa, kumi anaonekana ni mtu anayehusudu vijana wenye lifestyle ya kisharobaro. Si kwamba ni malaya (angalau kwa uchunguzi wa awali) ila kutokana na maongezi ya hapa na pale, uvaaji wake, kuongea, muziki anaoupenda inaelekea ni mtu wa kuzimika na mwanaume wa aina hiyo.
Mimi ni kijana ingawa ni msikilizaji sana wa msondo, kupiga soga la kisiasa na mambo ya historia...bongofleva imenipitia kando kidogo. Uongeaji wangu wa kiutu-uzima japo naweza kuchomeka maneno machache ya "kimjini".
Sasa ombi wana MMU nipeni dondoo za kujibadilisha angalau kidogokidogo ili niwe na "swagger" za kisharobaro. Sitanii.
Wakatabahu
platozoom